Inawezekana kuna makosa katika kauli zake, hakuna asiyekosea, lakini wanaompinga wameenda mbali zaidi kuliko uhalisia
Lema kuwa karibu na labda kuwa kabila moja na Freeman Mbowe au labda wote kutoka kijiji kimoja isiwe sababu ya kushambuliwa kwake, tuko wengi tuliokuwa karibu na Mbowe nikiwemo mimi na wengine wengi mpaka Tundu Lissu, sasa kwa jambo hilo sidhani kama tunazuiliwa kutoa maoni
Wakosoaji wa Lema ni kama walisubiri akosee ili wamshambulie, kwamba walikuwa na madukuduku yao wakisubiri upenyo, hizo ni siasa za kishamba ambazo hazikubaliki, si kila mchaga lazima apigwe vita, siasa za ukabila ndani ya chadema hazikubaliki.
Kingine ni hiki, Lema hana uwezo wa kushawishi jambo kubwa ndani ya chama hata kama ni mjumbe wa kamati kuu, kwahiyo wenye mashaka naye ondoeni, hii kwa sababu hakuna lolote litafanyika kwa ushawishi wake.
Ifahamike kwamba mimi ni miongoni mwa wale wasiotaka maridhiano na Shetani, hilo kila mmoja wenu analifahamu, sasa kwa andiko hili isitafsiriwe kwamba naunga mkono jambo hilo
Niko Tayari kusahihishwa.
WABHILLAH TAWFIQ