Kuhusu Godbless: Napingana na wengi, siungi mkono mashambulizi dhidi yake

Kuhusu Godbless: Napingana na wengi, siungi mkono mashambulizi dhidi yake

Inawezekana kuna makosa katika kauli zake, hakuna asiyekosea, lakini wanaompinga wameenda mbali zaidi kuliko uhalisia

Lema kuwa karibu na labda kuwa kabila moja na Freeman Mbowe au labda wote kutoka kijiji kimoja isiwe sababu ya kushambuliwa kwake, tuko wengi tuliokuwa karibu na Mbowe nikiwemo mimi na wengine wengi mpaka Tundu Lissu, sasa kwa jambo hilo sidhani kama tunazuiliwa kutoa maoni

Wakosoaji wa Lema ni kama walisubiri akosee ili wamshambulie, kwamba walikuwa na madukuduku yao wakisubiri upenyo, hizo ni siasa za kishamba ambazo hazikubaliki, si kila mchaga lazima apigwe vita, siasa za ukabila ndani ya chadema hazikubaliki.

Kingine ni hiki, Lema hana uwezo wa kushawishi jambo kubwa ndani ya chama hata kama ni mjumbe wa kamati kuu, kwahiyo wenye mashaka naye ondoeni, hii kwa sababu hakuna lolote litafanyika kwa ushawishi wake.

Ifahamike kwamba mimi ni miongoni mwa wale wasiotaka maridhiano na Shetani, hilo kila mmoja wenu analifahamu, sasa kwa andiko hili isitafsiriwe kwamba naunga mkono jambo hilo

Niko Tayari kusahihishwa.

WABHILLAH TAWFIQ
Lema ni mlezi wa kichama kanda ya Kati kwanini kelele za Heche kula hela za tone tone zilianzia kanda ya kati baada ya Lema kufanya mikutano ?
 
Hivi haiwezekani kuishi Sea Cliff? Mimi nimekuwa nakula Karambezi Cafe kwa miaka, Sea Cliff mnaona ghali sana!
Ndo ukae miezi miwili mfululizo? Hongera umejipata ila siku unialike nisikae kinyonge.
 
Watu hubadilika..
Yawezekana mwanzoni alikuwa na nia ya dhati..
Hata Lissu alifuatwa na Abdul amhonge pesa, Lissu akakataa.. si kila mtu ana roho aliyonayo Lissu...

What's so special about Lema?
Si Mungu ana mapungufu pia.. Watu walivyompambania Wenje kwenye uchaguzi miaka ya 2010, kuna siku mtu angeamini jamaa akahamia CCM na kuanza kuwatukana wana CHADEMA?
Kwa logic hiyo hata Lissu sio mtu special. Aint he?
 
Watu hubadilika..
Yawezekana mwanzoni alikuwa na nia ya dhati..
Hata Lissu alifuatwa na Abdul amhonge pesa, Lissu akakataa.. si kila mtu ana roho aliyonayo Lissu...

What's so special about Lema?
Si Mungu ana mapungufu pia.. Watu walivyompambania Wenje kwenye uchaguzi miaka ya 2010, kuna siku mtu angeamini jamaa akahamia CCM na kuanza kuwatukana wana CHADEMA?
Mimi hata Lissu simuamini
 
Kama uko tayari kusahihishwa kama ulivyomalizia, basi kubali hapa umeanguka kwenye mtego wa double standards. Unatetea urafiki na ukaribu badala ya misingi ambayo Chadema imekuwa ikisimamia.
Chadema kama Vyama vingine vya siasa hakiendeshwi kwa misingi bali kwa hali ya kisiasa iliyopo wakati huo. Ndio maana viongozi waandamizi wa serikali na Chama cha Mapinduzi wamekuwa wakijiunga na Chadema na kupewa nafasi kubwa kubwa za uwakilishi.
 
Lema tatizo mienendo yake inatia shaka.. uki connect dots utagundua...

Lissu nina imani nae... Heche nina imani nae pia...

Lema ni mpenda sifa tu.. nabii uchwara..
Mbona Heche anamiliki vitu vingi tofauti na uhalisia wa kazi yake?
 
Inawezekana kuna makosa katika kauli zake, hakuna asiyekosea, lakini wanaompinga wameenda mbali zaidi kuliko uhalisia

Lema kuwa karibu na labda kuwa kabila moja na Freeman Mbowe au labda wote kutoka kijiji kimoja isiwe sababu ya kushambuliwa kwake, tuko wengi tuliokuwa karibu na Mbowe nikiwemo mimi na wengine wengi mpaka Tundu Lissu, sasa kwa jambo hilo sidhani kama tunazuiliwa kutoa maoni

Wakosoaji wa Lema ni kama walisubiri akosee ili wamshambulie, kwamba walikuwa na madukuduku yao wakisubiri upenyo, hizo ni siasa za kishamba ambazo hazikubaliki, si kila mchaga lazima apigwe vita, siasa za ukabila ndani ya chadema hazikubaliki.

Kingine ni hiki, Lema hana uwezo wa kushawishi jambo kubwa ndani ya chama hata kama ni mjumbe wa kamati kuu, kwahiyo wenye mashaka naye ondoeni, hii kwa sababu hakuna lolote litafanyika kwa ushawishi wake.

Ifahamike kwamba mimi ni miongoni mwa wale wasiotaka maridhiano na Shetani, hilo kila mmoja wenu analifahamu, sasa kwa andiko hili isitafsiriwe kwamba naunga mkono jambo hilo

Niko Tayari kusahihishwa.

WABHILLAH TAWFIQ
Tatizo la wanaharakati wanajifanya sana wao ni watakatifu! Hivi mtu muovu akifiwa, akipewa pole kuna shida gani?
Yaani Lissu au Lema kutoa pole kwa muuaji ni tatizo?
Hivi siku upinzani wakichukua madaraka wanataka kutuaminisha kuwa watakuwa hawahudhurii kwenye misiba ya wapinzani wao?

Njia pekee ya kuondoa uovu si kuukoleza uovu zaidi!
Muovu atendewe kwa huruma ili aoneshwe utofauti!
Mange Kimambi, Maria Sarungi, Hilda Newton na wanaharakati wengine wajifunze kufanya siasa zenye kujali utu hata wa wale wanaowadhulu haki zao!
Nchi ni ya wote, waovu na wao "wasiokuwa" waovu!
 
Back
Top Bottom