Kuhusu Godbless: Napingana na wengi, siungi mkono mashambulizi dhidi yake

Lema tatizo mienendo yake inatia shaka.. uki connect dots utagundua...

Lissu nina imani nae... Heche nina imani nae pia...

Lema ni mpenda sifa tu.. nabii uchwara..
For now just keep connecting the dots... Kama yupo hivyo ni suala la muda tu! Tatizo lenu mnashindwa kufanya timing hadi mnawashtusha hao mnaowafuatilia!
Mbona kwa Mbowe yanaendelea kutimia? He is more associated with SSH than TAL!
 
Inanikumbusha tukio la Aldrich Ames... Miaka ya 1980s..

Alikuwa mkuu wa kitengo cha ujasusi dhidi ya Wasovieti, KGB, ndani ya shirika la CIA. Kazi yake ilikuwa kuajiri majasusi wa Urusi waifanyie kazi Marekani, ama watoe siri za Wasovieti..

Ames akapata shida za kifedha na madeni.. Yeye mwenyewe akaanza kuuza siri kwa KGB... Majasusi wa kirusi waliokuwa wakiifanyia kazi CIA wakaanza kuuawa huko Russia...

CIA wakafahamu kuna mchwa miongoni mwao lakini hawakufahamu ni nani haswa...

Ames alikuwa analipwa $60K kwa mwaka kama wafanyakazi wengine wa serikali..
Ghafla jamaa maisha yake yalibadilika akaanza kuishi maisha ya kifahari, akanunua gari la kifahari na nyumba karibu ya usd 500K .. alipoulizwa akasema mke wake anatokea familia ya kitajiri nchini Cambodia....

Alikamatwa 1994, ilibidi FBI waanze kufuatilia mienendo yake , wakifuatilia hadi kwenye dustbin nyumbani kwake na kukuta karatasi zilizochanwa zimeandikwa kwa codes... jamaa alifungwa maisha...

Hivyo kwenye ku connect dots huwa haidanganyi...
Na pia instincts zikikuambia kuna jambo halipo sawa inabidi uzingatie...

Mienendo ya Lema inatia shaka....
 
siasa zenye kujali utu
Unaona siasa za CCM ni zenye kujali utu?

Kuua , kufira, kubambika kesi, kuteka ndizo siasa zenye utu....

Msiba wa Ali Kibao huyo mfiwa alisemaje? Alisema kifo ni kifo tu..
Mauaji ya 29 Oct, alijibu nguvu iliyotumika ilikuwa sahihi..

Umeona hata mwenye video eneo la tukio Mdude Nyagali alitekwa? Ule ndio utu?

Unachozungumza ni toxic positivity, kauli za kutiana moyo hata katika nyakati ngumu za kufanya maamuzi magumu na yenye uhalisia , unachosema hakuna uhalisia hapo kwamba anayekufanyia mabaya wewe mtendee wema...
 
Inawezekana kuna makosa katika kauli zake, hakuna asiyekosea, lakini wanaompinga wameenda mbali zaidi kuliko uhalisia

Lema kuwa karibu na labda kuwa kabila moja na Freeman Mbowe au labda wote kutoka kijiji kimoja isiwe sababu ya kushambuliwa kwake, tuko wengi tuliokuwa karibu na Mbowe nikiwemo mimi na wengine wengi mpaka Tundu Lissu, sasa kwa jambo hilo sidhani kama tunazuiliwa kutoa maoni

Wakosoaji wa Lema ni kama walisubiri akosee ili wamshambulie, kwamba walikuwa na madukuduku yao wakisubiri upenyo, hizo ni siasa za kishamba ambazo hazikubaliki, si kila mchaga lazima apigwe vita, siasa za ukabila ndani ya chadema hazikubaliki.

Kingine ni hiki, Lema hana uwezo wa kushawishi jambo kubwa ndani ya chama hata kama ni mjumbe wa kamati kuu, kwahiyo wenye mashaka naye ondoeni, hii kwa sababu hakuna lolote litafanyika kwa ushawishi wake.

Ifahamike kwamba mimi ni miongoni mwa wale wasiotaka maridhiano na Shetani, hilo kila mmoja wenu analifahamu, sasa kwa andiko hili isitafsiriwe kwamba naunga mkono jambo hilo

Niko Tayari kusahihishwa.

WABHILLAH TAWFIQ
Chadema inabidi kuwa makini sana. Inaelekea kuna mpango wa kudhoofisha chama chenu kwa kuwaondoa wale wote wenye experience ya siasa za upinzani. Sio tu Lema, Boni na Sugu pia wametajwa kuwa ni wasaliti wa Chadema. Watu kama Boni na Sugu wana base ambayo itamchukua mtu mgeni muda mrefu kuweza kuijenga. Kwa mawazo yangu, kwa sasa hivi, Chadema ina watu wachache sana wenye mvuto wa kitaifa au hata wa kijimbo.

Majuzi nilimsikia Lissu akiuliza mbona kuna watu wachache Mahakamani. Hiyo hali sio nzuri.

Amandla...
 
Mali nyingi kama zipi?
Ungekuwa na data kamili, na data za kipato kwenye kazi yake nadhani unge eleweka...

Suala ni mienendo...
Mienendo ya Lema inatia shaka...
Wakiwepo watu waaminifu hii ndo furaha yetu Watanganyika.
Waendelee kua na mioyo safi hivyohivyo.
 
Chadema inabidi kuwa makini sana. Inaelekea kuna mpango wa kudhoofisha chama chenu kwa kuwaondoa wale wote wenye experience ya siasa za upinzani. Sio tu Lema, Boni na Sugu pia wametajwa kuwa ni wasaliti wa Chadema. Watu kama Boni na Sugu wana base ambayo itamchukua mtu mgeni muda mrefu kuweza kuijenga. Kwa mawazo yangu, kwa sasa hivi, Chadema ina watu wachache sana wenye mvuto wa kitaifa au hata wa kijimbo.

Majuzi nilimsikia Lissu akiuliza mbona kuna watu wachache Mahakamani. Hiyo hali sio nzuri.

Amandla...
Hili la CHADEMA kutokuwa na watu wengi wenye mvuto mimi nalichukulia kama positive (iwapo ni kweli kama unavyosema), Hii maana yake ni kwamba wananchi wanajali chama kuliko watu, na ndiyo maana ukipitishwa mchango watu wananchanga. Au mikutano inajaa mpaka serikali inapiga marufuku haramu. Hii inafanya kila kiongozi awe humble, ajue CHADEMA siyo yeye, Kumbuka CHADEMA ilihi kukimbiwa na watu wengi tu maarufu kama Dr Sla, Mbowe, Msigwa, mzee Mdee etc lakini bado inaendelea kutikisa,
 
Inawezekana kuna makosa katika kauli zake, hakuna asiyekosea, lakini wanaompinga wameenda mbali zaidi kuliko uhalisia

Lema kuwa karibu na labda kuwa kabila moja na Freeman Mbowe au labda wote kutoka kijiji kimoja isiwe sababu ya kushambuliwa kwake, tuko wengi tuliokuwa karibu na Mbowe nikiwemo mimi na wengine wengi mpaka Tundu Lissu, sasa kwa jambo hilo sidhani kama tunazuiliwa kutoa maoni

Wakosoaji wa Lema ni kama walisubiri akosee ili wamshambulie, kwamba walikuwa na madukuduku yao wakisubiri upenyo, hizo ni siasa za kishamba ambazo hazikubaliki, si kila mchaga lazima apigwe vita, siasa za ukabila ndani ya chadema hazikubaliki.

Kingine ni hiki, Lema hana uwezo wa kushawishi jambo kubwa ndani ya chama hata kama ni mjumbe wa kamati kuu, kwahiyo wenye mashaka naye ondoeni, hii kwa sababu hakuna lolote litafanyika kwa ushawishi wake.

Ifahamike kwamba mimi ni miongoni mwa wale wasiotaka maridhiano na Shetani, hilo kila mmoja wenu analifahamu, sasa kwa andiko hili isitafsiriwe kwamba naunga mkono jambo hilo

Niko Tayari kusahihishwa.

WABHILLAH TAWFIQ
"Ukiisha kula nyama ya mtu mara ya kwanza, huwezi kuacha"! Mwl. Nyerere.
 
Lema alishangaza alipoanza kucheza script za Lumumba mara "mama " sijui upendo "utawale"

Mara Heche kapata passport yake kwa njia za panya hii michezo walianza vibaka wa Lumumba waliojificha Chaumma wakiongozwa na Yericko Nyerere sasa leo ushahidi wa jinsi passport ile imepatikana umemuachia aibu.

Aombe radhi atulie pengine watu washashtukia moves zake arudi nyuma ajisahihishe.

Mange Kimambi amejijengea jina hasa kutokana na credibility ya taarifa zake sio kama Maria Sarungi , Mange akishusha bomu linakua bomu ndio maana hata kule Meta waliona ana coverage wakaona wampunguze upepo na sio kwamba hawezi kufungua account mpya ni kwamba akijaribut tu wanampa ban maana wamempa ban ya kudumu sio kwamba hawajui CCM wanamjua nani ni hatari zaidi katika harakati zao chafu tafakari hayo.
 
Chadema inabidi kuwa makini sana. Inaelekea kuna mpango wa kudhoofisha chama chenu kwa kuwaondoa wale wote wenye experience ya siasa za upinzani. Sio tu Lema, Boni na Sugu pia wametajwa kuwa ni wasaliti wa Chadema. Watu kama Boni na Sugu wana base ambayo itamchukua mtu mgeni muda mrefu kuweza kuijenga. Kwa mawazo yangu, kwa sasa hivi, Chadema ina watu wachache sana wenye mvuto wa kitaifa au hata wa kijimbo.

Majuzi nilimsikia Lissu akiuliza mbona kuna watu wachache Mahakamani. Hiyo hali sio nzuri.

Amandla...
Wanaotoa maoni ya usaliti siyo CHADEMA ni mahasimu wao wanaotumia fursa zinazotengenezwa na CHADEMA
CHADEMA unaweza kuona wanajibishana lakini ukweli ni kwamba wapo CHADEMA wanaojibishana na CCM

Issue ya Tone tone ilishikiwa Bango hadi akina Mwashamba na wenzake kuliko CHADEMA wenyewe
Issue ya Passport imeshikiwa bango hadi na mawakili kuliko CHADEMA wenyewe

Unajua lengo ni Heche tu waweze kupata 'puppet'' ili kupiga picha na kupoteza muda kama walivyomtenda Mbowe. Jiulize kwanini CCM wanachukizwa na kinachoitwa ''Ufisadi'' ndani ya CHADEMA kuliko eneo jingine lolote

Tatizo la CHADEMA ni haya ya kusema hovyo bila kujali madhara yake. Mfano, tone tone Lema alitajwa sana na hakuwahi kutoka kukanusha au kufafanua. CCM wakaidaka na kuitumia fursa!

Juzi Lema anaulizwa passport yake ana insinuate ya Heche na usalama wa Taifa! kulikuwa na ulazima gani na sasa imebainika si kweli, je amesaidia vipi Chama chake. CCM na Mawakili wanaitumia dhidi ya Makamu na Lissu

Kuhusu rambi rambi, Lema ana uhuru wa maoni. Hata hivyo lazima aangalie nyakati. Mfano, alipofariki dereva wa Heche katika mazingira tata, Lema alikuwa wapi kuandika bandiko la faraja kwa Familia na Chama chake!
Ni wapi CCM walitoa salam za rambi rambi kwa tukio hilo!

Na kubwa ni la kuunganisha kauli za Mwenyekiti na rambi rambi. Lema alipaswa kuelewa nyakati na atmosphere iliyopo. Angeweza kwenda kutoa pole zake bila kuleta sintofahamu.

Ni lazima atenganisha personal affairs na public affairs na aweze kusoma public mood.

Kwa hili, Lema ameshiriki kuvuruga Chama chake. Zama za wanasiasa wakongwe anapaswa akae pembeni. Tuchukulie mfano wa Marehemu Ndugai! CCM walimuondoa ili kuokoa taswira ya chama chao

Sidhani kama Lema ana vote of confidence katika Kamati kuu na public in general
Kama ana good will na Chama chake, it's time to resign abaki mwanachama.

JokaKuu Kalamu
 
Inawezekana kuna makosa katika kauli zake, hakuna asiyekosea, lakini wanaompinga wameenda mbali zaidi kuliko uhalisia

Lema kuwa karibu na labda kuwa kabila moja na Freeman Mbowe au labda wote kutoka kijiji kimoja isiwe sababu ya kushambuliwa kwake, tuko wengi tuliokuwa karibu na Mbowe nikiwemo mimi na wengine wengi mpaka Tundu Lissu, sasa kwa jambo hilo sidhani kama tunazuiliwa kutoa maoni

Wakosoaji wa Lema ni kama walisubiri akosee ili wamshambulie, kwamba walikuwa na madukuduku yao wakisubiri upenyo, hizo ni siasa za kishamba ambazo hazikubaliki, si kila mchaga lazima apigwe vita, siasa za ukabila ndani ya chadema hazikubaliki.

Kingine ni hiki, Lema hana uwezo wa kushawishi jambo kubwa ndani ya chama hata kama ni mjumbe wa kamati kuu, kwahiyo wenye mashaka naye ondoeni, hii kwa sababu hakuna lolote litafanyika kwa ushawishi wake.

Ifahamike kwamba mimi ni miongoni mwa wale wasiotaka maridhiano na Shetani, hilo kila mmoja wenu analifahamu, sasa kwa andiko hili isitafsiriwe kwamba naunga mkono jambo hilo

Niko Tayari kusahihishwa.

WABHILLAH TAWFIQ
Na ametangaza press conference kesho sasa sijui kila mwanachama wa chadema anaweza kutoa press conference tu au kuna utaratibu gani mkuu
 
Ni haki yake...

Mwache aongee, huenda tulimuelewa vibaya kesho akarekebisha...

Press conference wanafanya hadi watu duni kama Mwaipopo...

Ni haki ya kila ntu.
 
Lema alishangaza alipoanza kucheza script za Lumumba mara "mama " sijui upendo "utawale"

Mara Heche kapata passport yake kwa njia za panya hii michezo walianza vibaka wa Lumumba waliojificha Chaumma wakiongozwa na Yericko Nyerere sasa leo ushahidi wa jinsi passport ile imepatikana umemuachia aibu.

Aombe radhi atulie pengine watu washashtukia moves zake arudi nyuma ajisahihishe.

Mange Kimambi amejijengea jina hasa kutokana na credibility ya taarifa zake sio kama Maria Sarungi , Mange akishusha bomu linakua bomu ndio maana hata kule Meta waliona ana coverage wakaona wampunguze upepo na sio kwamba hawezi kufungua account mpya ni kwamba akijaribut tu wanampa ban maana wamempa ban ya kudumu sio kwamba hawajui CCM wanamjua nani ni hatari zaidi katika harakati zao chafu tafakari hayo.
Ni sahihi mkuu..
Halafu ushenzi wote alikuwa anaanza chinichini..

Sema wamemstukia mapema...
 
Back
Top Bottom