Sijui kama mtoa mada ushaweka huo mfumo au ulighairi. Kabla hujafunga, nenda pale DIT onana na mtu anaitwa Gurti. Ndiye mtaalamu wa huu mfumo. Mtashauriana kabla hujaamua la kufanya.
Unapofunga huu mfumo, hakikisha plugs zako ni original. Pia zipo plugs maalumu kwa CNG. Plugs zinazoendana na CNG ni za NGK. Sio zile za sindano. Badala ya kufunga plugs za 8000, heri ukanunua plugs used zilizokuja na injini za mtumba kule Ilala. Hizo zinahimili 'muziki' wa gesi.
Baadhi husema gesi inaua sana plugs na coils. Hizo hufa hata unapotumia petroli pekee.
Hakikisha ignition coils ziwe original. Hata ikifa, nunua original. Gesi haipatani na plugs au coils za mchina. Utapata misfire zisizoisha. Utafunga leo, kesho imekufa.
Kwa muda wa miezi 6 ambayo nimetumia gari yenye gesi, sijajutia kuweka huo mfumo. Nishakutana na Subaru Impreza na Forester kwenye kujaza gesi. Pia nimekutana na Harrier, Vanguard, X-Trail, Juke, Outlander, Prado, daladala za Nissan Caravan, n.k.
Ni kweli, kuna power loss kwa asilimia fulani hasa kwenye miinuko. Ukifika eneo hili unabonyeza kitufe cha kuhamia kwenye petroli. Ila kwenye flat surface, iko vzr. Kwa mwezi natumia elfu 30 tu ya petroli kwa ajili ya kuwashia gari (gari huwaka kwa petroli kwanza kabla haijahamia kwenye gesi automatically).
Mfumo wa gesi una ECU yake na unakuwa programmed pale gari inapokuwa kwenye mwendo. ECU yale inakuwa connected na laptop, fundi anaingia nayo barabarani anai-programme ktk vipimo sahihi kwenye kiasi cha gesi kitumikacho, power, air intake, idle control valve, na mengineyo.
Kingine cha kuzingatia ni engine oil level. Ikipungua sana, gari hukosa nguvu.
Ninaishi 30km kutoka kazini. Kwa siku ni 60km. Nikitumia petroli, natumia elfu 30 kwa siku. Ila gesi ya elfu 23 ninatumia siku 3 na nusu hadi nne. Wiki hii nikijaza mara 2, wiki ijayo najaza mara moja kwani ile ya mara ya pili hunipa hata siku 2 za wiki ya pili.
Barabara nyingi za Dar kwa sasa hazikupi nafasi ya kuendesha 80kph hata kwa dk5. Foleni kila mahali. Uamuzi ni wako.