Ahadi ya Iran ya kulipiza kisasi dhidi ya Israel kwa mauaji ya kiongozi wa kisiasa wa Hamas Ismail Haniyeh mjini Tehran itachukua muda, kwa mujibu wa msemaji wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini humo (IRGC).
"Wakati upo upande wetu na muda wa kusubiri majibu haya huenda ukaongezwa,” Ali Mohammad Naeini alinukuliwa akisema Jumanne na vyombo vya habari vya serikali.
Mashariki ya Kati imekuwa katika hali ya tahadhari tangu mwezi uliopita kufuatia mauaji ya Ismael Haniyeh huko Tehran, ambayo yalikuja siku moja baada ya kamanda wa Hezbollah Fu'ad Shukr naye kuuawa katika shambulio la anga huko Beirut.
https://www.cnn.com/2024/08/20/middleeast/iran-israel-irgc-comments-intl/index.html