Pre GE2025 Kuhusu kupokea fedha za Abdul, kutoka kwa Lissu kuna ukweli kidogo na uongo mwingi

Pre GE2025 Kuhusu kupokea fedha za Abdul, kutoka kwa Lissu kuna ukweli kidogo na uongo mwingi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Alimpa Abduli rushwa ya sh ngapi ili apate fadhila yake?
Kwani rushwa ni lazima kutoa?

Tundu Lissu alitaka kupokea rushwa ya fadhila kutoka kwa Abdul, ili Tundu Lissu apate haki yake.

Kupata fadhila kutoka kwa Abdul ili upate haki yako nje ya process husika ni rushwa. Ni rushwa ya fadhila.

Huelewi wapi?
 
Nikiandika utaweza kusoma?

Rushwa ni kitendo cha kutoa, kupokea, au kuomba pesa, kitu cha thamani au fadhila ili kuathiri mambo fulani ya kumpatia mtu faida isiyo ya haki kutoka kwa mtu mwingine anayesimamia au mwenye ukaribu na wanaosimamia mambo ya kijamii na kumfanya mtu kufanya mambo kinyume na haki, wajibu na kanuni za uwazi na uthabiti wa uadilifu.

Rushwa si lazima iwe pesa, inaweza kuwa ya ngono, adhila etc.

Tundu Lissu akikataa rushwa ya pesa, akakubali rushwa ya fadhila.

Hujapangua hii hoja.
Katika maelezo yako hapo kuhusu maana ya rushwa ha apo uliposema "kumpatia mtu faida isio ya haki" hapo Liasu anapata faida gani isio ya haki?
 
i dont beleive it, if that was the case asinge announce publick like that knowing itamchafua, not his fan but kusema alikubali aina ya rushwa akaacha pesa no such thing, lissu huyu aliekuwa akichangiwa pesa ya kununua gari?
Kutangaza public kunaonesha Lissu pengine hakuwa na nia mbaya, alifanya "in good faith", au alijiona ana haki ya kupata fadhila ili kupata haki yake.

Lakini, kujiona una haki ya kupatq fadhila ili upate haki yako, kama kupata fadhila hivyo ni rushwa, hakuondoi rushwa.

Swali la msingi hapa ni hili.

Kupata fadhila ili uoate haki yako ni rushwa au si rushwa?

Mfano tuseme kuna nafasi ya kazi ambayo ni haki ya kila mwenye degree kupata nafasi kufanya, akaja dada mmoja ana degree akatoa ngono (rushwa ya fadhila) ili apendelewe apate nafasi ya kufanya hiyo kazi.

Hapo utasema hiyo ngono si rushwa kwa sababu huyo dada ana degree na kufanya hiyo kazi ni haki yake?

Hiyo ngono ni rushwa, kwa sababu imempa unfair advantage dhidi ya wengine.

Tundu Lissu alitakiwa ku deal na mfumo kupata haki yake, bika kutafuta kubebwa na kina Abdul na Samia.

Kuingia kwenye favirs za kina Abdul na Samia ni rushwa kama rushwa na pesa tu, ila imewekwa ki fadhila zaidi.
 
Mwandishi umeandika mengi lakini unatulazimisha wasomaji wako tusihoji negativity za Wenje na unatutaka tuone Lissu ana shida ila Wenje alikua na nia njema. Yaani maandishi yako yapo bias, tayari umechagua upande. Wasomaji wako tuna uhuru wa ku question pia credibility yako kwenye hili SAGA la rushwa
 
Kwani rushwa ni lazima kutoa?

Tundu Lissu alitaka kupokea rushwa ya fadhila kutoka kwa Abdul, ili Tundu Lissu apate haki yake.

Kupata fadhila kutoka kwa Abdul ili upate haki yako nje ya process husika ni rushwa. Ni rushwa ya fadhila.

Huelewi wapi?

Fadhila gani kwenye kumtuma mtu apeleke mafaili ili alipwe haki yake?

Kwenye kumpa nyaraka, Lissu alimgeuza Abduli kama Tarishi tu wa kupeleka nyaraka zake.

Naamini Abduli alizipeleka kwa utaratibu unaotakiwa kisheria. Kama hakufanya hivyo basi amrudishie Lissu nyaraka zake ili Lissu amtume mtu mwingine ampelekee.
 
Katika maelezo yako hapo kuhusu maana ya rushwa ha apo uliposema "kumpatia mtu faida isio ya haki" hapo Liasu anapata faida gani isio ya haki?
Lissu anapata faida isiyo ya haki kwa sababu anaruka mstari wa process halali ya kupata fidia yake ya haki. Anatumia nafasi yake ya kisiasa kama mpinzani mahiri kujipatia faida binafsi ambayo wananchi wa kawaida hawawezi. Hapo hakuna usawa wala haki. Kuna mchezo wa kupeana fadhila kwa kujuana.

Abdul alitaka kumhonga Tundu Lissu pesa ili Tundu Lissu asimsakame rais Samia. Lissu akakataa pesa, lakini akakubali rushwa ya fadhila. Abdul bado alikuwa na expectations kuwa akitimiza upande wake, Lissu naye atatimiza upande wake kuacha kumsakama sana Samia. Suala la pesa au fadhila ni namna tu ya malipo, ila rushwa bado iko pale pale.

Kuna wazee wengi wanadai fidia zao, mafao yao, wamekaa kwenye mstari miaka mingi. Hawajuani na Abdul wala Samia, si wanasiasa. Wanasota.

Tundu Lissu alitakiwa kupigania haki kwa wote, atatue matatizo ya kimfumo.

Tundu Lissu kutaka kutatua tatizo lake yeye tu, kwa fadhila za Abdul na Samia kuruka mfumo rasmi, tena baada ya Abdul kutaka kumhonga pesa ili Tundu Lissu asimseme mama yake Abdul rais Samia ni vibaya, ni kukubali rushwa ya fadhila.

Tundu Lissu alikataa rushwa ya pesa, akakubali rushwa ya fadhila za Abdul.

Rushwa si lazima iwe ya pesa, hata fadhila ya kukurusha mstarini ili kukurahisishia kupata haki yako ni rushwa.

Fadhila hii ingempa Tundu Lissu advantage ambayo watu wasiojuana na Abdul na Samia hawana.

Hili ni tatizo kubwa Tanzania. Kila mtu anataka awe na mtu wake kwenye kila ofisi ili mambo yaende, hakuna mtu anayetaka kutatua matatizo ya kimfumo ili watu wapate huduma kwa haki bila hata ya kujuana na mtu.

Tundu Lissu kama mtu anayesimamia haki na usawa, alitakiwa ajue kuwa kutumia fadhila za Abdul ili arahisishiwe kupata haki yake ni rushwa.
 
Mbona watanzania hamjipi muda wakutafakari jambo kwakina Kisha uje na hoja mjarabu mleta hoja kajitahidi kuelekea Lile anafahamu KUU ya sakata la fedha Za Abdul alafu wewe unakoment kwamba eti pumba haya wewe tupe basi Michele ili tulinganishe pumba zake na Michele wako
 
Fadhila gani kwenye kumtuma mtu apeleke mafaili ili alipwe haki yake?

Kwenye kumpa nyaraka, Lissu alimgeuza Abduli kama Tarishi tu wa kupeleka nyaraka zake.

Naamini Abduli alizipeleka kwa utaratibu unaotakiwa kisheria. Kama hakufanya hivyo basi amrudishie Lissu nyaraka zake ili Lissu amtume mtu mwingine ampelekee.
Kuna process ya Tundu Lissu kupata haki yake.

Process hiyo haimhusishi Abdul wala Samia.

Abdul na Samia wanatumika kumrusha Tundu Lissu kwenye foleni ndefu ya kupata haki yake.

Hii fadhila ya kumrusha Tundu Lissu kwenye mstari halali wa kupata haki yaje ndiyo rushwa, rushwa ya fadhila.

Rushwa si lazima iwe ya pesa, ukipewa unfair advantage nayo ni rushwa.

Kumrusha Lissu apate haki yake kwa kutumia jina la Samia ni kumpa unfair advantage.

Si kila mtu anamjua Samia na Abdul.

Kuna wazee wanadai mafao yao tangu enzi za East African Harbours Authority hawajalipwa mpaka leo.

Hawa hawajuani na Samia wala Abdul.

Tanzania kuna utamaduni mbaya sana wa kila mtu akitaka kufanya jambo ofisi fulani lazima awe na mtu wake kwenye ofisi hiyo. Kupewa fadhila na mtu wake, badala ya kufuata process ya haki isiyohitaji fadhila ya mtu yeyote.

Nilitegemea Tundu Lissu, mpigania haki na usawa, akatae mfumo huu wa watu kupata haki zao kwa fadhila za kujuana, apambanie watu kupata haki zao kwa kutumia mfumo, bila kujuana.

Lakini ameshindwa mtihani huu.

Ametaka kutumia kujuana ili apate haki yake.

Hiyo ni rushwa ya fadhila.

This was a wasted opportunity for Tundu Lissu to make this a cause and help so many people.
 
Lissu anapata faida isiyo ya haki kwa sababu anaruka mstari wa process halali ya kupata fidia yake ya haki. Anatumia nafasi yake ya kisiasa kama mpinzani mahiri kujipatia faida binafsi ambayo wananchi wa kawaida hawawezi. Hapo hakuna usawa wala haki. Kuna mchezo wa kupeana fadhila kwa kujuana.

Abdul alitaka kumhonga Tundu Lissu oesa ili Tundu Lissu asimsakame rais Samia. Lissu akakataa pesa, lakini akakubali rushwa ya fadhila. Abdul bado alikuwa na expectations kuwa akitimiza upande wake, Lissu naye atatimiza upande wake kuacha kumsakama sana Samia. Suala la oesa au fadhula ni namna tu ya malipo, ila rushwa bado iko pale pale.

Kuna wazee wengi wanadai fidia zao, mafao yao, wamekaa kwenye mstari miaka mingi. Hawajuani na Abdul wala Samia, si wanasiasa. Wanasota.

Tundu Lissu akitakiwa kupigania haki kwa wote, atatue matatizo ya kimfumo.

Tundu Lissu kutaka kutatua tatizo lake yeye tu, kwa fadhila za Abdul na Samia kuruka mfumo rasmi, tena baada ya Abdul kutaka kumhonga pesa ili Tundu Lissu asimseme mama yake Abdul rais Samia vibaya, ni kukubali rushwa ya fadhila.

Tundu Lissu alikataa rushwa ya oesa, akakubali rushwa ya fadhila za Abdul.

Rushwa si lazima iwe ya pesa, hata fadhila ya kukurusha mstarini ili kukurahisishia kupata haki yako ni rushwa.

Fadhila hii ingempa Tundu Lissu advantage ambayo watu wasiojuana na Abdul na Samia hawana.

Hili ni tatizo kubwa Tanzania. Kika mtu anataka awe na mtu wake kwenye kika ofisi iki mambo yaende, hakuna mtu anayetaka kutatua natatizo ya kimfumo ili watu waoate huduma kwa haki bila hata ya kujuana na mtu.

Tundu Lissu kama mtu anayesimamia haki na usawa, alitakiwa ajue kuwa kutumia fadhika za Abdul ili arahisishiwe kuoata haki yake ni rushwa.
Usinichoshe na upumbavu wako.
 
Maridhiano yalifungua milango na madirisha, hivyo kuruhusu hewa mpya kuingia.
Hii sio kweli!
mikutano ya hadhara ilifunguliwa, waliokuwa wamekimbia nchi, walirejea. Unawezaje kumsimanga?
Mkuu mikutano ya kisiasa ni haki ya kikatiba sio zawadi, Hapa mbowe anashukuru kupewa haki yake ya kikatiba kama zawadi?
Je, alilamba asali ili aachiwe huru na kuunga mkono maridhiano?
Probably
Hivyo, inaleta ukakasi kuona Serikali bado inadaiwa fedha za matibabu ya Lissu.
Mkuu Fedha za Wananchi sio Fedha za Serikali, Bado ana haki ya kudai Fedha zake kwa sababu alikuwa mtumishi wa Serikali
Lissu anataka apewe fedha za matibabu ambayo ameshalipiwa na Watanzania?
The same logic as above
Nilimsikia Wenje akisema fedha za matibabu ya Lissu zinamhusu kwa sababu naye kuna za kwake
Lissu amesema Wenje hamdai hata mia Mbovu!
 
Lissu hakukataa hongo.

Alikataa hongo ya pesa akakubali hongo ya fadhila ya Abdul kumsaidia apate mafao yake.

Kwa maneno yake mwenyewe.

That was influence peddling.

Lissu should do better than that.
Lisu amejichanganya,na hana mwendelezo wa tuhuma anazodai.Ukiangalia mambo mengi anayosema hayana ushahidi.
 
Kuna process ya Tundu Lissu kupata haki yake.

Process hiyo haimhusishi Abdul wala Samia.

Abdul na Samia wanatumika kumrusha Tundu Lissu kwenye foleni ndefu ya kupata haki yake.

Hii fadhila ya kumrusha Tundu Lissu kwenye mstari halali wa kupata haki yaje ndiyo rushwa, rushwa ya fadhila.

Rushwa si lazima iwe ya pesa, ukipewa unfair advantage nayo ni rushwa.

Kumrusha Lissu apate haki yake kwa kutumia jina la Samia ni kumpa unfair advantage.

Si kila mtu anamjua Samia na Abdul.

Kuna wazee wanadai mafao yao tangu enzi za East African Harbours Authority hawajalipwa mpaka leo.

Hawa hawajuani na Samia wala Abdul.

Tanzania kuna utamaduni mbaya sana wa kila mtu akitaka kufanya jambo ofisi fulani lazima awe na mtu wake kwenye ofisi hiyo. Kupewa fadhila na mtu wake, badala ya kufuata process ya haki isiyohitaji fadhila ya mtu yeyote.

Nilitegemea Tundu Lissu, mpigania haki na usawa, akatae mfumo huu wa watu kupata haki zao kwa fadhila za kujuana, apambanie watu kupata haki zao kwa kutumia mfumo, bila kujuana.

Lakini ameshindwa mtihani huu.

Ametaka kutumia kujuana ili apate haki yake.

Hiyo ni rushwa ya fadhila.

This was a wasted opportunity for Tundu Lissu to make this a cause and help so many people.

Lete ushahidi kuwa Abduli hakuzipeleka Nyaraka za Abduli katika ngazi husika!

Maana ili rais asaini pesa za Lissu zitoke lazima ziwepo signatures nyingi za watu wa chini kila mtu kwa nafasi yake kwa mujibu wa sheria!

Hata kama Abduli atabeba nyaraka za Lissu na kuzipeleka Ikulu ofisini kwa mama yake hawezi kuzisaini mpaka watu wote wanaotakiwa kusaini wasaini. Na ikifanyika hivyo maana yake utaratibu utafuatwa tu.

Kumbuka, Rais (kwa kuvunja sheria) anaweza kuamuru Lissu alipwe bila hata kupeleka nyaraka yeyote, ikifanyika hivyo hayo madai yako yanapata uhalali kwa mbaaali. Lakini as long as Abduli atabeba nyaraka na kuzipeleka katika ngazi husika hatua kwa hatua mpaka zifike kwa mama yake, hiyo sisi tunaita bahati ya Lissu kupata tarishi wa kumfanyia kazi yake kwa ufanisi!
 
Lisu amejichanganya,na hana mwendelezo wa tuhuma anazodai.Ukiangalia mambo mengi anayosema hayana ushahidi.
Kwenye ushahidi ni vigumu kujua kwa uhakika.

Kwa sababu, mtu anapotaka kuja kukupa rushwa, hakuambii kwamba anakuja kukupa rushwa ili ujiandae kuchukua ushahidi. Hakuandikii hundi na kuiwekea label ya "Rushwa" na kuiwekea saini ili uje uitumie kama ushahidi.

Kuna maneno yamesemwa, kwamba Lissu, Wenje, David Djumbe na Abdul walikutana.

Hili Abdul hajalikanusha.

Lissu kasema Abdul alitaka kumpa pesa ili Lissu asimsakame mama yake Abdul. Hili Abdul hajalikanusha.

Lissu kasema alikataa pesa za Abdul, akamtaka Abdul amsaidie kupata pesa zake za kihalali.

Katika kanuni za habari, habari potofu ikitolewa, anayeona hiyo habari si sahihi ana haki na wajibu wa kuisahihisha.

Na habari isiyopingwa inachukuliwa kuwa ni ya kweli.

Kama Tundu Lissu kasema uongo, Abdul ajitokeze tu na kutupa upande wake tuusikilize.
 
Lissu hakukataa hongo.

Alikataa hongo ya pesa akakubali hongo ya fadhila ya Abdul kumsaidia apate mafao yake.

Kwa maneno yake mwenyewe.

That was influence peddling.

Lissu should do better than that.
Ilikuwa ni mbinu ya kumtoa Abdul tu pale nyumbani kwa lissu, pole mkuu
 
MKOA WA MARA,MKOA WA MARA.
RUSHWA YA FEDHA INANUKIA KWA AJILI YA KUWASHAWISHI WAJUMBE WAMCHAGUA MBOWE.

Katibu Wa Mkoa wa Mara Donard mwembe Akishirikiana na m/kiti wa chama wilaya ya Rorya Nyakiriga na katibu wa jimbo la Tarime Mjini Pamba Jana Tarehe.28.12.2024 Waliwatumia kwa makundi makundi Nauli wajumbe wa mkutano mkuu Taifa kutoka kwenye majimbo mbali mbali ya mkoa wa Mara ili waende ofisi ya chama mkoa iliyopo Makao makuu ya mkoa Musoma mjini maeneo ya Nyakato kwa Saa nane,wajumbe hao walipofika waliambiwa kuwa wamuunge mkono mbowe na wampigie kura ili ashinde uchaguzi mkuu utakaofanyika Tarehe.21.01.2024 na adi Leo Tarehe.29.12.2024 ninapoandika ujumbe huu wajumbe bado wanaendelea kuitwa kwenye ofisi izo za chama mkoa wa mara.
Na kiasi cha fedha kilichotengwa kwa ajili ya kuwapa hao wajumbe ni milioni tatu.
DONARD MWEMBE
Ikumbukwe donard mwemba alishinda nafasi ya katibu wa mkoa kwa kutumia Rushwa kubwa sana naona yale yale aliyoyafanya wakati wa uchaguzi wa mkoa ndo anayafanya tena kwenye uchaguzi huu wa ngazi ya Taifa.
OFISI ZA MKOA
Ofisi zetu za chama mkoa ndo leo hii zinatumika kugawa Rushwa za uchaguzi,ofisi zimefanywa chafu zimekuwa ni pango la kutolea Rushwa, hii ni atari sana na aipaswi kufumbiwa macho.
COVID-19
Ester Bulaya na Halima mdee walipokuwa Bunda walimuita katibu wa mkoa na kumkabidhi kiasi cha Tsh.5000,000/=(milion tano)Kwa ajili ya kuhakikisha wajumbe wanaitwa na kupewa fedha ,hawa madada wanasema mbowe akishinda wanarudishwa kwenye chama ivyo wanampambania.
ZOEZI LA KUWAITA WAJUMBE
Zoezi la kuwaita wajumbe linaendelea adi sasa na wanatumia nguvu kubwa sana ya fedha kuhakikisha wanawapata wajumbe,huu uchaguzi umegubikwa na rushwa,umegubikwa na fedha za covid-19.
MKOA MARA
Mkoa wa mara umeonekana ni mkoa mgumu sana ndo maana inatumika nguvu kubwa sana ya fedha kuhakikisha wajumbe wanarubuniwa na kupewa hongo ili wabadili mawazo yao.
Hatuwezi kuwa na viongozi waliyochaguliwa kwa Rushwa pia wanagawa fedha za Rushwa kwa wajumbe ili wakamchague m/kiti kwa Rushwa.
M/KITI WA MKOA WA MARA
M/kiti wa mkoa mwl.Chacha Heche alipotaftwa kuulizwa kama ametoa baraka ofisi za chama zitumike kugawa Rushwa alisema ata yeye anamshangaa katibu wake kwa nini anafanya ivyo anakichafua chama na anafanya ivyo kwa maslahi ya nani.Mwl.chacha heche yupo nje ya nchi kwa sasa.

TUTAKULA MACHAME TUTALALA IKUNGI.

CHUKUWA PESA KURA MPIGIE LISSU
#LISSU WILL FIX IT.
#LISSU M/KITI AJAYE
#NI YEYE
Usifanye makosa Tarehe.21.01.2024
Haahaa chadema inaanzia kugawa rushwa kwa staili hii kama ccm, uhalali wa kupinga ccm wataupata wapi? Nawaomba takukuru wafuatilie kwa karibu Sana uchaguzi wa chadema.Bila lissu kuwa mwenyekiti wa chadema, ccm na chadema kutakuwa hakuna utofauti
 
Ilikuwa ni mbinu ya kumtoa Abdul tu pale nyumbani kwa lissu, pole mkuu
Hapana Mkuu.

Lissu ni mtu bold sana. Lissu ni mtu muwazi sana. To a fault.

Angetaka kumfukuza Abdul pale angemfukuza bila mbinu yoyote.

Lissu ni kati ya wanasiasa wachache Tanzania wanaoweza kusema ukweli mchungu bila kuremba, kasema ukweli mchungu wa kuki expose chama chake mwenyewe kwenye rushwa.

Huyo mtoto Abdul, Lissu anamuogooa kwa kipi mpaka atumie mbinu kumtoa?

Lissu alitaka favor kweli.
 
  • Thanks
Reactions: Tui
Back
Top Bottom