Kuhusu kurudishiwa hela na HESLB pindi unapokatwa zaidi ya deni lako

Kuhusu kurudishiwa hela na HESLB pindi unapokatwa zaidi ya deni lako

Zero Competition

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2018
Posts
347
Reaction score
553
Habari za leo leo washikadau,

Nimesikia kwamba inapotokea ofisi yako imekukata zaidi kwenye mshahara wako kuliko deni lako halisi bodi ya mikopo wanarudisha hela yako ndani ya siku 90.

Hapa naongelea mfano deni lako lote lilikua ni milioni 5 lakini kwa bahati mbaya ofisi yako ikakata miezi mingi zaidi na hivyo jumla ya makato kufikia milioni 8.

Je, kuna ukweli juu ya hili?

Kuna yeyote humu ashawahi kukutana na tatizo hili na kweli akarejeshewa pesa yake yote iliyozidi?

Kama yupo naomba anipe ushuhuda au kama kuna yeyote ana ufahamu juu ya hili tunaomba atujuze taratibu za kupata zikoje
 
Unakusanya ushahidi kisha unaenda kitengo cha malalamiko. Wanarudisha tu ila siku 90 zinaweza zidi au pungua
 
naomba kujua total loan charges ya helsb ni nn maana naona nina kama 1.1 M lakin den langu la ukweli ni 1.4 m ila ukichanganya zte nakua na 2.4 m .
 
Ni kweli wanarudisha ndani ya siku hizo 90 na huenda zisifike
Mim niliwahi kukatwa na heslb kimakosa kwakuwa sijawah kupata mkopo wao lakin wakaniingizia makato kwenye salary slip nkafuatilia ndan ya siku hizo 90 wakanirudishia pesa yangu yote
 
Shukrani sana ndugu kwa mrejesho
 
naomba kujua total loan charges ya helsb ni nn maana naona nina kama 1.1 M lakin den langu la ukweli ni 1.4 m ila ukichanganya zte nakua na 2.4 m .
Hii total charge nimepigwa kama 991K.. sijajua inakuaje lazima niwaibukie wanipe maelezo
 
kama ni LAF,VRF NA PENALTY SI WALIFUTA? INAKUAJE WAWEKE.
VRF imefutwa lakini kuna kitu kipya kinaongezwa kwenye deni la msingi wanaita total charges kinaongezwa kwenye deni la msingi

B8990733-0F52-40E2-8B4E-33E1D190AE8C.jpeg
 
DA KWA KWELI ITABIDI NIENDE KWENYE OFIS ZAO WANIFAFANULIE. ZAIDI
 
naomba kujua total loan charges ya helsb ni nn maana naona nina kama 1.1 M lakin den langu la ukweli ni 1.4 m ila ukichanganya zte nakua na 2.4 m .
Inajumuisha:
1. Administration fees 1%
2. VRF paid before 1st May
3. Penalty before 1st June 10%
 
Habari za leo leo washikadau,

Nimesikia kwamba inapotokea ofisi yako imekukata zaidi kwenye mshahara wako kuliko deni lako halisi bodi ya mikopo wanarudisha hela yako ndani ya siku 90.

Hapa naongelea mfano deni lako lote lilikua ni milioni 5 lakini kwa bahati mbaya ofisi yako ikakata miezi mingi zaidi na hivyo jumla ya makato kufikia milioni 8.

Je, kuna ukweli juu ya hili?

Kuna yeyote humu ashawahi kukutana na tatizo hili na kweli akarejeshewa pesa yake yote iliyozidi?

Kama yupo naomba anipe ushuhuda au kama kuna yeyote ana ufahamu juu ya hili tunaomba atujuze taratibu za kupata zikoje
Binafsi hili lilinikuta...
Nilihisi nimekatwa zaidi ya ninachodaiwa... ilizidi Tshs. 800,000/-. Nikakusanya nyaraka zifuatazo;
1. Barua aliyoandikiwa mwajili wangu inayoonyesha deni langu
2. Salary slips zenye MAKATO ya HELB

Nikakokotoa nikapa kiasi kilichozidi. Cha kwanza nikamwandikia mwajili wangu juu ya kilichozidi, huku nikiambatanisha nyaraka tajwa hapo juu pamoja na mahesabu niliyoyafanya... MWAJILI AKAMIRUFISHIA HIYO LAKI NANE...

Nikaenda na the same documents pale ofisi za HELB, nao wakaniambia niwaandikie barua yenye kutaja chuo nilichosoma, Kozi niliyosoma na mwaka nilioanza na kumaliza chuo pamoja na akaunti number yangu.

Baada ya miezi minne nao wakanirudishia na wakanipa barua inayoonyesha kuwa nimemaliza mkopo..

KIFUPI nilirudishiwa mara mbili... toka kwa HELB na toka kwa mwajili wangu
 
Acha uongo... kwenye hili msemo wako hauswii...!

Uje ujaribu kwenda heslb uwaulze kwanin wanatuchanganya mara VRF before 1 MAY 2021 mara penalty before 1 july yaan wanachanganya sana uwambie watoe ufafanuzi
 
Uje ujaribu kwenda heslb uwaulze kwanin wanatuchanganya mara VRF before 1 MAY 2021 mara penalty before 1 july yaan wanachanganya sana uwambie watoe ufafanuzi
Mimi niliwauliza wakaniambia hizo ndio zimefutwa Ila wewe umeshazilipa kupitia marejesho yako.
Kwahiyo ambao wataanza kulipa deni lao kuanzia June ndio faida kwao maana hawatalipa kabisa
 
Back
Top Bottom