Super Handsome
JF-Expert Member
- Jul 16, 2013
- 3,844
- 6,448
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameliagiza Jeshi la Polisi kupitia kamati za ulinzi na usalama za mikoa na wilaya ziendelee kufanya tathimini juu ya utoaji wa vibali vya mabasi ya abiria kusafiri usiku.
Majaliwa alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Sophia Mwakagenda katika kipindi cha maswali ya papo kwa papo bungeni.
Mbunge huyo alitaka kufahamu nini Serikali inafanya ili kuruhusu mabasi ya abiria yasafiri usiku na mchana, hatua ambayo italiingizia mapato Taifa.
Akijibu swali hilo, Majaliwa amesema agizo la mabasi kutosafiri usiku lilitolewa kwasababu mara nyingi mabasi yalikuwa yanatekwa wakati yanaposafiri usiku na Serikali ilikuwa ikilazimika kuweka askari kwa kila basi linaposafiri ili kuhakikisha usalama kwa wasafiri.
“Ni kweli kuwa usalama umeimarika nchini na Serikali inaendelea kuimarisha zaidi usalama. Umuhimu wa hilo jambo upo lakini tutaendelea kuwasiliana na vyombo vya ulinzi na usalama na kama je wamejiridhishaje na usalama huo ili turuhusu mabasi kusafiri wakati wote ili kuboresha uchumi,”amesema.
Majaliwa amesema pia hatua hiyo ya kuruhusu mabasi kusafiri usiku itawezesha wafanyabiashara kuweka mipango yao ya kutoka eneo moja hadi nyingine katika kuendesha biashara zao kwa uhuru mkubwa.
Chanzo: Habari Kuu za Tanzania, Siasa, Afya, Uhalifu na zaidi - TanzaniaWeb