Kuhusu kutekwa kwa Hamphrey Polepole, kuna maswali yanakosa majibu kwangu

Kuhusu kutekwa kwa Hamphrey Polepole, kuna maswali yanakosa majibu kwangu

The unpaid Seller

JF-Expert Member
Joined
Oct 27, 2019
Posts
2,360
Reaction score
6,922
Wakuu regards kwenu,

Wote tonajua jinsi ndugu Polepole alivyo jiweka hatarini kuanzia kujiuzuru mpaka kuibua maovu mengi ya ndani ya serikali.
Screenshot_20251008-090340.jpg


Ni dhairi shairi alijua hatari kubwa iliyomzunguka ukizingatia nyakati tulipo utekaji na mauaji yameongezeka sana sana i.e ni juzi tu mzee Ally Kibao alikamatwa mchana kweupe na kuuawa.

Ilikuaje ndugu Humphrey kua nchini tena akiishi kwenye nyumba yake na akiwa hata hana ulinzi ??!!
Screenshot_20251006-105337.png

Niliposukia amekamatwa akiwa nyumbani kwake alipokua akiishi na wasaidizi wa kazi wawili NILISHTUKA, NIKAFADHAIKA SANA MOYONI MWANGU. Kwa tujuavyo Polepile ni mtu makini na mwerevu sana sana ilikuaje akajisisk ovyo namna hii.

Kuna mtu atasema "hakuna MUOGA, alikua jasiri" hakika huo sio ujasiri kuchukua risk ya wazi sio ushujaa. Katika mafunzo ya kijeshi (wasiopitia jeshi watakubaliana na Mimi) Moja ya msisitizo mkubwa katika uwanja wa mapambano ni "KUA HAI" ni lazima uhakikishe unaishi kabla ya kufikiria kumshinda adui maana hauwezi kumshinda adui ukiwa umekufa.

Kabla ya kuchukua uamuzi wowote ni lazima uwe na mpango wa kuhakijisha usalama wako maana wewe ni rasilimali kufa kwako ni hasara kwa team yako na kunadhoofisha team yako, ikitokea umekufa iwe ni kwa kuzidiwa na adui na sio kwa uzembe.

Mfano unayo taarifa uwepo wa mabomu ya kutegwa ardhini (landmiles) na babo ukaamua kupitia eneo Hilo eti kwenda kumpiga adui, unaakili wewe utalipuka kabla haujafika kwa adui wewe. Na hata usipokufa labda ukajeruhiewa na kurudisha kambini unastahili adhabu ukirudi kambini.

Au adui ana vifaa hodari kuliko nyie na wako wengi kuliko nyie na wakati nyie mna majeruhi wengi, mmeishiwa risasi na mmepoteza ramani ya eneo hapa yawapasa kuretreat kurudi nyuma mkajipange ni kukosa maarifa na kinyume cha kanuni za vita kama mtalazimusha kumfuata adui ilihali nyie ni majeruhi na mmeishiwa risasi.

Sasa ilikuaje Polepole awepo nchini tena nyumbani kwake Tena bila ulinzi. Huu ndio utaita ushujaa ??! Kumrahisishia adui Yako kukushinda ndio ushujaa ??!

Yani hata kimtaa mtaa tu ukizinguana na wana hauwezi kwenda kulala nyumbani kwako unajua defender la mapolisi litafuka natural instincts zitakwambia utafute pa kujibanza sio nyumbani kwako,

sasa IWEJE kwa kuikosoa serikali Tena kwa mambo nyeti na kuweka maovu Yao wazi kwa kuwataja majina na bado ATI akawa Tanzania Tena kwenye nyumba yake Tena bila ulinzi wowote ??! Na huo ndio ushujaa eti ??!

Ushujaa ni kua tayari kukabiliana na adui bila woga na sio kujiweka hatarini na kumrahisishia adui kukupiga.

Kama Hilo halijakushangaza kumbe bahati nzuri Hamphrey kapandikizwa chip bwana inayoweza kua tracked kujua alipo JAMBO ZURI KABISA. Haya ghafla anatokea ndugu yake na kuropoka "Humphrey ana chip tutamtafuta aliko" jamani WHAT THE *** !!? Huyu nae je kwa kuropoka huko hakukua hata waliomteka watapata taarifa hii muhimu na hakika wataichomoa mwilini mwake ??!

Wale wanaosema kujirisk kwake Polepole ni ushujaa je na hapa watasema kitendo cha huyu kaka wa Hamphrey kuropoka kua Hamphrey ana chip nako ni ushujaa ??! Yani kumrahisishia adui kukushinda ni ushujaa au ni uzembe ??!

Anyways yote kwa yote maombi yangu ndugu Hamphrey awe salama maana ni hazina kwa taifa letu, we still need him.
 
Ilikuaje ndugu Humphrey kua nchini tena akiishi kwenye nyumba yake na akiwa hata hana ulinzi ?
Nadhani alikuwa amepanga.
Niliposukia amekamatwa akiwa nyumbani kwake alipokua akiishi na wasaidizi wa kazi wawili NILISHTUKA, NIKAFADHAIKA SANA MOYONI MWANGU. Kwa tujuavyo Polepile ni mtu makini na mwerevu sana sana ilikuaje akajisisk ovyo namna hii.
Kuna kusalitiwa. Yesu ndio Yesu na alisalitiwa sembuse Polepole?
Kuna mtu atasema "hakuna MUOGA, alikua jasiri" hakika huo sio ujasiri kuchukua risk ya wazi sio ushujaa. Katika mafunzo ya kijeshi (wasiopitia jeshi watakubaliana na Mimi) Moja ya msisitizo mkubwa katika uwanja wa mapambano ni "KUA HAI" ni lazima uhakikishe unaishi kabla ya kufikiria kumshinda adui maana hauwezi kumshinda adui ukiwa umekufa.
Kuna muda lazima ukubali kuyatoa sadaka maisha yako kwaajili ya wengine.
Sasa ilikuaje Polepole awepo nchini tena nyumbani kwake Tena bila ulinzi. Huu ndio utaita ushujaa ??! Kumrahisishia adui Yako kukushinda ndio ushujaa ??
Tanzania ndio kwao. Nadhani maamuzi sahihi ni yale aliyoyafanya mwenyewe.
 
People, ni kama mnataka watu waseme HP alikuwa wapi siku zote na pale alienda lini, na alichomeshwa lini na …. na…. Kipindi ambacho hatma ya HP haijulikani. mnataka watu wahadithie ABCDs kwanza haisaidii, pili kuna wengine watapata matatizo zaidi kwa hizi chokochoko. Wote hatufahamu ila yale makazi yanaonekana ni temporary.

Kuwakosoa watawala ni vita, kawahiwa kabla…..

Kaka yake HP alipaniki tu, all empathetic people would understand his situation.
 
Hili la polepole ukilitafakari zaidi pia utakosa majibu mimi swali moja ninalojiuliza mpaka sasa hvi ni "KWANINI PAMOJA NA KUWANANGA VIONGOZI WA CCM LAKINI BADO HAJAVULIWA UANACHAMA"? Malisa alitikisa tu kiberiti chaap akatemeshwa mbung'o iweje polepole kipindi chote hicho anatamba tu. Tuwe makini mno CCM wana mbinu nyingi mno kulingana na aina ya mazwazwa yanayoongozwa
 
Further thinking, isijf ikawa ni trick kuhamisha wananchi mijadala kuhusu no reforms no election na kesi ya Lissu ili tu uchaguzi wa ajabu upite!
 
Further thinking, isijf ikawa ni trick kuhamisha wananchi mijadala kuhusu no reforms no election na kesi ya Lissu ili tu uchaguzi wa ajabu upite!
Umekosa ubongo, nani kakulazimisha uhame mjadala,
Si uendelee na NRNE,Yako.
Zaidi ya kuandika andika huku umechukua hatua Gani?
 
Umekosa ubongo, nani kakulazimisha uhame mjadala,
Si uendelee na NRNE,Yako.
Zaidi ya kuandika andika huku umechukua hatua Gani?
Bushmamy, vipi oktoba utaenda kutiki au utaandamana?
 
 
Back
Top Bottom