Ndio.
Unapewa baru ya RTO inayothibitisha kukaguliwa.
Pia unaweza kuwa na cheti cha chuo ambacho hakija sajiliwa kutoa daraja husika, ikala kwako.
Kua na cheti kabla ya leseni ni uhuni na sio utaratibu, unapokua na lena maanayake unaomba leseni, kisheria Polisi/ Vehicle Inspector ndie aliepewa mamlaka ya wewe kukupa daraja unaloomba au kukupa la chini yake au asikupe kabisa kwa mujibu wa drivig yako, baada ya V/INSP kukuthibitishia daraja linalokufaa hio ndio leseni ya udereva, hapo utarudi chuo ulichosoma ili wakutengenezee cheti kwa mujibu wa leseni yako/daraja lako, na itamaliza muda wake baada ya miezi 2 7bu hujalipia kodi leseni hiyo, ndio hapo sasa utaenda kulipia kodi ya leseni ya udereva ya miaka mi 5 ya Tsh- 70,000/= TRA na watakupa kadi inayoonyesha daraja alilokupa Polisi/V.INSP na muwa wa ku expire wa miaka mi 5.
TRA hutoa leseni ila siyo ya udereva.
Wengi hatuna elimu kuhusu upatikanaji sahihi wa leseni za udereva na kuamini TRA ndio wanatoa leseni za udereva, TRA wanakusanya kodi tu ya dereva husika. Ndio maana uhakiki unafanyika Polisi ndio wenye mamlaha na leseni za udereva.
Kupata cheti chuoni bila kua na leseni na ukaenda TRA ukalipa na kupewa kadi, ni nani aliekuthibitisha wewe kua dereva? Siku ukipata ajali na ukakutana na wajuaji mahakamani wakidai uthibitisho wa wewe kua dereva ndio utafurahi, baada ya kukosa sirio namba ya PF ya polisi. Unagongwa na kosa la kughushi/kufoji nyaraka za serekali.
NB. Nenda Veta ua NIT utapata leseni kiurahisi na isio na mashaka maana NIT pale walimu wengi ni ma Polisi/V.INSPECTOR wenyewe, hivyo wanakuthibitisha wenyewe na kila kitu kinaishia pale.
VETA pia wanao ma V.INSP wao.