Kuhusu madaraja ya leseni na magari yake

Kuhusu madaraja ya leseni na magari yake

Cheti cha kuzaliwa hakihusiki.
Namba ya nida ni lazima kwa Zanzibar, maana za kule zinatumika ichi za sadec hivyo kadi ya leseni ni lazima ionyeshe vitu V3 vya msing
1) Wewe ni raia wa taifa gani.
2) Group lako la damu.
3) Una kikwazo gani barabarani. Eg. Unatakiwa kuvaa miwani ya macho au la au leseni yako umezuiliwa kuendesha baadhi ya vyombo kwa muda fulani na mahakama au la, Mfano, umefungiwa daeaja "C" kwa mwaka m1 ila unarugusiwa kuendesha daraja "C2,Ç3 na E" na kama hauna kikwazo wanaandika NONE
Huku kwetu bara sio lazima nida na wakikufungia daraja kwa muda fulani wanafungia leseni yote maana wanachukua kadi hadi muda wa adhabu uishe, kadi zetu hazionyeshi pa kuzuiliwa daraja.
Asante mkuu kwakunielewesha vizuri
 
Ndio.
Unapewa baru ya RTO inayothibitisha kukaguliwa.
Pia unaweza kuwa na cheti cha chuo ambacho hakija sajiliwa kutoa daraja husika, ikala kwako.
Kua na cheti kabla ya leseni ni uhuni na sio utaratibu, unapokua na lena maanayake unaomba leseni, kisheria Polisi/ Vehicle Inspector ndie aliepewa mamlaka ya wewe kukupa daraja unaloomba au kukupa la chini yake au asikupe kabisa kwa mujibu wa drivig yako, baada ya V/INSP kukuthibitishia daraja linalokufaa hio ndio leseni ya udereva, hapo utarudi chuo ulichosoma ili wakutengenezee cheti kwa mujibu wa leseni yako/daraja lako, na itamaliza muda wake baada ya miezi 2 7bu hujalipia kodi leseni hiyo, ndio hapo sasa utaenda kulipia kodi ya leseni ya udereva ya miaka mi 5 ya Tsh- 70,000/= TRA na watakupa kadi inayoonyesha daraja alilokupa Polisi/V.INSP na muwa wa ku expire wa miaka mi 5.
TRA hutoa leseni ila siyo ya udereva.
Wengi hatuna elimu kuhusu upatikanaji sahihi wa leseni za udereva na kuamini TRA ndio wanatoa leseni za udereva, TRA wanakusanya kodi tu ya dereva husika. Ndio maana uhakiki unafanyika Polisi ndio wenye mamlaha na leseni za udereva.
Kupata cheti chuoni bila kua na leseni na ukaenda TRA ukalipa na kupewa kadi, ni nani aliekuthibitisha wewe kua dereva? Siku ukipata ajali na ukakutana na wajuaji mahakamani wakidai uthibitisho wa wewe kua dereva ndio utafurahi, baada ya kukosa sirio namba ya PF ya polisi. Unagongwa na kosa la kughushi/kufoji nyaraka za serekali.
NB. Nenda Veta ua NIT utapata leseni kiurahisi na isio na mashaka maana NIT pale walimu wengi ni ma Polisi/V.INSPECTOR wenyewe, hivyo wanakuthibitisha wenyewe na kila kitu kinaishia pale.
VETA pia wanao ma V.INSP wao.

Hii elimu itakuwa imetoka idarani [emoji28]
Asante sana mkuu kwa maelekezo yako[emoji119]
 
Chief karibu kwenye tasnia hii ya udereva

Madaraja ya leseni na maelezo kama ifuatavyo:

Daraja A,A1,A2 NA A3 NI kwa ajili ya pikipiki.

Daraja B NI MAGARI MADOGO YOTE AMBAYO HAYAJASAJILIWA KIBIASHARA YANI HAYANA PLATENAMBA NYEUPE.

DARAJA D NI MAGARI MADOGO NA MPAKA MWISHO YENYE UKUBWA WA TANI TATU NUSU MFANO CANTER PLATE NAMBA ZISIWE NYEUPE

DARAJA C1,C2,C3 HIZI NI KWA AJILI YA KUBEBA ABIRIA MFANO C1 NI COSTA NA EACHER ZINAZO BEBA ABIRIA PLATE NAMBA ZAKE NI NYEUPE

DARAJA C NI MABASI YA MKOA AU GARI INAYO BEBA ABIRIA KUANZIA 30 NA KUENDELEA

DARAJA E MAGARI MAKUBWA YA MIZIGO KUANZI TANI TATU NA NUSU MPAKA NAKUENDELEA

UTANISAMEHE KWA MUANDIKO MBOVU MANA NATUMIA KITOCHI SO EDITING NYINGI NAONA UVIVU

THANKS
Ukishakua na daraja D si hauna Baja ya daraja B?
 
Ukishakua na daraja D si hauna Baja ya daraja B?
Haja ipo. Ndio maana pia ikatofautishwa kati ya B na C3.
Zanzibar ndio unaruhusiwa kuendesha chombo cha daraja dogo/la chini endapo una daraja kubwa/la juu, 7bu wao leseni zao zipo SADEC, sisi kila hatua ya gari na daraja lake.
 
Ukishakua na daraja D si hauna Baja ya daraja B?
Kunatofauti kidogo chief kati ya daraja D na B daraja d ni magari madogo ya mizigo ya biashara na daraja b ni magari madogo binafsi yani haya ya kutembelea majumbani na kuendea ofisini haja ipo kwa sababu matumizi ni tofauti
 
Haja ipo. Ndio maana pia ikatofautishwa kati ya B na C3.
Zanzibar ndio unaruhusiwa kuendesha chombo cha daraja dogo/la chini endapo una daraja kubwa/la juu, 7bu wao leseni zao zipo SADEC, sisi kila hatua ya gari na daraja lake.
Samahani Mkuu Kwa hiyo ukiwa na daraja D huruhusiwi kuendesha hizi gari za daraja B?
 
Samahani Mkuu Kwa hiyo ukiwa na daraja D huruhusiwi kuendesha hizi gari za daraja B?
Ndio.
Kiufupi, B ni SALOON car, na D ni SUV car.
Pia B inakupeleka ktk gari za abiria kina C3 - C, wakati D inakupeleka kwenye mizigo huko kina E.
Ukiona umetofautishiwa ujue kuna tofauti ya UREFU, UZITO au KAZI kutoka daraja moja kwenda jengine.
 
Hey members nawapa mrejesho
Nimefanikiwa kusoma driving katika chuo Cha veta Pwani chini ya mwalimu Gaspar(mtaalam) kuanzia siku ya tarehe 27/11/2023 mpaka tarehe29/12/2023

Kuna swali nimeona juu hapo kuhusu daraja B na D kwa mujibu wa mwalimu amesema Amna ulazima wa kuwa na daraja B wakati ukiwa na daraja D
 
Ulichukuwa c3
 
Back
Top Bottom