Kichuchunge
JF-Expert Member
- Dec 2, 2020
- 384
- 970
"Naamini mwaka huu tutakuwa na ongezeko la Mashirika yanayotoa gawio, Mashirika yasiotoa gawio lazima tutumie sheria kuhakikisha yanatoa au yanaondoka, Msajili wa Hazina simamia hili. Taasisi zote zinazotakiwa kutoa gawio, zifanye hivyo kabla ya mwezi wa saba, haiwezekani hadi Jeshi limetoa gawio wao wasitoe, tena nikiona hata Polisi na Magereza wanatoa gawio, nitafurahi sana
Msajili wa Hazina hakikisha ifikapo mwezi Julai, Mashirika yote 253 nchini ambayo yamekuwa hayatoi gawio kwa Serikali, yawe yametoa gawio, la sivyo yafungwe. Kama Shirika halitoi gawio kwa sababu linajiendesha kwa hasara basi lifungwe, hakuna maana kuwa na Mashirika yanayofanya kazi kwa hasara, la sivyo watafute namna ya kutoa magawio yao Serikalini" nukuu ya JPM wakati akipokea gawio la TTCL