Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,362
- 48,879
Ndivyo alivyokuwa akijidanganya Rais Chasesku. Alikuja kushangazwa na uamuzi wa mahakama ya kijeshi kuwa yeye na mkewe wanatakiwa kuuawa kwa uhalifu alioutendea umma, na kisha kufuatiwa na maandamano ya umma kuunga mkono maamuzi ya mahakama.Yeah, waranzania 20 wa jf + chadema wachache. Huku uraiani watu tuko na mama hata milele!
Alishangazwa zaidi na kitendo cha askari ambao siku zote alikuwa akiwapa amri dhidi ya umma, siku hiyo kila mmoja akitaka apewe nafasi ya kutekeleza hukumu ya mahakama dhidi ya Rais, hadi ikalazimu kuchezesha bahati nasibu ili kumpata wa kufyatua risasi ya kuhitimisha ukomo wa maisha ya Chasesku Duniani.
Ukiwa kiongozi jivunie kutekeleza wajibu wako kwa kadiri ya katiba na sheria na siyo kelele za wapambe.
Rais Samia akishupaza shingo kwa sababu ya wapambe nuksi, kuna siku atajuta.