Kuhusu ujenzi wa kiwanda cha kuchakata mafuta Tanga.

Kuhusu ujenzi wa kiwanda cha kuchakata mafuta Tanga.

Heshima sana wanajamvi.

Nilimsikia Rais wa Kenya Dr W Rutto akihutubia Bunge juu ya ujenzi wa kiwanda cha kuchakata mafuta Jiji Tanga.

Wakati huo huo Rais wa Tanzania akihoji kutokuwa na taarifa ya ujio wa kiwanda hicho katika nchi yake.

Ujenzi wa kiwanda cha kuchakata au kusafisha mafuta ni suala kubwa sana.
Faida zake si haba.
Mosi ni ajira.
Pili uwekezaji wa mtaji mkubwa.
Tatu viwanda vingine ambavyo vitatumia malighafi ya kiwanda cha kusafisha mafuta eg Lami,Mbolea.......
Tatu ukuaji wa haraka sehemu kitakapojengwa kiwanda (Tanga)
Nne mapato kodi na wakaazi wa eneo husika.

Serekali ya awamu ya nne Kikwete ilipambana na Kenya kipindi kile cha ujenzi wa bomba la mafuta ya Uganda.

Kwa hakika kama serekali ya awamu ya sita ingekuwa madarakani kipindi kile kwa hakika bomba lingekwenda Kenya.

Nimejikuta nikisikitika jinsi ambavyo tunachezea fursa adimu.
Tumejikita zaidi kushangilia goli la mama badala ya kujikita katika mambo muhimu.

Ngongo kwasasa Mombasa.
Magufuli ndiye alifanikisha bomba la Hoima kuja Tanzania
 
Back
Top Bottom