KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA IBARA YA 147INASEMA
147.-(1) Ni marufuku kwa mtu yoyote au shirika lolote au
kikundi chochote cha watu, isipokuwa Serikali kuunda au
kuweka Tanzania jeshi la aina yoyote.
(2) Serikali ya Jamhuri ya Muungano yaweza, kwa mujibu
wa sheria, kuunda na kuweka Tanzania majeshi ya aina
mbalimbali kwa ajili ya ulinzi na usalama wa nchi na wananchi
wa Tanzania.
(3) Itakuwa ni marufuku kwa mwanajeshi yeyote kujiunga na
chama chohote cha siasa, isipokuwa tu kama atakuwa na haki
ya kupiga kura iliyotajwa katika ibara ya 5 ya Katiba hii.
(4) Kwa madhumuni ya ibara hii, "mwanajeshi" maana yake
ni askari aliyeajiriwa kwa masharti ya muda au ya kudumu
katika Jeshi la Ulinzi, Jeshi la Polisi, Jeshi la Magereza au Jeshi
la Kujenga Taifa
SASA HAO WANAOSEMA NANI NI BORA NANI NI MDOGO WANAYATOA WAPI. FIKIRI KWA KINA. Kumbuka Rais amewekwa na katiba na katiba ndiyo inanena hivyo.
Sent using
Jamii Forums mobile app