Huyo hajitambui,JWTZ maafisa wake wanaanza kupewa kamisheni(commissioned officer) kuanzia nyota moja(Luteni Usu).Kwa idara zingine kama Polisi,Magereza,Uhamiaji na Zimamoto wanaanzia nyota tatu (mrakibu msaidizi wa polisi au kwa kifupi ASP katika lugha ya kiingereza).Wenye kamisheni wote wanawajibika kwa Rais moja kwa moja.
Ulinganifu ni huu kwa maafisa wenye kamisheni(wanaowajibika kwa rais):
JWTZ Vs. POLISI
Jenerali(Gen). - -----------(neal)
Luteni jenerali. - ------(neeal)
Meja jenerali. - IGP(mkuu wa polisi)
Bregadia jen. - Kamishina wa polisi
Kanali(col). - Naibu kamishina(DCP)
Luteni kanali - kamishina msaidizi mwandamizi(SACP).
Meja - Kamishina msaidizi (ACP).
Kapteni - Mrakibu mwandamizi(SSP)
Luteni. - Mrakibu wa polisi(SP)
Luteni usu - Mrakibu msaidizi (ASP)
NB:
Maafisa wenye kamisheni katika JWTZ wananzia nyota moja(luteni usu),na polisi,magereza,uhamiaji na zimamoto ni kuanzia nyota ya tatu(ASP au ASI Kwa uhamiaji na ASF kwa zimamoto).
Kwa hiyo hao ndio maofisa wanaowajibika kwa rais na viapo vyao viko tofauti na askari wengine.