Kuhusu Value Retention Fee(VRF) ya HESLB

Mbishi 4 real

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2014
Posts
640
Reaction score
651
Habari za jioni waungwana

Nilikua naomba kuuliza kuhusu hii Value Retention Fee ambayo ilikua inatozwa kwenye mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu

Kulingana na tamko la muheshimiwa Rais kwamba hii tozo imefutwa rasmi, lakini sasa nashindwa kujua je kwa wale ambao washaongezewa mzigo wa deni kutokana na hii tozo madeni yao yatapungua baada ya mahesabu kufanyika upya au watalipa deni halali pamoja na VRF ?

Kwa wale wanaojua utaratibu utakaotumika naomba mnijuze
 
wengi tuna maswali kuliko majibu ngoja nisubiri majibu hapa huenda nikapata
 
VRF ama Value retention fee ni gharama za kulinda thamani ya pesa ya mkopaji ambaye ni mwanafunzi. Gharama hii inatozwa pindi mdaiwa anapopitisha kipindi cha marejesho mara baada ya kuhitimu.

Kwa kesi ya HESLB walikua wanatoza kiwango cha asilimia sita (6%) kwa kila mdaiwa.

Hivyo basi baada ya tamko la Mh. Rais siku ya Mei mosi, tozo hiyo imetolewa na itafanya wadaiwa wote kulipa kiasi kile kile walichonufaika wakati wa maombi. Kama ulikopa shilingi milioni 5, utarejesha milioni 5 hiyo hiyo bila gharama za ziada.
 
VRF ama Value retention fee ni gharama za kulinda thamani ya pesa ya mkopaji ambaye ni mwanafunzi. Gharama hii inatozwa pindi mdaiwa anapopitisha kipindi cha marejesho mara baada ya kuhitimu. Kwa kesi ya HESLB walikua wanatoza kiwango cha asilimia sita (6%) kwa kila mdaiwa.
Hivyo basi baada ya tamko la Mh. Rais siku ya Mei mosi, tozo hiyo imetolewa na itafanya wadaiwa wote kulipa kiasi kile kile walichonufaika wakati wa maombi
Kwa hiyo madeni yooooote yatakokotolewa upya?
 
VRF ama Value retention fee ni gharama za kulinda thamani ya pesa ya mkopaji ambaye ni mwanafunzi. Gharama hii inatozwa pindi mdaiwa anapopitisha kipindi cha marejesho mara baada ya kuhitimu. Kwa kesi ya HESLB walikua wanatoza kiwango cha asilimia sita (6%) kwa kila mdaiwa.
Hivyo basi baada ya tamko la Mh. Rais siku ya Mei mosi, tozo hiyo imetolewa na itafanya wadaiwa wote kulipa kiasi kile kile walichonufaika wakati wa maombi
apa naona mil 32 nitalipa
 
Umejibu vyema ila bado hujakata kiu ya muuliza swali. Je kwenye slip yake pataonekana badiliko lolote? Au itaendelea kupungua vilecile tu kama ambavyo ilikuwa?

Kwa mfano deni kwenye slip ya mwezi wa nne lilikua linasomeka 1, 000, 000/ baada ya makato ya wezi huo je litaendelea kusomeka hivyo au litapungua?
 
VRF ama Value retention fee ni gharama za kulinda thamani ya pesa ya mkopaji ambaye ni mwanafunzi. Gharama hii inatozwa pindi mdaiwa anapopitisha kipindi cha marejesho mara baada ya kuhitimu. Kwa kesi ya HESLB walikua wanatoza kiwango cha asilimia sita (6%) kwa kila mdaiwa.
Hivyo basi baada ya tamko la Mh. Rais siku ya Mei mosi, tozo hiyo imetolewa na itafanya wadaiwa wote kulipa kiasi kile kile walichonufaika wakati wa maombi. Kama ulikopa shilingi milioni 5, utarejesha milioni 5 hiyo hiyo bila gharama za ziada.
Mbona nahisi umechanganya...

Ile 10% ya adhabu ni nini?

Ile inayoongezeka 6% kila mwaka ni nini?
Maana deni lilikua kila ikibadilika mwaka lina panda...

Yaani ulifunga na 100,000/= utashangaa unafungua financial yr na 160,000/=

#YNWA
 
Ni hivi hyo 6% ndo ilikuwa value retention fee ambayo ndo imeondolewa na hyo 10% ni adhabu ya kupitisha miezi 24 bila kulipa for now utalipa ulichokopeshwa.
 
VRF ama Value retention fee ni gharama za kulinda thamani ya pesa ya mkopaji ambaye ni mwanafunzi. Gharama hii inatozwa pindi mdaiwa anapopitisha kipindi cha marejesho mara baada ya kuhitimu.

Kwa kesi ya HESLB walikua wanatoza kiwango cha asilimia sita (6%) kwa kila mdaiwa.

Hivyo basi baada ya tamko la Mh. Rais siku ya Mei mosi, tozo hiyo imetolewa na itafanya wadaiwa wote kulipa kiasi kile kile walichonufaika wakati wa maombi. Kama ulikopa shilingi milioni 5, utarejesha milioni 5 hiyo hiyo bila gharama za ziada.

Unasema ukwel mnufaika atalipa kiasi kile kile?mbona wanufaika wengi wanalalamika kwamba vrf ya miaka ya nyuma haijafutwa?
 
Back
Top Bottom