Kwanza nichukue fursa hii kuipongeza serikali ya mhe Samia Suruhu Hassan kwa kujali na kusikiliza kero mbalimbali za walimu.Lakini pia nikipongeze Chama Cha walimu Tanzania CWT kwa yale mliyoafikiana na serikali.
Hoja yangu ni hii CWT imesema serikali imeridhia kuwapa madaraja ya Mseleleko walimu takribani elfu 50,hawa ni wale waliopaswa kupanda madaraja 2016/2017, ni jambo jema na la kupongezwa.
Lakini serikali na CWT wasisahau kuna walimu waliopaswa kupanda madaraja mwaka 2018 hawakupanda badala yake walikuja kupandishwa mwaka 2021, yaani takribani miaka Saba wametumikia cheo kimoja mfano halisi ni watu waliopanda daraja mwaka 2015 mara ya mwisho wamekuja kupandishwa tena mwaka 2021.
Kwa maoni yangu CWT na Serikali wanapaswa kuwajali watumishi hao pia.