Kuibuka kwa "Dunia ya Kusini" kumeleta mabadiliko makubwa duniani na kuielekeza dunia kwenye mustakbali mzuri

Kuibuka kwa "Dunia ya Kusini" kumeleta mabadiliko makubwa duniani na kuielekeza dunia kwenye mustakbali mzuri

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,116
Reaction score
1,121
1732153154723.png


Tangu kuingia karne ya ishirini na moja, nchi za "Dunia ya Kusini" zimeanza kubadilika hatua kwa hatua kutoka nchi nyingi zenye ukimya mkubwa hadi kuwa nguvu kuu inayoendesha mabadiliko katika utaratibu wa kimataifa.

Nchi na mashirika ya kimataifa kutoka Kusini, kama vile China, India, Umoja wa Afrika, na ASEAN, sio tu kwamba zimepiga hatua kubwa katika maendeleo yao bali pia zimekuwa wahusika wakubwa wa kuleta mabadiliko muhimu kwenye mazingira ya kimataifa, kuweka sawa hali za kikanda, na hata kukuza ushirikiano baina ya mataifa makubwa.

Kutokana na maendeleo haya, imefanya hata nchi zilizoendelea zinazowakilishwa na Marekani, Ulaya, na Japan kutambua uwezo mkubwa wa "Dunia ya Kusini".

Katika miaka ya hivi karibuni, mifumo ya usimamizi duniani ilishindwa kukabiliana kikamilifu na changamoto za kimataifa, na kusababisha kuongezeka kwa tatizo moja juu ya jingine. Hivyo kushindwa kwa mfumo wa kimataifa kukazima kama mshumaa azma ya nchi mbalimbali ya kudumisha usalama wa kikanda na kukuza ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara katika ngazi ya kikanda, jambo ambalo lilitoa nafasi ya kuanzishwa kwa mifumo mbalimbali kama vile FOCAC, BRI, BRICS, kwa ajili ya kutoa sauti ya nchi za "Dunia ya Kusini" na nchi zinazoendelea.

Kuinuka kwa pamoja kwa "Dunia ya Kusini" ni kiashiria tosha cha mabadiliko makubwa kote duniani. Leo hii nchi za "Dunia ya Kusini" zinawakilisha zaidi ya asilimia 70 ya watu duniani, na zaidi ya asilimia 40 ya Pato la Taifa la dunia.

BRICS, ambayo hivi karibuni ilifanya Mkutano wake wa 16 huko Kazan, Russia kuanzia Oktoba 22 hadi 24, iko mstari wa mbele katika nchi za "Dunia ya Kusini" ikilenga kuunganisha hekima za pamoja ili kufungua matarajio mapya ya maendeleo na ustawi kwa nchi zote zinazoendelea.

Katika mkutano huo, China ilitoa wito kwa nchi za BRICS kudumisha amani, kujitahidi kuleta usalama wa pamoja na ustawi wa pamoja na kuhimiza kustawisha ustaarabu duniani. Mapendekezo haya yanajibu hitaji la dharura la "Dunia ya Kusini" juu ya amani, maendeleo na ushirikiano, na yanawiana na Mpango wa Maendeleo wa Dunia, Mpango wa Usalama wa Kimataifa na Mpango wa Ustaarabu wa Kimataifa iliyotolewa na China.

Wakati huohuo itambulike kuwa juhudi za China kuhamasisha umoja na ushirikiano kati ya nchi za "Dunia ya Kusini" hazilengi kuzikabili nchi za Magharibi, bali zinalenga kupunguza pengo la Kaskazini-Kusini, kuhimiza maendeleo ya kimataifa yenye uwiano na jumuishi, na hatimaye kufikia lengo la maendeleo ya pamoja duniani.

Kama nchi kubwa zaidi inayoendelea na yenye uchumi mkubwa ndani ya nchi za "Dunia ya Kusini", China ina nafasi na wajibu wa kipekee katika kukuza maendeleo, ushirikiano, na utawala wa mataifa ya Kusini. Ikiwa na azma ya kusaidia maendeleo barani Afrika, katika mkutano wa kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) uliofanyika mwezi Septemba mjini Beijing, rais Xi Jinping alizindua hatua kumi za ushirikiano katika kuungana mkono na Afrika ili kuendeleza mambo ya kisasa katika miaka mitatu ijayo, ambapo aliahidi kutoa msaada wa fedha yuan bilioni 360 (sawa na dola bilioni 49.7)

Pia katika hotuba aliyoitoa kwenye Kikao cha I cha Mkutano wa 19 wa G20 kuhusu Mapambano dhidi ya Njaa na Umaskini, yenye kichwa "Kujenga Dunia ya Haki ya Maendeleo ya Pamoja," Xi akiwa mmoja wa viongozi kutoka nchi za "Dunia ya Kusini", alibainisha kuwa katika mkutano wa kilele wa Hangzhou, kwa mara ya kwanza China iliweka maendeleo kama kiini cha uratibu wa sera ya uchumi mkuu wa G20, ambapo toka wakati huo viongozi wa G20 wamekuwa wakifanyia kazi lengo moja, ambalo ni kujenga dunia ya maendeleo ya pamoja.

Kwa mantiki hiyo kuwepo kwa nchi za "Dunia ya Kusini", na maono yake ya utaratibu wa kimataifa, vinatukumbusha kuwa amani na maendeleo bado vitaendelea kuwa matakwa makuu ya jumuiya ya kimataifa na pia kuonesha mchango wake katika kujenga dunia itakayokuwa na mustakbali mzuri.
 
Back
Top Bottom