Kuibuka kwa suala la bandari ya Bagamoyo ni uthibitisho kuwa Kikwete ndo anaeongoza nchi kwa sasa!

Kuibuka kwa suala la bandari ya Bagamoyo ni uthibitisho kuwa Kikwete ndo anaeongoza nchi kwa sasa!

Hata kama amefariki lazima tuseme ili waliopo wajifunze

1. Alikuwa mtu mwenye roho mbaya, mshenzi, muuaji na aliyependa kuona watu wenye maendeleo au waliotofautiana nae wakiteseka sana. Mfano wa haya ni kwa vile walivyowafanyia Manji, Erick Kabendera, Ben saanane, Rwabaje, Mama yake Erick Kabendera, Mdude Nyangali, Zacharia na watu wengine wengi

2. Alikuwa mtu Mbinafsi sana, aliyependa sifa zote zirudi kwake. Alipenda kusifiwa, kuonekana yeye ni bora kuliko wenzake. Hata kwenye hotuba zake alipenda kujionesha ni yeye zaidi na wala sio wenzake. Rejea hotuba alizokuwa akisema bila yeye miradi haitofanikiwa. Aliwapa vyeo bila aibu watu waliokuwa wakimsifu yeye binafsi. Mf. Katambi, Sabaya, kafulila, Mrema, Babu

3. Alikuwa mkabila na mbaguzi wa kikanda aliyetukuka. Kwenye awamu yake alijaza watu wa kanda ya ziwa hasa wasukuma na mapandikizi wenzake kutoka Rwanda na Burundi kwenye nafasi nyeti serikalini. Bashiru, Kakoko, Doto James na wengineo wengi ni mifano michache tu. Hawa watu walikuwa hawagusiki na waliweza kufanya lolote lile kwa jina lake na yeye hakusema lolote. Hawa watu waliweza hata kuwadharau waziwazi Waziri Mkuu na Makamu wa Rais na wala hawakujali mfumo wa utendaji serikalini. Waliweza kupiga simu au kupita moja Kwa moja ikulu hadi kwa Magufuli bila kupita kwa waziri, waziri mkuu au hata Makamu wa Rais.

4. Kwa kujua kwake kuwa ni kweli aliharibu uchumi wa nchi kwa sera zake mbaya, aliwekeza sana kwenye propaganda za kujitangaza sana kupitia vyombo vya Habari ili kuwa brainwash watu wasiofikiri vizuri. Tv zote, magazeti, blogu na hata viongozi wa dini aliwatumia kumtangaza yeye muda wote na kumsifu yeye muda wote ili aonekane ni Bora kuliko wenzake. Ofisi za Taifa zilifanywa kutengeneza data za uongo ili aonekane anafanya vizuri kumbe nchi ilikuwa inaenda pabaya sana. Rejea taarifa aliyotoaga kuwa ATCL inapata faida ya bil 28.

5. Aliwadharau sana wenzake. Na alifanya kila jitihada wenzake waonekane watu wasiofaa ( hasa viongozi waliopita). Aliishi nao kiunafiki akiwatumia vijana wake Kama Msiba, Sabaya , Makonda na Aly Happi kuwatukana na kuwatisha ili aharibu taswira yao kwa jamii na ajitengeneze kuwa ni Bora kuliko wao.

6. Alianzisha mambo ili kuwakomoa watu waliokuwa tofauti nae. As Kofi niwemugizi, Aidan Eyakuze, Yusuph Manji ni wachache kwenye hii list, walianza kuhojiwa uraia, wakanyang’anywa passport na kupewa kesi mbalimbali ili kukomolewa kutokana na kutofautiana nae.

7. Kwa sera zake mbovu, aliharibu kwa kiasi kikubwa uchumi hivyo kupelekea kuwepo tatizo kubwa la ajira . Ili kujiokoa na Tatizo hili Kwa kuwapumbaza watanzania wajinga alianzisha utaratibu wa kujifanya kuwa karibu na Mama lishe na bodaboda huku akisema kuwa wanaruhusiwa kufanya Biashara popote pale. Alifanya hili Kwa sababu alijua kabisa kuwa ameharibu uchumi wa Tanzania na amesababisha watu wengi kukosa ajira. Kuepuka lawama akataka kuifanya nchi nzima kuwa nchi ya wachuuzi huku akiharibu mipango miji na kusababisha walipa kodi wapungue kwa kasi.

8. Kutokana na kuwa na sera mbovu za kiuchumi huku akiiba Mali za watanzania Kwa kigezo cha uzalendo, akiogopa kupinduliwa na jeshi na wasaidizi wake, aliamua kufuatilia maongezi ya wasaidizi wake wote akiwemo Makamu wa Raisi , Mawaziri na viongozi wa Ccm. Alikuwa hadi meseji zao anasoma na alivyo mshamba alikiri hadharani kuwa anafuatilia mawasiliano ya watu. Alianzisha pia utaratibu wa wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama kuwa nae popote pale anapokuwepo. Huu utaratibu ulikuja kuonekana katika awamu ya 5 tu maana Kwa awamu ya 1 hadi ya 4 haikuwai kutokea wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama pamoja na spika na Jaji mkuu kuambatana na Rais popote pale anapokuwa.

9. Alikuwa muuaji
Niliwai bishia watu wengi kwenye hili ila nilikuja kuthibitisha alipokuja tamka hadharani kuwa huwezi kuwa msaliti alafu uka survive na baada ya hotuba yake iyo Tundu Lissu alikuja kushambuliwa kwa Risasi 38 huku 16 zikiingia mwilini wake.

10. Alijiona ni Bora kuliko mtu yeyote yule na alitaka neno lake ndo liwe mwisho. Alisema hadharani kuwa hashauriki na kila mtu aliyekuwa akimshauri alimchukulia kama adui yake. Siku za mwisho za uhai wake alitofautiana na kupingana Hadi na viongozi wa dini wa kanisa katoliki ambao waliamua kushauri nchi kuchukua hatua tofauti dhidi ya corona.

Mungu fundi sana! Alale anapostahili mwendazake.
Mtasema yote lakini msiba wake umewaumbua Sana. Umeonyesha namna gani mtu huyu alipendwa na watanzania walio wengi na kuchukiwa na genge dogo la mafisadi, wauza unga, misheni town, wahujumu uchumi na vyeti feki.
 
Mtasema yote lakini msiba wake umewaumbua Sana. Umeonyesha namna gani mtu huyu alipendwa na watanzania walio wengi na kuchukiwa na genge dogo la mafisadi, wauza unga, misheni town, wahujumu uchumi na vyeti feki.
Wengi waliudhuria so kwa walimpenda ila kujihakikishia kama kweli kafaa.
 
Mtasema yote lakini msiba wake umewaumbua Sana. Umeonyesha namna gani mtu huyu alipendwa na watanzania walio wengi na kuchukiwa na genge dogo la mafisadi, wauza unga, misheni town, wahujumu uchumi na vyeti feki.
Mimi mwenyewe sikumkubali kabisa kwa ajili ya ukabila na double standard za kina Makonda basi nilipenya mpaka bandani kuhakikisha mwendazake ni yeye aliyelala.
Maana katika Hotuba ya Uhuru Kenyatta ali-pause kupisha Adhana basi tulinyong;onyea baada ja fununu kutufikia kuwa jamaa kafufuka.
Sio wote tulioandamana tulilia bali kilio cha mamba na bia zetu kichwani
sasa tunamsahau kabisa
 
Mtasema yote lakini msiba wake umewaumbua Sana. Umeonyesha namna gani mtu huyu alipendwa na watanzania walio wengi na kuchukiwa na genge dogo la mafisadi, wauza unga, misheni town, wahujumu uchumi na vyeti feki.
Mie na kundi langu tulienda barabarani kuangalia na kufurahia kuwa mshenzi kafa
 
Nadhani tanzania tuna kosa sera na mipango ya maendeleo kulingana na mahitaji na uwezo tulio kuwa nao wa kifedha, bandari ya dar bado ina kidhi mahitaji yetu kwasasa, hivyo kwa mipango ya baadae labda mradi wa bandari huu wa bagamoyo ungepelekwa tanga au mtwara,
Tanga ni karibu na nchi za uganda , rwanda na burundi pamoja na drc
 
Lakini wachina si ndio marafiki zetu au umesahau mara hii?
Hao Wachina na Bagamoyo km ikishindikana nimuombe Mam awachukue
Rais wangu Mama Samia achana na Madaraja ya Busisi, mara Bandari ya Bagamoyo ya Matrilioni tujengee daraja la BAGAMOYO - ZANZIBAR kilomita 35 tu, mpe Mchina
kwa muda huo tutakukumbuka kuliko wote waliokutangulia
Maana utuunganisha Muungano kwa vitendo, tutaenda hata kwa daladala na baiskeli kukutembelea
Lakini nili li SGR matrilioni 11 eti Mwanza isaka wenzako walitaka wakamuone Kagame
 
Safi sana kama kikwete ndio anaongoza kwa ss. Bagamoyo kuchele
 
Hivi karibuni kumeibuka suala la bandari ya bagamoyo ambayo mh. Hayati JPM alilikataa kwa kuwa mkataba wake ulikuwa wa kinyonyaji.

Hivi karibuni suala hilo limeibuka tena upya na spika wa bunge ameonekana kulikingia kifua na kudiriki kusema kuwa Mh Rais alishauriwa vibaya.

Je, Mh Ndugai ameamua kuwa kibaraka wa mabeberu baada ya hayati kututoka? Au ni mpango mkakati wa Mh. JK ambaye ndo muasisi wa mradi huo kutumia bunge kuuhuisha mradi huo.

Ni dhahiri kuwa JK aliutamani sana mradi huo ili aache legacy kwa watu wake wa Bagamoyo. Kwa kuwa inasemekana ndo mshauri mkubwa kwa mama SSH ataitumia nafasi hiyo kikamilifu kuurudisha!

Hitimisho: Kwa kuwa mkataba huo una sintofahamu kadhaa ni vyema basi ukapitiwa upya ili kuepuka ulaghai wa wachina. Ni aibu kubwa kwa viongozi wetu wa karne ya 21 kuingia kwenye bogus treaties km kina Mangungo wa msowero!
Yawezekana uko sawa, lakini za kuambiwa changanya na za kwako. Cha msingi hapa kwako ni kupima umuhimu wa bandari hiyo kwako na kwa watanzania kwa ujumla. Hili ndio nafikiri lilikuwa kubwa la kuandika hapa, halafu hitimisho ndio ungemwingiza Kikwete. Jaribu tena kutushawishi.
 
Wewe iyo mikataba aliyoingia hayati umewahi kuiona? Una uhakika gani kama sio ya upigaji? Mambo mangapi amesema ambayo yamekuja kuwa sio kweli?

Aliwahi kutuambia ndege zimetengeneza faida ya deal milion kumi na nne juzi CAG anasema ndege zimeingiza hasara kwa miaka 5 mfululuzo. Utamwamini vipi mtu kama huyu?
Acheni uhuni soma vzr report ya CAG hasara za air tanzania ni madeni ya kurithi na mengine ni matatizo ya covid muwe mnaacha kuropoka
 
Kuna watu wana maslahi na bandari ya bagamoyo walipelekwa china na kuhahidiwa gonge nono ndio maana wanalilia donge lao. walikuwa wapi kabla Jeshi ajafa na walikuwa nae tena ni viongozi wakubwa na washauri wa Rais. kweli Mnafiki hana kwao watanzania wamebakia mdomo wazi. kweli kikulacho kinguoni mwako.
 
Kwahuo mkataba aliosema hayati hasara ni kubwa kuliko faida!
 
Kabla ya lolote. Tafuta ili ripoti ya huu mradi uisome.

Magu alitulisha matango pori.

Na huu mradi sasa una fanywa Msumbiji.
Kama Msumbiji wamekubali masharti yao hao wachina waacheni wavae msalaba wao; sisi lazima tulinde maslahi yetu.
 
Back
Top Bottom