Kuibuka sasa kwa kashfa ya LUGUMI ni mpango wa Mungu Watanzania wamjue waliomuamini na kumsifia

Kuibuka sasa kwa kashfa ya LUGUMI ni mpango wa Mungu Watanzania wamjue waliomuamini na kumsifia

Hapo miwani ya mbao, Magufuli and his team siyo watu wa kubadiri gia angani, anafanya kazi kwa data, the matter still on Bunge's, naamini na yeye anachunguza - give him time.
Usituletee maswala ya Bunge hapa wakati mmegoma kuwasilisha mkataba kwenye Kamati ya Bunge
 
Haki Huinua Taifa Lakini Dhambi Ni Aibu Kwa Watu Wote.


Rais Tuondolee Hii Dhambi Ya Lugumi Kwasasa
 
UKAWA wanahangaika kusubiri mkono udondoke...

Hahahahaha...

Magu kanifanya niitoe hata imani ndogo nliyokuwa nayo kwa vyama vya upinzani....
 
Watoto yatima hawakupenda kuwa hivyooooo..... kabla hujafa hujaumbika ..
Fikiria kwanza kabla ya kutumia mifano yako..
Mh rais hawezi kuingilia kati kabla vyombo husika havijamaliza kazi ,maana PAC ndo ilifuatilia kuhusu huu mkataba ,so lazima asubili maamzi ya PAC kabla ya ku-step in.
 
Hawezi mtumbua huyo.magu hawezi kuifikia kasi ya hayati sokoine hata robo.
 
sijaona hata raia unaosema wanamkubali magufli namba zake za kukubalika zimeshuka sana baada ya kuchagua mabishoo wapiga dili kama akina Muhongo Mwigulu January Makamba Nape, Jenestina Mhagama and so fourth kwa kweli hana nyimbo wamebaki wapiga mapambio tu
Sasa wewe uko kwenye familia ya mbowe utamkuta anae kubali utendaji wa magu kweli?
 
Rais Magufuli atafumua mfumo mzima. CCM imezaliwa upya baada ya mafisadi kuwajibishwa


kila baada ya miaka 50 inazaliwa upya.


kweli toka chaguo la mungu saiv ni sokoine na nyerere.....
 
Ata ile Tenda ya kuangiza magari 700 ya maji ya kuwasha tusubiri picha ndio kwanza imeanza tutasikia mengi.
 
ccm ni ileile,..katibu niyule yule mwenyekiti niyuleyule
system ni ileile......ridh1 akitumbuka na kalamagi,......ntahamia ACT kutoka cdm
 
kuna kila dalili ya mh rais kukumbatia huu ufisadi maana hakuna hata dalili ya kumtumba waziri wake au hata kumuweka kando kupisha uchunguzi.
 
Salary Slip mbona unaongea kama umeachishwa kunyonya jana? CAG ameliibua, kamati ya Bunge inafuatilia ukweli wake kufahamu mkataba unasema nini hasa, nini kimekosewa nini kimepatiwa na nani wahusika. Sasa wewe mbona unataka kuvuka mto kabla haujaufikia. Punguza ashki za chuki na subiri kila mamlaka ifanye kazi yake, huo ndio uawala wa sheria, huwezi kuingilia jambo
linaloshughulikiwa na Bunge. Bunge litatoa mapendekezo kama ilivyofanyika kwa Richmond na Escrow. Kama tunataka tukosoe kwa weledi basi angalau tuzifahamu taratibu zinasemaje na tusitake yatokee yanayotokana na ashki zetu.
mkuu ilitakiwa vitendo vichukuliwe haraka kama ambavyo vimechukuliwa kwa watu na matukio mengine has hata kapress ka kinafiki.
 
Usituletee maswala ya Bunge hapa wakati mmegoma kuwasilisha mkataba kwenye Kamati ya Bunge
Naona unanifanyia hasira mimi, unadhani serikali inaendeshwa kwa kuzungusha mikono? Nenda kachukue basi - iwapo haumwamini mwakilishi wako "bunge"
 
Mh rais hawekufanyailia kati kabla vyombo husika havijamaliza kazi ,maana PAC ndo ilifuatilia kuhusu huu mkataba ,so lazima asubili maamzi ya PAC kabla ya ku-step in.
Bunge sio chombo cha uchunguzi cha serikali. Hiyo kazi inapaswa kufanywa na TAKUKURU, ila Bunge huingilia kati pale ambapo serikali imeshindwa au haitaki kuchukua hatua kama msimazi wa serikali (complimentary). Tangu lini Bunge ikaachiwa kuchunguza makosa ya jinai? Mbona wale wabunge waliotuhumiwa kwa rushwa wamefunguliwa mashtaka wakati Bunge nalo lina utaratibu wa kuwawajibisha wabunge?
 
Mungu ana makusudio kwa watu wake waliokuwa wameanza kulishwa matango pori kupitia vyombo vya habari kuwa amepatika malaika tena mtenda haki asiyestahili hata kukoselewa na ukimkusoa wewe si mzalendo bali una wivu tu na chuki dhidi yake.

Tumeaminishwa haangali sura,hana chama,anasimamia haki,hamuogopi mtu, n.k na zaidi tumuombe kwa mungu.

Hata hivyo,limeibuka jambo ambalo litawasaidi wengi kama si wote kujua ukweli halisi kuhusu mtu huyu na kama kweli anafanya mambo yanayostahili yeye kuombewa.

Mungu aliona asisubiri sana maana watu wake wanazidi kupotea.

NB: Kupitia mungu huyo huyo,vice versa is also true.

Tusubiri.
Jombaaaa! Tulia.
 
Salary Slip mbona unaongea kama umeachishwa kunyonya jana? CAG ameliibua, kamati ya Bunge inafuatilia ukweli wake kufahamu mkataba unasema nini hasa, nini kimekosewa nini kimepatiwa na nani wahusika. Sasa wewe mbona unataka kuvuka mto kabla haujaufikia. Punguza ashki za chuki na subiri kila mamlaka ifanye kazi yake, huo ndio uawala wa sheria, huwezi kuingilia jambo linaloshughulikiwa na Bunge. Bunge litatoa mapendekezo kama ilivyofanyika kwa Richmond na Escrow. Kama tunataka tukosoe kwa weledi basi angalau tuzifahamu taratibu zinasemaje na tusitake yatokee yanayotokana na ashki zetu.
Ashki hata wewe unazo, acha kushauka. Kuna watu waliwekwa kizuizini immediately baada ya mambo yao kuibuliwa ili wasitoroke, je hawa hawawezi kutoroka?

Au unataka kuniambia wewe hapa jukwaani ndio unaweza saaaana kiasi uone matusi ya ashki yanatustahili wote tunaodhani kwamba 'wamesimamishwa kupisha uchunguzi' was the right move?

Kumbe mkiguswa wakali eeeh!
 
Naonserikaifanyia hasira mimi, unadhani serikali inaendeshwa kwa kuzungusha mikono? Nenda kachukue basi - iwapo haumwamini mwakilishi wako "bunge"
Elewa hivi, "Bunge sio chombo cha uchunguzi cha serikali katika makosa ya jinai bali hiyo kazi hufanywa na polisi na TAKUKURU kwa mujibu wa sheria. Bunge huingilia tu kati kama msimamizi wa serikali pale ambapo serikali imeshindwa au haitaki kuchukua hatua ndo maana Bunge hutoa maazimio kuilazimisha serikali kuchukua hatua. Hata huo uchunguzi wa Bunge hauwezi kutumika dhidi ya mtuhumiwa mahakamani ni kwa ajili tu ya Kamati kujiridhisha na ubadhilifu ili kutoa mapendekezo ili kupeleka bungeni kwa ajili ya maazimio ya Bunge. Kwa hiyo hapo unamaanisha kwamba serikali inasubiri maazimio ya Bunge ndo ichukue hatua?
 
mkuu ilitakiwa vitendo vichukuliwe haraka kama ambavyo vimechukuliwa kwa watu na matukio mengine has hata kapress ka kinafiki.

Ndio maana nasema kuna umuhimu wa kujua utendaji kazi wa Taasisi zetu mbalimbali. Hapa swala lilipo si katika utndaji wa mhimili wa exuctive kwa maana rahisi 'serikali'. Lipo katika mamlaka ya Bunge na bunge kazi yake ni kuisimamia serikali. Bunge inachokifanya ni kujiridhisha kama serikali imetenda ipasavyo au la. Kama haijatenda ipasavyo bunge litatoa maagizo kwa serikali na mapendekezo kadri itavyoona inafaa. Serikali kwa upande wake itatumia 'machinery' zake kuona kama wasiwasi wa bunge ni valid au la hapo sasa serikali itafanya kazi yake accordingly na kujibu maazimio ya Bunge. Huo ndio utawala wa sheria tulio nao na ndio tuufatao. Kama tunataka mwingine basi tubadili katiba na sheria, lakini muda huu ni huu huu.
 
Sasa mbona mnakua vigeugeu, akifukuza mnasema anapapara, akiacha uchunguzi ufanyike mnasema anaogopa baadhi ya watu. Hivi nyie cdm mnataka nini hasa?mbona hamueleweki.
 
Ashki hata wewe unazo, acha kushauka. Kuna watu waliwekwa kizuizini immediately baada ya mambo yao kuibuliwa ili wasitoroke, je hawa hawawezi kutoroka?

Au unataka kuniambia wewe hapa jukwaani ndio unaweza saaaana kiasi uone matusi ya ashki yanatustahili wote tunaodhani kwamba 'wamesimamishwa kupisha uchunguzi' was the right move?

Kumbe mkiguswa wakali eeeh!

Kama hufahamu taratibu na unataka lile la hamu yako ndilo lifanyike basi unatumwa na ashki zako na wala si maarifa yako. Mimi pia nina ashki zangu ukizitaka utazipata.

Nani aliyewekwa kizuizini ishu zake zilipoibuliwa? Mtaje ilituweze kuzifananisha ishu na tufahamu ilikuwa chinaa ya mamlaka ipi. Hii ishu kweli ni yenye kutia shaka lakini bayana ya mashaka utapatikana baada ya kamati ya Bunge kupitia mkataba. Ishu iko chini ya Bunge,bado haijafika serikalini. Serikali inaweza ikapewa maagizo na bunge ifuatilie. Huwezi kumkamata mtu eti kwa vile tu fulani ana wasiwasi nae. Itaangaliwa kama taratibu za zabuni zilifuatwa, kama hazikufuatwa nani alihusika, kwa nini vifaa havijafungwa pamoja na pesa asilimi 99 kulipwa. Actually kuna maswali kadhaa ya kujibiwa likiwemo ni akina nani hasa wahusika. Kama hata wahusika hawajajulikana bayana nani sasa akamatwe? Kama kweli tunataka utawala wa sheria basi hatuna budi kuisubiri na kuivumilia sheria hata kama ashki zetu zinataka kwa uharaka namna gani. Tukiendekeza ashki na tukadharau sheria matokeo yake ni hatari kubwa
 
Back
Top Bottom