Leo Rais Magufuli anasifiwa kwa sababu ana uwezo na ana uthubutu wa kuingilia mhimili wa Bunge na kuweka shinikizo wabunge wahojiwe kwa rushwa. Kesho Rais huyo huyo anashindwa kusaidia mhimili huo huo upate taarifa za ufisadi.
Wapiga vigelegele hawakosi sababu.
Suala la Lugumi linahusisha Mhimili wake mwenyewe, tena moja kwa moja (the executive). Waziri wa mambo ya ndani, IGP, Katibu Mkuu, ni wateule wa Rais. Waziri husika - ambae anahusishwa na tuhuma kupitia kampuni yake ya infosys, ndio bosi wa IGP na Katibu Mkuu ambao tunawatupia lawama juu ya hili.
Mwisho wa siku, wa kulaumiwa ni Rais Magufuli. Katibu mkuu na IGP wapo chini ya Waziri Kitwanga, mshirika kibiashara wa Lugumi. Ni sahihi kupiga danadana na nyaraka husika kwa kufuatana na Kiapo chao cha kazi kwa aliyewateua - Rais!
Kitendo cha Rais kutotengua UWaziri wa Kitwangwa lazima kizuie watendaji wake (Katibu Mkuu na IGP) kutoa ushirikiano kwani ukimya wa Rais maana yake ni kwamba mamlaka ya uteuzi (Rais) hajaridhia. Wangekuwa wamethibitishwa uteuzi wao na Bunge tungekuwa mbali na hili. Lakini Katiba ya wananchi hamtaki, na Rais Magufuli alishadokeza kwamba katiba ya Chenge ndio sahihi.
Suluhisho la suala hili lazima lianze na Rais mwenyewe. Anze kwa kutengua uwaziri wa Kitwanga kwanza, then rest will return to equilibrium.
Tusiwalaumu IGP na Katibu Mkuu mambo ya ndani bali Rais Magufuli kwa ukimya wake ambao tafsiri huko polisi na wizarani lazima iwe "Bwana mkubwa hajaridhia". Vinginevyo mtakuwa "Majipu".