Watu wengine wanakesha kumuombea JPM mabaya...... Yeye pia ni binadamu ana mapungufu yake.... lakini suala la kutumbua majipu acha aendelee tuuu. Maana nchi ilifikia pabaya ilikuwa zaidi ya shamba la bibi.
Kuhusu naye kuwa na kashfa.... mimi kwangu sishangai.... kwa maana kwa awamu iliyopita ilikuwa imechafuka hivi kwamba kwa yeyote aliyekuwa anahudumu hata kama ni msafi namna gani hataweza nusurika, japo harufu ya uchafu utaipata.
Mimi nimekulia kijijini, mara nyingi tulikuwa tunapakia mbolea ya samadi kwenye trekta toka nyumbani kwenda shambani umbali wa kati ya kilometa 4 mpaka 8, siku zote trekta hilo lilikuwa chafu sana, hivi kwamba mtu yeyote atakayepanda trekta hilo lazima achafuke tu, hata akiwa amevaa suti au suruali ya Michael Jackson au Zico (Vikali vya miaka hiyo kwa wale waliokuwa wakijitambua miaka ya themanini na mwanzoni mwa tisini) lazima uchafuke tu.
Ndivyo ilivyokuwa serikali iliyopita, hata kama hupendi kuchafuka, utachafuka tu. Kuna watu wengi ambao hawakuwa wakipenda ufisadi na rushwa bali walipenda unyoofu lakini walilazimishwa moja kwa moja au na mazingira kuiba mali ya umma.
Hivyo maoni yangu mimi binafsi awe JPM alishiriki au hakushiriki kuiba mali ya umma, mimi binafsi namsamehe. Na sababu kubwa ya kumsamehe ni kwamba ameirudishia nchi heshima kwa kutofumbia macho vitu vingi tu vya kijinga ambavyo vilikuwa ni vya hovyo na ambavyo vilikuwa vikihujumu mali ya umma. Nina uhakika hata wewe uliyeleta hii mada unaona utofauti uliopo kati ya awamu hizi ambazo nchi yetu ilipitia.
Kwa wananchi wote wapenda maendeleo na wanaoitakia mema nchi yetu ya Tanzania, wanakubali na wanafurahia jinsi JPM anavyoshughuluka na matatizo ya nchi hii.
Nomba kuwasilisha.
eli.