Kuibuka sasa kwa kashfa ya LUGUMI ni mpango wa Mungu Watanzania wamjue waliomuamini na kumsifia

Ya balali na epa yalikuwa hivi hivi,tukajaambiwa wahusika wakikamatwa au kutajwa majina yao nchi itaangamia.
 
"Mkikamata mafisadi wa EPA nchi italipuka" - IGP Mstaafu.
Kumbuka huyu bwana alikuwa amekula kiapo cha utiifu wakati akiyasema haya, na mlango wa nyuma aliyajua haya ya Lugumi pia. Kama viongozi wanawekwa na Mungu na wanaishia kufanya haya si ajabu ndio maana nchi yetu inaendelea kuandamwa na laana.
shetani ananafasi kubwa sana ya kuwaweka viongozi hasa wa kidunia kuliko hata Mungu! Ni kiongozi yupi amewekwa na Mungu?
 
jipu la lugumi limekaa pabaya sana
Lina tumbulika vizuri tu. Ni kiasi cha kufanya maamuzi. Osama pamoja na jeshi lake alipatikana sembuse muosha viatu. Wapeni kazi Interpol muone kama kesho asubuhi na mapema hajarudishwa.
 
Nyuma yake kuna foleni mpaka mkuu wa polisi mstaafu,hadi prince,unaweza kuta mpaka mfalme anakumbwa
 
Halafu kuna watu walikuwa wanalegezwa na kuamini maneno ya Rais kwamba amelitendea mema Taifa. Lile swali lake la "Kwani nimechomeka wapi? " Jibu lake ni "Kwa Lugumi."
 
Mungu ana makusudio kwa watu wake waliokuwa wameanza kulishwa matango pori kupitia vyombo vya habari kuwa amepatikana malaika tena mtenda haki asiyestahili hata kukoselewa na ukimkusoa wewe si mzalendo bali una wivu tu na chuki dhidi yake.

Tumeaminishwa haangali sura,hana chama, anasimamia haki,hamuogopi mtu, n.k na zaidi tumuombe kwa mungu.

Hata hivyo,limeibuka jambo ambalo litawasaidia wengi kama si wote kujua ukweli halisi kuhusu mtu huyu na kama kweli anafanya mambo yanayostahili yeye kuombewa.

Mungu aliona asisubiri sana maana watu wake wanazidi kupotea-the earlier the better.

NB: Kupitia mungu huyo huyo,vice versa is also true.

Tusubiri.
Wacha ujuha wako humu JF, tumo watu waelewa, mkataba wa lugumi ni wa mwaka 2011, Je unataka kutuambia nini hapo mnafiki wewe?
 
Kasi ya kumtimua Mama Kilango ilifurahisha lakini Ligumi mhaaa haaa ha aaa eti Tanzania tumempata Sokoine wetu hata 2% bado hajamfikia.
Ukiwa, monduli, kina Kitillya team etc, bado mtatumbuliwa tu, msifanye diverting hapa ni kazi tu
 
Wanaogopa kulamba moto maana hawajui utawaunguza vipi. Mkuu usisahau ile kauli ya na wapigwe tu tumechoka AKA Pinda alipodai kwamba mafisadi wa EPA ni matajiri wakubwa sana nchini kama wakikamatwa basi nchi itawaka moto, si ajabu na hawa mafisadi wa Lugumi ni watu wazito sana nchini kama wakikamatwa basi nchi itawaka moto na kuwa na mtikisiko mkubwa sana ambao haujawahi kutokea nchini katika miaka 55 ya uhuru wa Tanganyika hivyo ni bora wajinyamazie tu kama vile hawajui nini kinaendelea kuhusu Lugumi na mabilioni yake haramu.

Kwa tuhuma hizi nzito nilitarajia kusikia watu fulani wamesimamishwa au teuzi zao zimetenguliwa ila cha ajabu bado wako ofisini alafu tunaambiwa tumempata Sokoine!!!
 
Wanaogopa kulamba moto maana hawajui utawaunguza vipi. Mkuu usisahau ile kauli ya na wapigwe tu tumechoka AKA Pinda alipodai kwamba mafisadi wa EPA ni matajiri wakubwa sana nchini kama wakikamatwa basi nchi itawaka moto, si ajabu na hawa mafisadi wa Lugumi ni watu wazito sana nchini kama wakikamatwa basi nchi itawaka moto na kuwa na mtikisiko mkubwa sana ambao haujawahi kutokea nchini katika miaka 55 ya uhuru wa Tanganyika hivyo ni bora wajinyamazie tu kama vile hawajui nini kinaendelea kuhusu Lugumi na mabilioni yake haramu.
Suala hapa ni UKWELI wa watawala, kama JPM angekuwa sehemu ya hii kashfa ya lugumi asingeruhusu iende bungeni huku akijua wabunge walio wengi wana hasira ya kukatwa mafao yao yaani marupurupu, ikiwemo ziara za nje ya nchi nk, Ndio maana ana uhakika wa kuacha mambo hadharani
 
Mkikamata mafisadi wa EPA nchi italipuka" - IGP Mstaafu

Tafadhali jitahidi kuandia vitu ambavyo una uhakika navyo, hayo maneno hayakutamkwa na huyo unaemwita IGP mstaafu bali yalitamkwa na waziri mkuu mstaafu MTOTO WA MKULIMA Pinda!!!
 
Sasa bila shaka anayo majina ya wahusika ndani ya polisi na wizara ya mambo ya ndani ambao bado wako kazini kwanini hawasimamishi kazi hawa bila mshahara ili kupisha uchunguzi wa kina? wakiendelea kuwepo kwenye nyadhifa zao wanaweza kabisa kutumia nyadhifa zao kuharibu ushahidi. Na iweje huo mkataba unakuwa mgumu hivyo kuwakilishwa kwa Wabunge na kamati husika? tatizo ni nini? Kama umeshaibwa si waseme tu kama mkataba umepotea badala ya kujibaraguza baraguza huku na kule?

Suala hapa ni UKWELI wa watawala, kama JPM angekuwa sehemu ya hii kashfa ya lugumi asingeruhusu iende bungeni huku akijua wabunge walio wengi wana hasira ya kukatwa mafao yao yaani marupurupu, ikiwemo ziara za nje ya nchi nk, Ndio maana ana uhakika wa kuacha mambo hadharani
 
Jeshi la polisi ni jipu..tunamwomba rais achunguze zaidi mamlaka hii ni jipu kubwa sana hapa nchini
 
Ni kweli hayakutamkwa naye lakini siku yalipotamkwa alikuwepo pamoja na mwanasheria mkuu wa Serikali pia alikuwepo wote hawa walikuwa na Pinda alipoyatamka maneno yale.

Tafadhali jitahidi kuandia vitu ambavyo una uhakika navyo, hayo maneno hayakutamkwa na huyo unaemwita IGP mstaafu bali yalitamkwa na waziri mkuu mstaafu MTOTO WA MKULIMA Pinda!!!
 
Awali tulisema hatua ya wahusika kuutoa mkataba husika kutoka PAC kwenda kamati ya ulinzi na usalama ililenga nini - kugeuza suala husika kuwa ni la siri na sio la media/public kama ilivyo kwa kazi za kamati nyingine.

Baadae tukaeleza kwamba tusipoteze muda kumlaumu IGP au Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani kwa suala linalomhusu bosi wake (Waziri Mambo ya Ndani) ambae bado mamlaka ya uteuzi haijamwajibisha.

Sasa taarifa iliyopo na ambayo waandishi wa habari wameanza kuipokea ni kwamba:

Katibu mkuu wa wizara ya mambo ya ndani jaji Projest Rwegasira ametoa ya moyoni kuhusu mkataba iliyopewa Lugumi Enterprises Ltd kusambaza vifaa maalum vya kuchukua alama za vidole kwenye vituo vyote vya jeshi la polisi nchini mwaka 2011.

Ndugu Rwegasira amesema kuwa ameagizwa na mamlaka ya juu kuuzuia mkataba kati ya Lugumi Enterprises Ltd na jeshi la polisi kwa madai kuwa kuutoa hadharani kwa wasio husika nao ni kukiuka taratibu za jeshi hilo.

Aidha ndugu Rwegasira amesema kuwa watakaoruhusiwa kuuona mkataba huo ni kamati ya bunge yenye mamlaka na jeshi la polisi nchini ambayo ni ya mambo ya nje, ulinzi na usalama na si vinginevyo.

Tanzania nakupenda kwa moyo wote. Hakika Jina lako ni tamu sana.
 
Haya yote uliyoandika sijaona wapi huyo uliyemlenga anahusika

Lizabomi;
Amekukumbuka ndugu yangu?? Umemtetea sana humu jf, Nilidhani ungeukwaa hata U DC sijasikia. Hakika asipokukumbuka hata hapo, basi muasi yaani Toroka uje ashikishwe adab
 
Wanaogopa kulamba moto maana hawajui utawaunguza vipi. Mkuu usisahau ile kauli ya na wapigwe tu tumechoka AKA Pinda alipodai kwamba mafisadi wa EPA ni matajiri wakubwa sana nchini kama wakikamatwa basi nchi itawaka moto, si ajabu na hawa mafisadi wa Lugumi ni watu wazito sana nchini kama wakikamatwa basi nchi itawaka moto na kuwa na mtikisiko mkubwa sana ambao haujawahi kutokea nchini katika miaka 55 ya uhuru wa Tanganyika hivyo ni bora wajinyamazie tu kama vile hawajui nini kinaendelea kuhusu Lugumi na mabilioni yake haramu.
Mkuu, nina imani yataendelea kuibuka mengi na mazito ambayo Magufuli hatoweza kuyagusa. Hapa leo wameleta kisingizio cha taarifa za majeshi/usalama lakini yataibuka mengine ambayo watakosa kisingizio.Tusubiri na taarifa ya CAG maana nayo itakuja na mengine.

Si muda mrefu watu watamchoka Magufuli.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Awali tulisema hatua ya wahusika kuutoa mkataba husika kutoka PAC kwenda kamati ya ulinzi na usalama ililenga nini - kugeuza suala husika kuwa ni la siri na sio la media/public kama ilivyo kwa kazi za kamati nyingine.

Baadae tukaeleza kwamba tusipoteze muda kumlaumu IGP au Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani kwa suala linalomhusu bosi wake (Waziri Mambo ya Ndani) ambae bado mamlaka ya uteuzi haijamwajibisha.

Sasa taarifa iliyopo na ambayo waandishi wa habari wameanza kuipokea ni kwamba:

Katibu mkuu wa wizara ya mambo ya ndani jaji Projest Rwegasira ametoa ya moyoni kuhusu mkataba iliyopewa Lugumi Enterprises Ltd kusambaza vifaa maalum vya kuchukua alama za vidole kwenye vituo vyote vya jeshi la polisi nchini mwaka 2011.

Ndugu Rwegasira amesema kuwa ameagizwa na mamlaka ya juu kuuzuia mkataba kati ya Lugumi Enterprises Ltd na jeshi la polisi kwa madai kuwa kuutoa hadharani kwa wasio husika nao ni kukiuka taratibu za jeshi hilo.

Aidha ndugu Rwegasira amesema kuwa watakaoruhusiwa kuuona mkataba huo ni kamati ya bunge yenye mamlaka na jeshi la polisi nchini ambayo ni ya mambo ya nje, ulinzi na usalama na si vinginevyo.

Tanzania nakupenda kwa moyo wote. Hakika Jina lako ni tamu sana.

Mkuu,leo nimesoma The Guardian online Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani amekanusha mkataba huo kupelekwa kwenye kamati hiyo ya Mambo ya Nje ili hali jana gazeti la Nipashe liliripoti Mwenyekiti wa Kamati hiyo ya Mambo ya Nje amethibitisha kamati yake kupokea mkataba huo.Sasa unajiuliza kwanini yote haya yanatokea na ni kwa faida ya nani hasa?Magufuli kimyaaa!
 
Back
Top Bottom