Kuifanya League ya Tanzania a Better Product

Logikos

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2014
Posts
15,460
Reaction score
24,233
Camarades, na Wadau wa Mpira.., ni ukweli usiopingika kwamba Ligi yetu haina ushindani na Timu nyingi ni masikini na mashabiki hakuna kutokana na ushindani mdogo...

Kwa ushauri ni kipi kifanyike ili hii Product ipendwe ?, hata English Premier League ilikuwa invented sio zamani 1992 na matokeo yake tumeyaona.. kwa ushauri wangu naona yafuatayo yafanywe :-

Kuongeza Wadhamini
TFF na wadau watafute wadhamini zaidi, hata kuuza TV rights za kila game ili ionyeshwe na kuwashauri wadau wenye makampuni kufadhili league

Kuonyesha kila Game kwenye TV
Kuuza rights za kuonyesha Mpira / Mechi zote kwa Pesa nyingi itakayosaidia kuwekwa kwenye Fungu la Kuzigawia Timu entrance Fee ya Washibi watakaoingia kwenye mpira ni Pesa ndogo kuzitegemea, na hazitatosha.

Kuongeza / Kubadilisha Aina ya Fungu la Kugawia Timu
Badala ya Fungu la kiingilio kugawiwa timu zinazoshinda kwa percent nusu kwa nusu (baada ya makato ya TFF, Uwanja n.k.) Nashauri fedha igawiwe kwa Mafungu ya Percent Kubwa Zaidi kwa Timu itakayoshinda Mchezo husika na Ndogo kwa timu itakayofungwa (endapo Timu zitadraw) basi wote wapewe fungu dogo na zinazobaki ziwekwe kwenye Kapu na kuja kupewa Timu mwisho wa League itakayochukua Kombe.., kwa kufanya hivi nadhani kutapunguza Timu masikini kuuza Mechi; pia kila game itakuwa na maana sababu kushinda game kutakuwa na faida kubwa, kuliko kufungwa

Kuhakikisha / Kusaidia Mashabiki kuwa Regional
Kwa sasa tumeona kwamba zaidi ya Simba na Yanga timu nyingine za mikoani hazina kabisa mashabiki.., kwahio ili kuwe na uzalendo na watu kupenda Timu inasaidia kama Timu itakuwa ina uhusiano mkubwa na mkoa inakotoka.., Kwa mfano kama kila Mkoa ikiwa na Timu yake Mfano Mwanza Heroes; au Igembensabo, au Simiyu Stars.., kwa kuanzia wakazi wa mji husika watakuwa na uhusiano na upendo zaidi na Timu zao na wafadhili local watapatikana zaidi, ingawa hizi Timu zitaruhiwa kusajili kutoka popote na kila mkoa utaruhusiwa kwa na Timu hata zaidi ya moja kwa kuanzia ila mwisho wa ligi zikishuka hata kama mkoa fulani utakuwa hauna timu itaendelea hivyo hivyo. Na kwa kuanzia Timu ambazo zipo tayari kwenye League kina Simba na Yanga n.k. zitaendelea hivyo hivyo ila kila mkoa kwa kuanzia huimizwe kuwa na Timu ya mkoa ambayo ipo kwenye league (na hii itasaidia kupata vipaji kutoka mikoani)

HITIMISHO

Nadhani kwa kufanya hayo italeta uzalendo zaidi na kila game sababu itakuwa na faida kubwa kila mshindi wa game atapata pesa na mwisho wa siku atakayeshinda League mwisho wa mwaka na yeye apate dau la pesa nyingi kulingana na Nafasi atakayomaliza nayo.

Kwa kuwa kila game itakuwa na Price Tag/Kifuta Jasho kikubwa nina uhakika kutakuwa na Ushindani Mkubwa

c.c Jamal Malinzi; Pazi; Mbu; Katavi; Belinda Jacob; Nzi; EMT; na wadau wote wa Soka
 
Last edited by a moderator:
Bidhaa ndio inayovutia wadhamini, bila kuboresha bidhaa wadhamini hawawezi kushawishika kuwekeza kwenye mpira.
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Kunahitajika ushindani wa kweli baina ya timu. Kukiwa na ushindani, ligi itavutia watizamaji. Watizamaji wakivutika, wadhamini watavutika. Wadhamini wakivutika, timu na wachezaji zitapata motisha. Motisha ukipatikana, ushindani halali utaongezeka hata nje ya uwanja. Ushindani halali nje ya uwanja ndio utazaa miundombinu zaidi ya kimpira (viwanja stahiki, akademia za kweli, TV za vilabu na ligi yenyewe, n.k.). Hayo yakitokea,ushindani utaongezeka sambamba na vinavyotokana nao, ad infinitum (hadi milele). Lakini ili hayo yatokee,kunahitajika kutofungamana miongoni mwa wadau wote wa timu (isipokuwa washabiki). Ligi yetu inakosa ushindani kwa sababu wachezaji, waamuzi, wadhamini,viongozi, walimu, madaktari, wanahabari na wadau wengine wote wanafungamana na upande (timu) fulani, hivyo kulazimsha msimamo wa mwisho wa Ligi usio halisi. Tungeweza kuajiri CEO wa Ligi yenyewe kutoka nje ya nchi na kwa hivyo asifungamane na timu yoyote. Lakini hao wadau wengine je? Vinginevyo, matatizo ya sekta ya soka ya hapa kwetu si tofauti sana na (na huenda yakawa ni afadhali zaidi ya) Ligi nyingi nyengine (Nigeria, Ghana, Gabon, Mali, B.Farso, Croatia,USA, n.k.). Ila wao, matatizo yao yanageuka kuwa changamoto kwa sababu wadau hukusanya nguvu zao kunyanyua kiwango cha soka kwa ujumla wake, sio kubeba timu mojamoja kwa maslahi binafsi ya wadau binafsi wenye ubinafsi.
 
Bidhaa ndio inayovutia wadhamini, bila kuboresha bidhaa wadhamini hawawezi kushawishika kuwekeza kwenye mpira.

Wadhamini wanaangalia sana ni wangapi waangalia mechi kwahio kama kila game itakuwa kwenye TV nina uhakika hata coverage itaongezeka..

Alafu nadhani cha muhimu sana ni ushindani; sio sasa zaidi ya Simba na Yanga wengine ni kama wasindikizaji, ndio maana nikashauri kama mgao wa pesa utakuwa unaendana na kila game timu inyoshinda hata zile timu masikini zitacheza kufa na kupona..

Na kuondoa Usimba na Uyanga nadhani Kukiwa na Timu za Mikoa kutaleta ushindani.., kwamba "Dar hawawezi kutufunga Sisi Mwanza" hivyo mashabiki wa Mwanza wote kushabikia Timu zao za Mikoa.., Sio sasa Simba na Yanga ndio wametapakaa Tanzania nzima
 
Sema ukweli, kwa 'uswahili' uliopo katika soka la Tanzania, ni kitambo sana nimeacha kuwa mfuatiliaji wa nini kinaendelea katika soka la bongo.
 
Ushirikina,Hongo,utapeli,tamaa ya madaraka ndio unaharibu soka Kama watu walivyoliharibu neno Waswahili ukirudi 1970 kwenda nyuma neno Waswahili lilikuwa linda maana nzuri kwa vitu Vingi tu sasa hivi limeegemea kwenye sehemu sio. Ni kweli bora tutizame ligi za watu.
 
Nili tegemea Azam wangekuwa Mfano wa kuiga lakini nimeona na wao wanapotea na soon Tutawasahau kwenye Soka.
 
KeyserSoze nimekusoma.Tunashukuru kwa sasa Tv rights za ligi zina mmiliki na anatoa milioni mia moja kwa kila timu kwa msimu,mwenye naming rights naye anatoa fungu zuri kwa kila timu,jitihada zinafanyika kuboresha maslahi ya vilabu.
 
Nili tegemea Azam wangekuwa Mfano wa kuiga lakini nimeona na wao wanapotea na soon Tutawasahau kwenye Soka.

Azam wanapotea kivipi Kibanga?
Binafsi nadhani Azam haitaweza kuwa kama Simba na Yanga na sababu kubwa ni ile association na watu.., yaani Mashabiki wengi hawatakuwa na ile mentality kwamba hii timu ni ya kwetu, bali ni Timu ya Azam; issue kama hii tena imeipata hata Toto ya Mwanza wakazi wengi hawaipendi sababu inaonekana ni Timu ya viongozi wachache..

Ndio maana nikasema kama shinikizo na motisha ikitolewa kwamba kila mkoa waanzishe Timu ya Mkoa ambayo watu wengi watakuwa na mahusiano na Timu husika kwamba ni Timu yao, hii itapelekea watu kuwa wapenzi badala ya kushabikia peke yake.., yaani hata timu ikifanya vibaya. Nadhani bahati hii wanayo England Utamaduni wao ni watu kushabikia Timu zinazotoka sehemu yao
 
Soka la bongo lina changamoto nyingi ambazo zinasababishwa na wenyewe kwa makusudi, sasa kwa sababu zinasababishwa kwa makusudi, tusitarajie soka letu kubadilika kamwe.
 
Je uzalendo na wabongo kutoangalia au kwenda uwanjani kuangalia Timu zao haichangii kuporomoka kwa soka
 
Camarades, na Wadau wa Mpira.., ni ukweli usiopingika kwamba Ligi yetu haina ushindani na Timu nyingi ni masikini na mashabiki hakuna kutokana na ushindani mdogo...

Kwa ushauri ni kipi kifanyike ili hii Product ipendwe ?, hata English Premier League ilikuwa invented sio zamani 1992 na matokeo yake tumeyaona.. kwa ushauri wangu naona yafuatayo yafanywe :-

Kuongeza Wadhamini
TFF na wadau watafute wadhamini zaidi, hata kuuza TV rights za kila game ili ionyeshwe na kuwashauri wadau wenye makampuni kufadhili league

Kuonyesha kila Game kwenye TV
Kuuza rights za kuonyesha Mpira / Mechi zote kwa Pesa nyingi itakayosaidia kuwekwa kwenye Fungu la Kuzigawia Timu entrance Fee ya Washibi watakaoingia kwenye mpira ni Pesa ndogo kuzitegemea, na hazitatosha.

Kuongeza / Kubadilisha Aina ya Fungu la Kugawia Timu
Badala ya Fungu la kiingilio kugawiwa timu zinazoshinda kwa percent nusu kwa nusu (baada ya makato ya TFF, Uwanja n.k.) Nashauri fedha igawiwe kwa Mafungu ya Percent Kubwa Zaidi kwa Timu itakayoshinda Mchezo husika na Ndogo kwa timu itakayofungwa (endapo Timu zitadraw) basi wote wapewe fungu dogo na zinazobaki ziwekwe kwenye Kapu na kuja kupewa Timu mwisho wa League itakayochukua Kombe.., kwa kufanya hivi nadhani kutapunguza Timu masikini kuuza Mechi; pia kila game itakuwa na maana sababu kushinda game kutakuwa na faida kubwa, kuliko kufungwa

Kuhakikisha / Kusaidia Mashabiki kuwa Regional
Kwa sasa tumeona kwamba zaidi ya Simba na Yanga timu nyingine za mikoani hazina kabisa mashabiki.., kwahio ili kuwe na uzalendo na watu kupenda Timu inasaidia kama Timu itakuwa ina uhusiano mkubwa na mkoa inakotoka.., Kwa mfano kama kila Mkoa ikiwa na Timu yake Mfano Mwanza Heroes; au Igembensabo, au Simiyu Stars.., kwa kuanzia wakazi wa mji husika watakuwa na uhusiano na upendo zaidi na Timu zao na wafadhili local watapatikana zaidi, ingawa hizi Timu zitaruhiwa kusajili kutoka popote na kila mkoa utaruhusiwa kwa na Timu hata zaidi ya moja kwa kuanzia ila mwisho wa ligi zikishuka hata kama mkoa fulani utakuwa hauna timu itaendelea hivyo hivyo. Na kwa kuanzia Timu ambazo zipo tayari kwenye League kina Simba na Yanga n.k. zitaendelea hivyo hivyo ila kila mkoa kwa kuanzia huimizwe kuwa na Timu ya mkoa ambayo ipo kwenye league (na hii itasaidia kupata vipaji kutoka mikoani)

HITIMISHO

Nadhani kwa kufanya hayo italeta uzalendo zaidi na kila game sababu itakuwa na faida kubwa kila mshindi wa game atapata pesa na mwisho wa siku atakayeshinda League mwisho wa mwaka na yeye apate dau la pesa nyingi kulingana na Nafasi atakayomaliza nayo.

Kwa kuwa kila game itakuwa na Price Tag/Kifuta Jasho kikubwa nina uhakika kutakuwa na Ushindani Mkubwa

c.c Jamal Malinzi; Pazi; Mbu; Katavi; Belinda Jacob; Nzi; EMT; na wadau wote wa Soka

Ili kufanikisha ligi yetu inabidi Simba na Yanga wasipewe vipaumbele katika ligi ama matokeo kwani kwao kufungwa na timu za mikoani wanaona ni kasoro. Au la ni kuua tu Simba na Yanga kwani hazina manufaa yeyote hapa Tanzania. Vingine vyote nakubaliana nawe.
 
Je uzalendo na wabongo kutoangalia au kwenda uwanjani kuangalia Timu zao haichangii kuporomoka kwa soka

Watu wanapenda timu zao na kuzisapoti kwa nguvu zote, lakini ubabaishaji wa viongozi ndo unasababisha haya
 
Ili kufanikisha ligi yetu inabidi Simba na Yanga wasipewe vipaumbele katika ligi ama matokeo kwani kwao kufungwa na timu za mikoani wanaona ni kasoro. Au la ni kuua tu Simba na Yanga kwani hazina manufaa yeyote hapa Tanzania. Vingine vyote nakubaliana nawe.

Kuamua kuziua Simba na yanga ni vigumu sababu zina wanachama na washabiki Tanzania nzima.., ndio maana nikasema inabidi zife natural death; na kuhamasisha timu za kila mkoa zitafanya watu wawe wazalendo wa Timu zao za Mikoa na kupunguza ule usimba na uyanga.., Au tuamue kabisa tuanzishe ligi za mikoa na ingawa kwa kuanzia hata hizi timu za sasa ziwemo kwenye hii league (Kama mambo yakienda vizuri hizi Timu zitashuka daraja labda tutabaki na Timu nzuri na Zenye nguvu za mikoa)
 
Ni kweli kabisa na hapa nakubaliana na wewe kwa asilimia 100. Kwanza ukiangalia tu mpira wenyewe wa Simba na yanga yaani hauna hata mvuto na ndiyo maana hata makocha wa nje wakija na kuziona hizi timu wanazikandia kwa mpira walionao. Kingine nilicho gundua ni kwamba watanzania wengi huwa hawajuwi mpira kihivyo, utakuta mtu anashabikia eti Mrisho Ngassa kukimbia uwanjani bila mpira, yaani mtu/Ngassa kakosa wazo/mbinu za kumtoka beki watu wanashangalia na utawasikia dah Ngassa bwana ana mikiki uwanjani? Kocha akiona ubovu wake na kumtoa mashabaiki wanaandamana, for what jiulize. Hizi timu bwana ni za kijinga na zinatawaliwa kwa mfumo wa kijinga. Wewe jiulize, wale wazee sijuwi kina Akilimali na kunuka mdomo kote kule anaisaidia nini Yanga? Na bado yupo tu kupiga kelele wakati hana mchango wowote klabuni zaidi ya kuleta migogoro. Kampuni ya bia ikitoa misaada yote inakwenda Simba na Yanga....kama kweli wanataka kuendeleza mpira wa Tanzania kwanini wasigawe hayo mabasi kwa timu zote za Premier League? Toa mgao sawa uone kama Simba na Yanga watashinda ubingwa bara. Tanzania vipaji vipo vingi tu huko mikoani ila mfumo wetu wa kis.enge pamoja na kukosa viongozi makini wa kuendeleza soka letu ndiyo unaoua mpira wa kibongo na kufanya ukose msisimko.
 
Kunahitajika ushindani wa kweli baina ya timu. Kukiwa na ushindani, ligi itavutia watizamaji. Watizamaji wakivutika, wadhamini watavutika. Wadhamini wakivutika, timu na wachezaji zitapata motisha. Motisha ukipatikana, ushindani halali utaongezeka hata nje ya uwanja. Ushindani halali nje ya uwanja ndio utazaa miundombinu zaidi ya kimpira (viwanja stahiki, akademia za kweli, TV za vilabu na ligi yenyewe, n.k.). Hayo yakitokea,ushindani utaongezeka sambamba na vinavyotokana nao, ad infinitum (hadi milele). Lakini ili hayo yatokee,kunahitajika kutofungamana miongoni mwa wadau wote wa timu (isipokuwa washabiki). Ligi yetu inakosa ushindani kwa sababu wachezaji, waamuzi, wadhamini,viongozi, walimu, madaktari, wanahabari na wadau wengine wote wanafungamana na upande (timu) fulani, hivyo kulazimsha msimamo wa mwisho wa Ligi usio halisi. Tungeweza kuajiri CEO wa Ligi yenyewe kutoka nje ya nchi na kwa hivyo asifungamane na timu yoyote. Lakini hao wadau wengine je? Vinginevyo, matatizo ya sekta ya soka ya hapa kwetu si tofauti sana na (na huenda yakawa ni afadhali zaidi ya) Ligi nyingi nyengine (Nigeria, Ghana, Gabon, Mali, B.Farso, Croatia,USA, n.k.). Ila wao, matatizo yao yanageuka kuwa changamoto kwa sababu wadau hukusanya nguvu zao kunyanyua kiwango cha soka kwa ujumla wake, sio kubeba timu mojamoja kwa maslahi binafsi ya wadau binafsi wenye ubinafsi.

Umeongea kitu cha maana ndugu
 
tatizo ya watu wa bongo hatusemagili ukweli. na ukweli ni huu ILI MPIRA WA BONGO UPIGE HATUA TUNAHITAJI EDUCATED COACHES BECAUSE.THESE ARE.THE PEOPLE THAT WILL PRODUCE QUALITY PLAYERS WHO WILL IN THE END IMPROVE THE LEAGUE.
kwa sasa we selling a poor product because the players that are supposed to produce that product are not well trained.
 
Mkuu suala la kiwango sidhani kama lina ukweli sana.., issue kubwa ni kwamba hakuna USHINDANIndio maana hata league za mashule kipindi kile UMISETA / UMISHIMUTA au League za Mbuzi na za Mitaani hata kama kiwango sio kikubwa ila bado watu wanapenda kuangalia.., ukiona hapa issue ya kupendwa huku ni Ushindani na sio vinginevyo, na ile sense of belonging kwamba hii Timu ni ya kwetu na sio ya Individual fulani.., ndio maana nikasema sioni ni vipi AZAM inaweza ikapendwa kama Simba au Yanga au Mbeya City au Kagera Stars
 
Back
Top Bottom