rosesalva
New Member
- Aug 14, 2022
- 1
- 1
Familia na dini zimekuwa zikiaminika kama taasisi muhimu katika hatua za awali za malezi na makuzi ya watoto wadogo na hata vijana wa rika balehe kwa kuwapa mafunzo na miongozo inyowajenga kiimani, kiakili na kiroho.
Kwa kipindi cha mwaka 2000 hadi kufikia 2024 katika nchi ya Tanzania kumekuwa na ongezeko la makanisa ambayo pia hutumia mitandao ya kijamii kuonyesha mafundisho yao.
Pamoja na ongezeko la makanisa bado kumekuwa na ongezeko la vitendo vya ukosefu wa maadili na vitendo vya ukatili ndani ya Jamii ya Tanzania.
Lakini kama jamii lazima tukubaliane kuwa uwepo wa makanisa haya umekuwa na matokeo hasi na chanya ndani ya familia kama taasisi ya malezi na jamii kwa ujumla.
MATOKEO CHANYA
1. Makanisa yanayotumia teknolojia yameweza kuwa sehemu jumuishi na kutoa huduma za wazi bila ubaguzi kwa mwanajamii yeyote anayepata fursa ya kusikiliza mafundisho yanayotolewa, makanisa mengi ya sasa hayabagui asili ya yule anayeshiriki kusikiliza.
2. Makanisa yameweza kujiimarisha na kuongeza wigo wa kutoa huduma nyingi za kijamii kwa watu wenye uhitaji kama wajane, watoto kutoka kaya maskini na yatima ambao hupewa msaada wa kulipiwa gharama za masomo pamoja na kushiriki kutoa mahitaji kwa watu wanapopata majanga kama vile mafuriko na tetemeko la ardhi.
3. Kwa upande wa familia kama taasisi makanisa yamesaidia kuongeza na umoja katika familia yenye imani moja, maelewano na masikilizano juu ya mambo yahusuyo imani, malezi, makuzi pamoja na kusaidia maendeleo ya watoto kwa kuwapa fursa za kuhudhuria kambi za mafunzo na semina, na huduma za mkoba zinazotolewa na makanisa katika mikoa mbalimbali.
4. Matumizi ya vyombo vya muziki na ala za muziki za kisasa zimeweza kuvutia vijana wengi kujiunga na huduma za kanisa hivyo kupata pia fursa za kujumuika na vijana wengine kujifunza stadi mbalimbali za maisha pamoja na kusimamia maadili yao hii inapunguza idadi ya vijana wanaojiingiza katika vikundi rika vinavyojihusisha na uhalifu na matumizi mabaya ya vipawa vyao na hata pia kuwaingia kipato
5. Makanisa haya pia yamesaidia vijana na wanafamilia kupata huduma za kisaikolojia wanapokuwa na msongo wa mawazo kwa kutoa huduma za ushauri na pengine matibabu.
ATHARI HASI
1. Familia kutokuwa na muitikio wa kujumuika pamoja na wanajamii wengine katika nyumba za ibada badala yake wengi husikiliza na kutazama kupitia mitandao ya kijamii, hii hunyima watoto fursa ya kujifunza umuhimu wa ushiriki wa pamoja katika matukio ya kijamii ikiwemo misiba. Pia kutokufika katika makanisa huweza kuzuia fursa za kujifunza stadi mbalimbali na kujijenga kiimani na hata kiakili kupitia semina na kambi mbalimbali za mafunzo.
2. Kumeshuhudiwa pia baadhi ya vitendo vya ukatili kwa watoto na ukatili wa kijinsia kwa wanawake ukifanywa ndani ya makanisa na viongazi husika kwa kutumia kigezo cha kutoa misaada mbalimbali kwa wahanga, pia kuwepo kwa maudhui yanayoleta mkinzano na tamaduni na imani za watu wengine kurushwa kwa uwazi kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.
3. Kumekuwa na ongezeko la migogoro ya kifamilia hasa pale mzazi mmoja anapoamua kubadili kanisa la awali na kwenda kuabudu katika kanisa lingine ambapo huweza kuwa na uelewa tofauti juu ya tafsiri ya mafundisho yatolewayo na viongozi husika.
4. Migogoro ya kiuchumi hasa kwa familia inapotumia muda mwingi katika shughuli za kanisa na kushindwa kufanya shughuli za kujipatia kipato kuimarisha uchumi wa familia zao. Kutokukukubaliana katika matumizi ya rasilimali za familia pia hutokea hasa pale imani inapomlazimu kutoa misaada zaidi ya uwezo wa familia.
5. Migogoro ya kindoa imekuwa ikiongezeka hasa kwenye jamii za vijijini ambapo kina mama wengi huhamia kwenye makanisa na kuacha majukumu yao kama wake na mama wa familia hii huathiri pia mgawanyo wa majukumu katika familia.
6. Katika migogoro hii hata watoto pia hukosa fursa ya kupata malezi sahihi, kushiriki katika masomo na hata huduma za matibabu, watoto na vijana wenye tatizo la madiliko ya kitabia na wengine hupata msongo wa mawazo.
7. Katika migogoro ya kifamilia pia suala la ukatili wa kisaikolojia limeongezeka hasa kwa wanandoa kukosa muda wa faragha kutimiza mahitaji ya mwenza na kwa upande wa wanaume wamekuwa wakiathirika kuona wake zao ni watiifu zaidi kwa viongozi wa dini kuliko kwao kama baba wa familia.
8. Katika hatua ya mwisho migogoro hii inaposhindwa kutatuliwa athari katika jamii imekuwa kuongezeka kwa talaka na familia zinazolelewa na mzazi mmoja,
NINI KIFANYIKE:
Familia ndiyo taasisi ya awali na muhimu katika makuzi na malezi kwa watoto na jamii ikubali kuwa makanisa hayawezi kuchukua jukumu hili kwa kujifanya kama mbadala wa wazazi au nyumba kwa watu. Hivyo lazima kuzingatia yafuatayo:
• Kanisa likubali kuwa familia itaendelea kuwa taasisi ya kwanza katika kufundisha na kuendeleza mila na tamaduni za jamii husika. Hivyo jukumu la kanisa ni kusaidia familia kutimiza jukumu hili na si kuchukua nafasi ya familia.
• Kanisa liwe na msimamo na kutoa mafundisho sahihi yanayohimiza umoja wa familia, kukemea mmomonyoko wa maadili na kutaka ndoa ziheshimike kwakua ndoa ndiyo msingi wa familia imara, mafundisho yalenge pia kusaidia vijana kutokujiingiza kwenye ushiriki wa vitendo vya ngono na kupelekea mimba kabla ya ndoa.
• Makanisa yaendelee kuhimiza washiriki na familia kuhudhuria makanisani badala ya kutegemea mitandao ya kijamii, hii inadumisha umoja na ushirikiano katika matukio ya kijamii pia ni rahisi kutoa huduma na msaada pale unapohitajika kwan watakuwa na taarifa sahihi za waumini.
• Kuwekeza katika programu za watoto na vijana italeta maendeleo endelevu katika kuwa na jamii yenye misingi na maadili mazuri.
• Familia ziandae na kutenga muda maalumu wa kuendelea kujifunza mafundisho ya imani yao kwa umoja, hii itapunguza migogoro ya kifamilia na idadi ya wenza kuhama makanisa.
• Serikali na vyombo vya usimamizi kwa makanisa kama taasisi ya usimamizi wa makanisa (CCT) kuendelea kusimamia maadili, kutoa miongozo juu ya mafundisho yanayotolewa katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii. Pia kuhakiki maudhui ya kila mafundisho ikiwa na pamoja kuhakikisha viongozi wanaotoa mafunzo hayo wana elimu ya theolojia na maadili yanayokubalika katika jamii.
• Makanisa yawajengee uwezo wa kujiimarisha kiuchumi waumini wake hasa wanawake ambao huhama makanisa kutafuta mafanikio ya haraka kwa kuamini miujiza. Itoe mafunzo yenye kuendana na hali ya maisha ya sasa kwa uwazi ili jamii ijue hakuna mafanikio ya kiuchumi kupitia miujiza.
HITIMISHO:
Kuwa na taasisi bora za malezi ya awali kutaandaa kizazi bora chenye maadili na tabia njema ndani ya jamii yetu ya kitanzania tuitakayo ndani ya miaka 5 hadi 25 ijayo, hivyo ni muhimu kuandaa mazingira na misingi imara kwa watoto na vijana ambao ndiyo baba na mama katika familia zijazo pia wapo watakaokuwa viongozi wa makanisa. Jamii yenye maadili na misingi imara haitatawaliwa na migogoro ya kifamilia pamoja na vitendo vya ukatili kwa watoto na ukatili wa kijinsia hivyo kuwa sehemu salama kwa makuzi na malezi ya watoto.

Upvote
2