babu onyango
JF-Expert Member
- Jan 12, 2023
- 378
- 984
Wakuu salaam,
Imekuwa ni kasumba sasa kwa washabiki/viongozi pamoja na wachambuzi uchwara kuwa timu ya Simba ni bora hapa nchini kwakuwa bado ipo inashiriki ligi ya mabingwa barani Afrika.
Ukweli ni kuwa uwepo wa Simba cafcl ni bahati tu kutokana na njia nyepesi waliyopitia na kufika hapo makundi.
Niwatolee mfano tu timu za Chelsea na Liverpool zipo ligi ya mabingwa barani ulaya hatua ya mtoano ila kwa sasa ni timu mbovu sana na zisipoangalia zinaweza kuteremka daraja msimu huu.
Upande mwingine timu za Arsenal na Man U ambazo zipo Europa league baada ya kutolewa ligi ya mabingwa zikikiwasha vilivyo ambapo timu ya Arsenal unaweza kusema ndio klabu Bora kabisa duniani Kwa sasa kulingana na kabumbu safi linalooneshwa na Hawa washika bunduki wa London.
Ndugu zangu wa Simba mnatakiwa muukubali ukweli huu kuwa ninyi kwa sasa ni timu ya kawaida sana au tunaweza kuwaita timu dhaifu na kuendelea kuwepo kwenu huko cafcl sio kigezo cha ubora na mifano tayari nimeitoa.
Ukweli mchungu ni kuwa mwaka huu pia mnatoka bila kikombe chochote, na hata huko Cafcl msipokuwa makini mnaweza msipate points yoyote huko makundi kwa maana Mna timu iliyochoka sana na kwa usajili huu wa tia maji tia maji mnaoufanya taifa linaenda kupata aibu ya mwaka.