Kuingia makundi CAF Champions League kusiwadanganye kuwa mna timu bora

levo zipi umefika wewe kwani kuna tuzo ya kufika robo au nisu fainali
Maajabu ya mwaka kuna timu iliwahi kujiandalia kombe la 50 unbeaten ila sherehe ikavurugwa na timu choovu kuliko zote bara
 
Wakuu salaam..

Imekuwa ni kasumba sasa kwa washabiki/viongozi pamoja na wachambuzi uchwara kuwa timu ya Simba ni bora hapa nchini kwakuwa bado ipo inashiriki ligi ya mabingwa barani Afrika.

Ukweli ni kuwa uwepo wa Simba cafcl ni bahati tu kutokana na njia nyepesi waliyopitia na kufika hapo makundi.

Niwatolee mfano tu timu za Chelsea na Liverpool zipo ligi ya mabingwa barani ulaya hatua ya mtoano ila kwa sasa ni timu mbovu sana na zisipoangalia zinaweza kuteremka daraja msimu huu.

Upande mwingine timu za Arsenal na Man U ambazo zipo Europa league baada ya kutolewa ligi ya mabingwa zikikiwasha vilivyo ambapo timu ya Arsenal unaweza kusema ndio klabu Bora kabisa duniani Kwa sasa kulingana na kabumbu safi linalooneshwa na Hawa washika bunduki wa London.

Ndugu zangu wa Simba mnatakiwa muukubali ukweli huu kuwa ninyi kwa sasa ni timu ya kawaida sana au tunaweza kuwaita timu dhaifu na kuendelea kuwepo kwenu huko cafcl sio kigezo cha ubora na mifano tayari nimeitoa..

Ukweli mchungu ni kuwa mwaka huu pia mnatoka bila kikombe chochote, na hata huko Cafcl msipokuwa makini mnaweza msipate points yoyote huko makundi kwa maana Mna timu iliyochoka sana na kwa usajili huu wa tia maji tia maji mnaoufanya taifa linaenda kupata aibu ya mwaka..
Tumeanza Leo kuingia makundi? Utopolo bhana!
 
Kila awazalo mpumbavu anataka aandike na kupost humu.
 
Niwatolee mfano tu timu za Chelsea na Liverpool zipo ligi ya mabingwa barani ulaya hatua ya mtoano ila kwa sasa ni timu mbovu sana na zisipoangalia zinaweza kuteremka daraja msimu huu.
Je selection ya timu kushiriki UEFA kwa mfano Uingeleza inafanyikaje? Je Chelsea ama Liverpool kuingia mtoano Ligi ya mabigwa wamesaidiwa tu sababu kwenye ligi hawafanyi vizuri?

Majibu ya haya yatakusaidia.
 
Si lazima uandike Kila uwazalo. Simba hii yenye magoli 37, ni dhaifu kwa timu inayoshinda kwa ujanja ujanja! Unadhani kudroo na csk Moscow ni rahisi? Unadhani kuongoza kundi club bingwa ni sawa na ligi ya bahasha ? Unadhani nafasi ya 11 Africa inapatikana kwa maneno? Hao De Augosto kama ni dhaifu ucheze nao kama utatoboa.mtadhulumu sana Simba kwenye ligi hii,lakini kwenye marefa wenye weledi,hamtoboi.Jaribu kuheshimu walioheshimisha ligi, hiyo nafasi ya ligi kuwa namba 12 kwa ubora point nyingi ni za simba.
 
Ukweli upi zaidi ya wivu.

Miaka yote Simba iliyofanya vizuri kimataifa iwe klabu bingwa au shirikisho mliibeza sana kwenye media zenu mlizozihonga ili wakate tamaa na ilitoboa,mwishoni aibu mliona nyie.

Hamna jipya,toboeni shirikisho mfikie level zetu ndio muanze kujifananisha na sisi walimu wenu wa mpira wa wakubwa.

Huko hakuna marefa dizaini ya Kina Kayoko mliozowea kuwahonga ili mpate unbeaten za mchongo,huko ni show show tu.

Karibuni kwenye show za wakubwa tuwafunde.
Unasemaje?
 
Kwa hiyo ninyi kuingia hatua ya makundi ya mashindano ya kombe la waliofeli ndio inamaana mna timu bora? Ninyi mna uhakika mtarudi na kombe kwenye hayo mashindano? Tuanzie hapo kwanza!
Haya tuone sasa nyie kwenye hayo mashindano ya waliofeli 😂😂😂
 
Back
Top Bottom