Mkuu, usituchoke😀
Vipi nikifanya hivi, natengeneza site moja ya kiingereza ambayo naiombea Adsence, then natengeneza nyingine ya kiswahili ikiwa na mwonekano na content zile zile ila kwa lugha ya kiswahili. Then nafanya kuiunga kwenye ile ya kiingereza kwa kuweka ka button kenye link ya hiyo web ya kiswahili. Lengo ni maarifa yasiwapite pia waswahili wenzangu.
Je, bots wa google wanataamua vipi katika hiyo scenario.?
Kuchoka hamna, mkuu. Point ya kuanzisha thread ilikua kushare maarifa kwenye topic husika.Ko maswali yakiwepo, uliza 😁
Nimekupata. Kuliko kucomplicate mambo kuna kitu inaitwa,
subdomain. Ukinunua domain, let's say
www.kainetics.com na ukaipea hosting, nadhani unayo ruksa ya kuitegenezea subdomain 20 kwa plan ndogo kabisa au unlimited kwa business plan.
Cha kufanya, domain yako ya msingi, bdo inakua site ya kingereza, yaani site kuu. Na inakuwa kwa Kingereza. Then unaweza tengeneza subdomain maalumu kwa ajili ya content za kiswahili, zipo option mbili, either iwe
SUFFIX au
PREFIX.
Mfano;
Kifupisho cha lugha ya Kiswahili, huwa SW. Hivyo unaenda unda
prefixed subdomain ya
sw.kainetics.com ukacopy design nzima ya kainetics.com lakini badala ya kuweka content za Kingereza, ukaweka za Kiswahili. Google hawatokuwa na muda nayo.
Option B ni ya kutumia
Suffixed subdomain. Mfano ukitembelea
bbc.com, utakutana na site ya kingereza. Ila ukitembelea
bbc.com/swahili utakutana na content zile zile ila kwa Kiswahili. Unaweza fanya vivyo hivyo kwako pia, as long as files za hizo sites mbili ziko kwa directory tofauti.
Hivyo,
kainetics.com inaweza kuwa na aidha
sw.kainetics.com au
tz.kainetics.com au subdomain yoyote ile. AU
kainetics.com/sw au
kainetics.com/tz au
kainetics.com/swahili zote ni sawa as long as
directory zake zijitegemee. Then hutokuwa na shida na Adsense au Adsterra au InfoLinks 🙂