Kuiona Yanga vs TP Mazembe bure, njooni kwa wingi

Kuiona Yanga vs TP Mazembe bure, njooni kwa wingi

Wakubali pia kama kikitokea kitu chochote uwanjani kibaya au maafa ambayo hatuombei au hata vitu kuharibiwa uwanjani basi wawajibike pia maana kuachia uwanja bure ina maana hakuna control kila mtu ana haki ya kuingia si bure ila hatari ni kubwa kuliko wanavyofikiria.
Nadhani kutakuwa Na control maana sio Mara ya kwanza manji kufanya hivyo
 
Swala la kulinda mashabiki ni jukumu la serikali hasa ukizingatia ni mechi inayotambulika kimataifa,mlitaka Yanga wafanyeje labda?Waweke walinzi wao?
 
Mbona Stars alivyochukua Chalenji tulikuwa tunaingia bure Taifa.

Nijiavyo kuna kiwango cha mashabiki kikifika wanazuia kuingia uwanjani. Hapo kazi kwako kuwahi.
 
HaHaHaaaaaa. TFF na rafiki yao AZAM walishapanga kurusha mpira laivu bila kuishirikisha Yanga. Sasa yanga nae kamwaga mboga. Ngoma inogile
Uzuri Yanga wanagombana na Yanga wenzao waliopo TFF. Hata hivyo bado mechi itaonyeshwa LIVE Azam TV, sina haja ya kwenda kuumizana Taifa
 
Sema hata kama ni bure watu hawawezi kuwa wengi kiasi hicho naamini tahadhari itachukuliwa kubwa.
 
Milango inafunguliwa SAA ngapi maana nilishapanga hata kiingilio kiwe vipi (najua kisingezidi laki)hii game lazima niione


Milango itafunguliwa saa kumi na moja alfajiri. Wahi na maandazi ya kunywea chai asubuhi.
 
HaHaHaaaaaa. TFF na rafiki yao AZAM walishapanga kurusha mpira laivu bila kuishirikisha Yanga. Sasa yanga nae kamwaga mboga. Ngoma inogile
Ungekuwa unajua wala usingeandika upuuzi huo,hizo ni hasira za mkizi,kwani mechi kurushwa live kuko palepale na gharama zote za mchezo lazima yanga azilipe kuna uwanja asilimia 15,zitoke mfukoni kwa manji kuna ulinzi,sasa hizo ni akili au matope!?unajiita wa kimataifa wakati una mawazo ya kimchangani!!kanuni hamsomi mnafuata anavyosema yule vuvuzela wenu!!akiwalisha tango poli mnameza tu!!hakuna kanuni ya caf inayosema eti muishirikishe timu husika kwenye maamuzi ya nani aonyeshe mechi husika.mlizoea kuwapeleka tff,sio caf.
 
KAZI tadani taidani

Wapendwa watanzania uongozi wa Yanga kwa moyo mmoja umekaa nakuona tunaitaji watanzania wengi kuona mechi zetu

Hivyo basi mechi ya yanga na TP Mazembe tumeondoa viingilio kila mtu ataingia buure na atakaekuuliza tkt piga mayowe vijana watakuja kuwasaidia

Timu ni ya watanzania wote wapo waliotamani kuiona Yanga lakini kwa sababu fulani wangeshindwa sasa tunawakaribisha wooote

Imetolewa na msemaji mkuu Yanga

Jerry C Muro
Huyu aliisha tangaza viingilio au alikuwa hajaamrishwa na bosi wake? Mbona imetamkwa baada ya kuona wameshindwa kusitisha urushaji wa mechi hiyo hai (live)? Wao wangewapa AMRI TANESCO kuzima umeme Dar yote ifikapo saa tisa alasiri mpaka saa moja tu ingetosha.
 
Wakubali pia kama kikitokea kitu chochote uwanjani kibaya au maafa ambayo hatuombei au hata vitu kuharibiwa uwanjani basi wawajibike pia maana kuachia uwanja bure ina maana hakuna control kila mtu ana haki ya kuingia si bure ila hatari ni kubwa kuliko wanavyofikiria.
Huo uwanja ni wa Serikali hivo pana gharama zinazitumika katika mechi sasa hapo atalipa nani?
 
Back
Top Bottom