Kuishi kwingi kuona mengi: Soma kisa nilichokiona Kawe

Nakumbuka miaka kama kumi na kidogo hivi mjini Arusha, alikuja nabii mmoja mwanamke ambaye alikuja kufungua kanisa jipya na kumuweka wakfu mchungaji mpya wa kanisa hilo.

Nilichoshangaa ni pale mchungaji mpya alipodondoka alipokuwa anawekwa
a wakfu kwa kuombewa na nabii huyo mwanamke.
Nilishangaa sana, sasa kama yule ambaye anakuwa mchungaji anaanguka ikimaanisha ana mapepo sisi wengine itakuwaje??

Imani yetu tuiweke kwa Mungu Baba, Mwana na Roho mtakatifu, na sio kwa watu.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 

Nilichokiona kwa Mwamposa watu wengi wapo na misongo ya mawazo tu, madeni, na wale ambao Koo zao zina mambo ya kishirikina.
Wengine matatizo ya kisaikolojia tu yanawasumbua.
Asante kwa utafiti shirikishi! Nadhani upo sahihi, ulipata relief yoyote?
 
Nishawai kwenda kanisani tukapangwa foleni ya kupakwa mafuta[emoji3][emoji3][emoji3]...ikawa mchungAji anakupaka mafuta kuchwani alafu akaongea maneno yake...Mimi nikawanashangaa Watu wanaanguka TU...mmoja baada ya mwingine.

Kuna Watu nyuma yetu na wamama wamebeba khanga...

Kila mtu akawa anaanguka ..ilivyofika zamu Yangu nami nikaapiga kelele...alafu nikaajiangusha chini[emoji3][emoji3][emoji3]....

Wengine wanajinyonganyonga Kama nyoka nguo zinawavuka wamama wanakuja kuwafunika...

Kwakweli Sijawai kujua Sababu ya Watu kuanguka...Mimi nilifuata mkumbo.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Mgf
Umenichekesha sana umeunga tella
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Mgf
Umenichekesha sana umeunga tella
Mgf nlifuata mkumbo tu...nikatoka nimechafuka nguo zote zimejaa vumbi na mafuta ya mzaituni[emoji23][emoji23]..

Alinipeleka mtoto wa mamdogo nlikua namatatizo mengi..Basi akaniambia twende huko Calvary Assembles of God.

Niliyoyashuhudia huko..nlirudi kwenye Imani Yangu Nasijawai Rudi tena.
 
Katika watu 10 β€˜wanaoangukaga’ makanisani, 80% ni wanawawake.
Nikweli..wanaume wamesimama nyuma ya wanawake eti wanawadaka na kuwabeba wakianguka..

Kuna Muda wa maombi Huyu Ndugu Yangu alikua TU anaapiga kelele anaanguka ...wanakuja vijana wanambeba wanampleka mbele ya kanisa..

Sijajua kwa undani sababu ya kuanguka..Rashid Gwajima anaweza kuwa na jibu.
 
umenikumbusha mchizi wangu mmoja aliwahi nambia alienda kuombewa wote wana dondoka yeye kakaza tu. yule bwana anamsukuma kwa nguvu yeye kakausha tu

alipozidi sukumwa akaona yaishe tu akaanguka na yeye.

wanamaombi watakuja na ufafanuzi.
Hhhhhhhhh
 

[emoji1787][emoji1787][emoji1787]hiyo zamu ya kupokeana wakidondoka wana ushirikiano sana[emoji23]
 

Umenikumbusha kitu. Ilikuwa mwaka 2014, akaja mtumishi wa Mungu mgeni Kanisani kwetu kwa ajili ya huduma ya Ibada ya jioni. Aliposimama madhabahuni, sikusikia anatoa hata sala, na wala hakusoma hata fungu moja kutoka kwenye maandiko matakatifu kipindi chote alichokuwa amesimama madhabahuni, mwanzo mwisho wa Ibada. Zaidi ni kuwa mtumishi huyu alisimulia kisa cha harakati za utumishi wake halafu kikaniacha midomo wazi.

Mtumishi alisema kuwa kuna kipindi alikuwa anaenda kutoa huduma ya neno la Mungu kwenye haya makabila ya wawindaji yanayoishi porini, ila bahati mbaya watu hao walikuwa hawaitaki na hawaipendi kabisa huduma hiyo.

Kwa hiyo huyu mtumishi alikuwa akifika huko, wawindaji hao wanaamua kuanza kumpiga hadi inafikia hatua wale wanaompiga, wanazimia kwa kukosa nguvu, wanachoka kutokana na namna walivyokuwa wananmpiga mtumishi huyo.

Hata hivyo hali hiyo bado haikumsababisha mtumishi huyo, kuacha kwenda kufanya huduma hiyo kwa watu hao kwa sababu yeye ni mwinjilisti. Sasa mimi nikajiuliza kwamba wale wanaokupiga wanazimia, halafu wewe bvado upo mzima, na kesho tena unakwenda huko, ukiwa unajua kabisa kuwa unaenda kupigwa, wakati wahitaji wa huduma kama hiyo na ambao hawawezi kukupiga wamejaa kila mahali? Hiki kitu kiliwahi kunishangaz sana.

Halafu ukimwangalia yule ambaye alikuwa antaoa kisa hiki, unaona kabisa kwa nje kuwa huyu mtu hawezi kudanganya, wakati alichokuwa anakisema kinapingana kabisa na uhalisia.

Anyway, hata Yoshua na Kalebu walikuta majitu ya miraba minne kule Yeriko, lakini miraba hiyo haikuakisi uhalisia wake mbele za nguvu za Mungu.

Pengine mtumishi huyu anaweza kuwa alikuwa anasema ukweli, ila inahitaji watu waliobobea kiroho kwa kiwango cha juu sana kuweza kuumeza ukweli huu, assming kwamba kweli ulikuwa ni ukweli
 

[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji23]aisee
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚dah pole sna
 
Nina dada yangu humwambii kitu kuhusu Mwamposa, kila akija kunitembelea lazima aje na mafuta kwenye kichupa huwa akinipa nachukua akiondoka natupa, nahisi amegundua, jana nilipita nyumbani kwake kumsalimia akanivizia akanipaka kichwani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…