Mwaka 2011 nilimtembelea ndug yangu maeneo ya Block T, Mbeya. Yeye na familia yake wanasali AGAPE, ni walokole kwelikweli na mkuu wa kaya ni mzee wa kanisa.
Viongozi wengi wakubwa AGAPE hupenda kutembelea kaya ile kwa maombi, mafundisho, maongezi na chakula. Hadi Mr. Fenandez na mkewe, Annie nao huwatembelea kila wafikapo Mbeya.
Wakati nimefika nilikuta wiki ya maombi ya kazi, na msaidizi wa Askofu Fenandez alikuwa Mbeya akiongoza maombi hayo ya wiki. Kulikuwa kile kinaitwa kufunguliwa, ambao hawajampokea Bwana walimpokea, wengi makumi kwa makumi, isipokuwa mimi. Jambo lile halikuwafurahisha wenyeji wangu, walitaka niokoke pia.
Maombi yakawa maombi, kila siku usiku wanatembelea kaya ile na kufanya maombi, kama kawaida waombewaji hudondoka. Wao wakifanya maombi, mim huwa chumbani nikiperuzi FB na Twitter. Ndugu walinishawishi sana, nikaona acha nifanye watakayo kwakuwa nipo kwao, nikiondoka kurudi home, naendelea na kanisa langu.
Kabla ya maombi, ilianza Sara ya toba, nikifuatisha maneno ya yule msaidizi ya Fenandez. Baada ya hapo alinishika kichwani kuniombea. Kwa kweli sikusikia nguvu yoyote ya ajabu, ulikuwa mkono tu, jambo lililofanya niendelee kusimama wima tela mwenye utulivu huku nimefumba macho.
Nahisi alipoona sitetereki, nikaona anaanza kunifinya maeneo ya misuli ya macho, yakaanza maumivu ya kichwa, nikavumilia... Alipoona nimetulia, akaweka mkono wa pili na kuzidi kuomba huku akiniminya zaidi, maumivu yalizidi, nikapata akili kuwa anataka nidondoke, basi taratiiiiiiibu nikaanza kushuka chini. Bro alipoona nanyong'onyea, akaja nyuma yangu na kunidaka, kisha nikalazwa chini na kila mtu akaanza kukemea pepo chafu la kiburi litoke ndani yangu.
Baada ya kuamka, mchungaji akasema pepo aliyekuwa ndani yangu hakuwa wa kawaida, kama angekuwa mchungaji dhaifu, asingetoka hakika.
Nilicheka kimoyomoyo, siku ikaisha