Kuishi kwingi kuona mengi: Soma kisa nilichokiona Kawe

Nishawai kwenda kanisani tukapangwa foleni ya kupakwa mafuta[emoji3][emoji3][emoji3]...ikawa mchungAji anakupaka mafuta kuchwani alafu akaongea maneno yake...Mimi nikawanashangaa Watu wanaanguka TU...mmoja baada ya mwingine.

Kuna Watu nyuma yetu na wamama wamebeba khanga...

Kila mtu akawa anaanguka ..ilivyofika zamu Yangu nami nikaapiga kelele...alafu nikaajiangusha chini[emoji3][emoji3][emoji3]....

Wengine wanajinyonganyonga Kama nyoka nguo zinawavuka wamama wanakuja kuwafunika...

Kwakweli Sijawai kujua Sababu ya Watu kuanguka...Mimi nilifuata mkumbo.
hahahahaaha hizi comment zitaniua ...
 
Picha linaanza napokea simu kwa ndugu zangu upande wa mama watoto wangu wanasema, samahani tunakuja kwenye maombezi kwa Mwamposa wewe kama mwenyeji tunaomba utupokee ili utupeleke kwa Mwamposa tukaombewe.

Nikasema ok poa nitawapeleka nyie njooni. Ijumaa wakaingia ndani ya jiji la Dsm nikawapokea, Jumamosi chapu nikawapeleka Kawe kuombewa, mimi nikaamusha kwenye mishe zangu za hapa jijini.

Kesho yake jumapili waakambiwa warudi tena kweli jumapili tena nikawarudisha kwenye ibada kama kawida nikasema ibada ikiisha mtanishitua nije kuwachukua.

Mida ya saa nane ibada ikaiisha wakanishitua nikawachukuwe nilipofika kwa Mwamposa mmoja wao akasema kuwa kuna mfanyakazi mwenzake walishawahi kufanya naye kazi miaka ya nyuma kwenye kampuni kampigia simu waonane maeneo ya PICOLO HOTEL kuna maombezi pia.

Basi bwana tukaenda pale Picolo hotel kufika pale wakatupandisha juu kuna ukumbi kule wanasali.

Nilichokikuta kule kinashangaza sana kwa kuwa ilibidi niwasubiri basi nikasema hebu ngoja nikae nisikilizie hapahapo ukumbini.

Kanisa lina waumini 13 tu, wanawake 10 na wanaume 3. Maombi yakaanza nguvu ya upako sijui nini inawashukia wakawa wanadondoka waumini wote hadi ndugu zangu nao wanadondoka.

Nikajisemea moyoni mbona haya majanga. Ikawa kama mchezo sasa wanaombewa watano waliobaki wanasimama nyuma yao kuwashikilia ili wasijibamize sakafuni. Wakizinduka wengine tena wanaombewa halafu waliodondoka wanaamka tena kuwashikilia wenzao.

Nikachoka kuangalia movie ya kitoto nikawambia oya nyie si mnadondoka humu hebu niwaache mkipona mtanishitua nije niwachukue twende nyumbani. Nimeshangaa hivi kipi kinamfanya mtu anadondoka hovyo wakati wa maombezi au ni michezo ya kuigiza?​
Usiumize kichwa. Hizo zote ni vurugu zinazosababishwa na fumbo la uhai na kifo. Yaani tumetoka wapi na tukifa inakuwaje?
Chamsingi wewe piga maisha. Kula bata. Kwasababu mpaka sasa Hakuna majibu ya Hilo fumbo. Kila mmoja anakuja na mbwe mbwe zake.😄😄
 
Kwenye maombi pale hamna tofauti na walevi wanaolewa kumaliza matatizo yaliyokichwani pombe ikiisha msoto uko palepale.
Mtu ameshindwa kurejesha Mkopo anaenda kwenye maombi unategemeea benki imsamehe kivipi sasa?​

Awaja sema usamehewe mkopo,ila unafanyiwa maimbi ili upate baraka za lizki uweze kulipa mkopo,Mimi ni muumini wa Arise and Shine,kwanza mafundisho ni mazuri,ukienda uende na imani sio kwenda kumchunguza mtu,hata huko mnako abudu kama auna imani ni sawa na bure.

Na mara nyingi nyuzi za namna hii mtoa post anatoa kishabiki sana pasipo jua kipi ana kisemea.

Dunia kubwa hii yaki kukuta ndo unajua ujui.

Asanteni.
 
Pale PICOLO HOTEL hadi camera man walianguka sema wanabadilishana tu na wanarecord kwa kutumia smartphone maana kanisa bado changa.
Halafu mchungaji anakomalia hii mbona hamrecord njooni mpige picha nyie vipi.​
😛😛😛 Aise duuu eti hii mbona hamrecord njooni mpige picha nyie vipi.
 
Umenikumbusha kitu. Ilikuwa mwaka 2014, akaja mtumishi wa Mungu mgeni Kanisani kwetu kwa ajili ya huduma ya Ibada ya jioni. Aliposimama madhabahuni, sikusikia anatoa hata sala, na wala hakusoma hata fungu moja kutoka kwenye maandiko matakatifu kipindi chote alichokuwa amesimama madhabahuni, mwanzo mwisho wa Ibada. Zaidi ni kuwa mtumishi huyu alisimulia kisa cha harakati za utumishi wake halafu kikaniacha midomo wazi.
Mtumishi alisema kuwa kuna kipindi alikuwa anaenda kutoa huduma ya neno la Mungu kwenye haya makabila ya wawindaji yanayoishi porini, ila bahati mbaya watu hao walikuwa hawaitaki na hawaipendi kabisa huduma hiyo. Kwa hiyo huyu mtumishi alikuwa akifika huko, wawindaji hao wanaamua kuanza kumpiga hadi inafikia hatua wale wanaompiga, wanazimia kwa kukosa nguvu, wanachoka kutokana na namna walivyokuwa wananmpiga mtumishi huyo. Hata hivyo hali hiyo bado haikumsababisha mtumishi huyo, kuacha kwenda kufanya huduma hiyo kwa watu hao kwa sababu yeye ni mwinjilisti. Sasa mimi nikajiuliza kwamba wale wanaokupiga wanazimia, halafu wewe bvado upo mzima, na kesho tena unakwenda huko, ukiwa unajua kabisa kuwa unaenda kupigwa, wakati wahitaji wa huduma kama hiyo na ambao hawawezi kukupiga wamejaa kila mahali? Hiki kitu kiliwahi kunishangaz sana. Halafu ukimwangalia yule ambaye alikuwa antaoa kisa hiki, unaona kabisa kwa nje kuwa huyu mtu hawezi kudanganya, wakati alichokuwa anakisema kinapingana kabisa na uhalisia.
Anyway, hata Yoshua na Kalebu walikuta majitu ya miraba minne kule Yeriko, lakini miraba hiyo haikuakisi uhalisia wake mbele za nguvu za Mungu. Pengine mtumishi huyu anaweza kuwa alikuwa anasema ukweli, ila inahitaji watu waliobobea kiroho kwa kiwango cha juu sana kuweza kuumeza ukweli huu, assming kwamba kweli ulikuwa ni ukweli
Aah nimecheka sana[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Huu ulimwengu hatujauumba sisi tumezaliwa tumeukuta. Kama unatambua uwepo wa uchawi naamini utaamini kuna Mungu. Wewe jiulize tu maswali rahisi tu kwanini hakuna siti namba 13 kwenye Ndege, Wewe jiuliza tu unaambiwa mtu kafa hivi nini kinaondoka mwilini maana kila kitu ukikagua vipo mwilini lakini hapumui. Jiulize vijiswali vyepesi tu inakuaje Mtu anatoa kafara familia yake kisha anakuwa Tajiri,Hivi nini kinamkuta mtu tunayeambiwa anayo Mapepo unakuta Mtu anapiga kelele anapiga ukuta vichwa, anazama kwenye maji masaa mpaka mawili akiwa Hana mtungi wa gesi pamoja na yote akiombewa na Sheikh au Mchungaji anapona na anaendelea na Shughuli zake, Jiulize nini dhumuni la wewe kuwepo duniani, Natakua kujua kwanini haujiulizi Dunia imetengenezwa na nani na ni Fundi wa aina gani.Jichunguze mwenyewe kisha jiulize tu kwanini Daktari wa Macho kwanini hawezi kutibu moyo halafu jiulize ni nani anaweza kutibu vyote. Umewahi kufikiri kwanini Madaktari nguli lakini bado wanakwenda Ibadan. Umewahi kuona watu wanapasua Nazi njia panda? Au kuchinja Mbuzi njia panda, Leo fikiria kwa upana zaidi Hivi walioandika vitabu vitKatifu walikuwa na upeo gani wa kufikiri?. Jiulize vijiswali vidogo hivyo kisha njoo utujibu..
 
Kuna jamaa yangu alinibembeleza Sana niende kanisani kwao kwenye maombi nikaenda, muda wa maombi watu wanaangukia tu asee nikashangaa...mchungaji akanifata na kuanza kuniombea lakini sikuanguka...ghafla nikapigwa kibao kwenye kisogo nikayumba nikafumbua macho na kugeuka nakutanisha macho na mchungaji, nilichukia Sana nikaondoka...tangu siku hiyo siwezi na sijawaji Tena kwenye makanisa ya aina hiyo.
 
😂 😂 😂 😂 😂
Wachungaji hao waxenge sana, wanachapa hadi vibao!
 
Picha linaanza napokea simu kwa ndugu zangu upande wa mama watoto wangu wanasema, samahani tunakuja kwenye maombezi kwa Mwamposa wewe kama mwenyeji tunaomba utupokee ili utupeleke kwa Mwamposa tukaombewe.

Nikasema ok poa nitawapeleka nyie njooni. Ijumaa wakaingia ndani ya jiji la Dsm nikawapokea, Jumamosi chapu nikawapeleka Kawe kuombewa, mimi nikaamusha kwenye mishe zangu za hapa jijini.

Kesho yake jumapili waakambiwa warudi tena kweli jumapili tena nikawarudisha kwenye ibada kama kawida nikasema ibada ikiisha mtanishitua nije kuwachukua.

Mida ya saa nane ibada ikaiisha wakanishitua nikawachukuwe nilipofika kwa Mwamposa mmoja wao akasema kuwa kuna mfanyakazi mwenzake walishawahi kufanya naye kazi miaka ya nyuma kwenye kampuni kampigia simu waonane maeneo ya PICOLO HOTEL kuna maombezi pia.

Basi bwana tukaenda pale Picolo hotel kufika pale wakatupandisha juu kuna ukumbi kule wanasali.

Nilichokikuta kule kinashangaza sana kwa kuwa ilibidi niwasubiri basi nikasema hebu ngoja nikae nisikilizie hapahapo ukumbini.

Kanisa lina waumini 13 tu, wanawake 10 na wanaume 3. Maombi yakaanza nguvu ya upako sijui nini inawashukia wakawa wanadondoka waumini wote hadi ndugu zangu nao wanadondoka.

Nikajisemea moyoni mbona haya majanga. Ikawa kama mchezo sasa wanaombewa watano waliobaki wanasimama nyuma yao kuwashikilia ili wasijibamize sakafuni. Wakizinduka wengine tena wanaombewa halafu waliodondoka wanaamka tena kuwashikilia wenzao.

Nikachoka kuangalia movie ya kitoto nikawambia oya nyie si mnadondoka humu hebu niwaache mkipona mtanishitua nije niwachukue twende nyumbani. Nimeshangaa hivi kipi kinamfanya mtu anadondoka hovyo wakati wa maombezi au ni michezo ya kuigiza?​
Yulia uombewe
 
Huu ndio upuuzi wa dini,wanafikiri wataweza kutatua changamoto za dunia kwa maombi,
Ajira,maendeleo ya sayansi na tekinolojia,kilimo,viwanda,Elimu,IT,innovation ,hivi vitu haviji kwa kukesha kanisani,
Kama maombi tu ndio yanakuza nchi,onesheni wachina wamesali wapi wakaunda kampuni giant Kama Huawei,tekinolojia ya 5G,6G,miradi yote mikubwa ya flyovers Afrika inajengwa na mchina,wahandisi wa kwetu wamelala,
Mwsfrika,hana ajira,chakula,maradhi yanamsumbua,anaenda kuombewa kanisani.
 
Pia mimi nilikuwa naombewa hivyox2 niache bangi miaka ya nyuma nikawa nakomaa kudondoka wakati wengine wanaoombewa wanadondoka. Mchungaji akanisogelea na kuninong'onezea Dogo Aisee chalii yangu jidondoshe basi mbona unazingua mbele ya kadamnas? Bado nikawa nimekomaa tu na kumuambia Mchungaji aniwekee laki mfukoni kwanza kisiri. Bas nikamuona kaenda kunong'onezana na wale wanawashikilia wanaodondoka wasijibamize halafu nakuendelea kumpigia Mungu kelele na sauti za ajabux2 baadaye wale wanaosaidia wanaojidondosha wawili wakanisogelea kwa nyuma. Mchungaji akanifuata na kuanza kubwabwaja kwa sauti za ajabu nikashtukizia nachomwa vipini kama sindano makalioni nilipiga ukunga wa hatarii nikasikia mchungaji akipaza sauti toka kwa jina yesu nikawa bado nakomaa kudondoka nikachomwa tena kipini cha hatarii na mtama kima cha nyoka na wale wanaowashikilia wanaodondoka wasijibamize ikabidi tu niende chini
Hii sidhani kivile
 
Back
Top Bottom