Kuishi kwingi kuona mengi: Soma kisa nilichokiona Kawe

Kuishi kwingi kuona mengi: Soma kisa nilichokiona Kawe

Nimesoma comments za juu zote kumbe makanisani kuna vioja vikubwa sana
Ndio maana kuna rafiki zangu wakiristo ukiwambia waende kanisani wanakataa sijui kiliwakuta nini kutoka kwa wachungaji
 
Niliombewa na bibi yangu mzaa mama' alitumia jina la Yesu kukemea ugonjwa huo.. bibi yangu ni nurse ila nilikataa dawa zake kwani hazikunisaidia na hali ilikua mbaya' nilimwambia nipeleke kwa mchungaji.. nadhani hii imani ndiyo iliniponya

Nb.sisali kanisa lolote!
Kwa hiyo, Je, unaamini kwamba Yesu Kristo ni mponyaji?
 
Mombi bila kuanguka huko ni kukosa uzalenfo wa kiroho.

Haya amaigizo ya imani sijui wapi mwisho wake
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]duh I see nimecheka sana eti bila ya kuanguka huko ni kukosa uzalendo wa kiroho[emoji851][emoji851][emoji851][emoji851][emoji851][emoji851][emoji851][emoji851][emoji851][emoji851][emoji851][emoji851]
 
Kwenye maombi pale hamna tofauti na walevi wanaolewa kumaliza matatizo yaliyokichwani pombe ikiisha msoto uko palepale.
Mtu ameshindwa kurejesha Mkopo anaenda kwenye maombi unategemeea benki imsamehe kivipi sasa?​
Hili wazo finyu sana. Fikiria zaidi ya hapo. Ukijibu naweza kukufungukia kidogo utapata kitu.
 
Umenikumbusha kitu. Ilikuwa mwaka 2014, akaja mtumishi wa Mungu mgeni Kanisani kwetu kwa ajili ya huduma ya Ibada ya jioni. Aliposimama madhabahuni, sikusikia anatoa hata sala, na wala hakusoma hata fungu moja kutoka kwenye maandiko matakatifu kipindi chote alichokuwa amesimama madhabahuni, mwanzo mwisho wa Ibada. Zaidi ni kuwa mtumishi huyu alisimulia kisa cha harakati za utumishi wake halafu kikaniacha midomo wazi.

Mtumishi alisema kuwa kuna kipindi alikuwa anaenda kutoa huduma ya neno la Mungu kwenye haya makabila ya wawindaji yanayoishi porini, ila bahati mbaya watu hao walikuwa hawaitaki na hawaipendi kabisa huduma hiyo.

Kwa hiyo huyu mtumishi alikuwa akifika huko, wawindaji hao wanaamua kuanza kumpiga hadi inafikia hatua wale wanaompiga, wanazimia kwa kukosa nguvu, wanachoka kutokana na namna walivyokuwa wananmpiga mtumishi huyo.

Hata hivyo hali hiyo bado haikumsababisha mtumishi huyo, kuacha kwenda kufanya huduma hiyo kwa watu hao kwa sababu yeye ni mwinjilisti. Sasa mimi nikajiuliza kwamba wale wanaokupiga wanazimia, halafu wewe bvado upo mzima, na kesho tena unakwenda huko, ukiwa unajua kabisa kuwa unaenda kupigwa, wakati wahitaji wa huduma kama hiyo na ambao hawawezi kukupiga wamejaa kila mahali? Hiki kitu kiliwahi kunishangaz sana.

Halafu ukimwangalia yule ambaye alikuwa antaoa kisa hiki, unaona kabisa kwa nje kuwa huyu mtu hawezi kudanganya, wakati alichokuwa anakisema kinapingana kabisa na uhalisia.

Anyway, hata Yoshua na Kalebu walikuta majitu ya miraba minne kule Yeriko, lakini miraba hiyo haikuakisi uhalisia wake mbele za nguvu za Mungu.

Pengine mtumishi huyu anaweza kuwa alikuwa anasema ukweli, ila inahitaji watu waliobobea kiroho kwa kiwango cha juu sana kuweza kuumeza ukweli huu, assming kwamba kweli ulikuwa ni ukweli
Au itakuwa hukumwelewa? But miujiza ipo sana
 
Pia mimi nilikuwa naombewa hivyox2 niache bangi miaka ya nyuma nikawa nakomaa kudondoka wakati wengine wanaoombewa wanadondoka. Mchungaji akanisogelea na kuninong'onezea Dogo Aisee chalii yangu jidondoshe basi mbona unazingua mbele ya kadamnas? Bado nikawa nimekomaa tu na kumuambia Mchungaji aniwekee laki mfukoni kwanza kisiri. Bas nikamuona kaenda kunong'onezana na wale wanawashikilia wanaodondoka wasijibamize halafu nakuendelea kumpigia Mungu kelele na sauti za ajabux2 baadaye wale wanaosaidia wanaojidondosha wawili wakanisogelea kwa nyuma. Mchungaji akanifuata na kuanza kubwabwaja kwa sauti za ajabu nikashtukizia nachomwa vipini kama sindano makalioni nilipiga ukunga wa hatarii nikasikia mchungaji akipaza sauti toka kwa jina yesu nikawa bado nakomaa kudondoka nikachomwa tena kipini cha hatarii na mtama kima cha nyoka na wale wanaowashikilia wanaodondoka wasijibamize ikabidi tu niende chini
Itakuwa bange uliotumia wakati unaandika siyo ya nchi hii
 
Niliombewa na bibi yangu mzaa mama' alitumia jina la yesu kukemea ugonjwa huo.. bibi yangu ni nurse ila nilikataa dawa zake kwani hazikunisaidia na hali ilikua mbaya' nilimwambia nipeleke kwa mchungaji.. nadhani hii imani ndiyo iliniponya

hiyo imenifanya ni amini ukiwa na IMANI hakuna haja ya wachungaji

Nb.sisali kanisa lolote!
Enda kanisani jaman
 
Ha haaaaa uminikumbusha vibao vya kustukiza vya kisogoni E.A.G.T city center kwa pastor Katunzi....vinavurugaaa ila sikudondoka
😂😂😂😂 Hawa wachungaji ni Hatari😂
 
Huu ulimwengu hatujauumba sisi tumezaliwa tumeukuta. Kama unatambua uwepo wa uchawi naamini utaamini kuna Mungu. Wewe jiulize tu maswali rahisi tu kwanini hakuna siti namba 13 kwenye Ndege, Wewe jiuliza tu unaambiwa mtu kafa hivi nini kinaondoka mwilini maana kila kitu ukikagua vipo mwilini lakini hapumui. Jiulize vijiswali vyepesi tu inakuaje Mtu anatoa kafara familia yake kisha anakuwa Tajiri,Hivi nini kinamkuta mtu tunayeambiwa anayo Mapepo unakuta Mtu anapiga kelele anapiga ukuta vichwa, anazama kwenye maji masaa mpaka mawili akiwa Hana mtungi wa gesi pamoja na yote akiombewa na Sheikh au Mchungaji anapona na anaendelea na Shughuli zake, Jiulize nini dhumuni la wewe kuwepo duniani, Natakua kujua kwanini haujiulizi Dunia imetengenezwa na nani na ni Fundi wa aina gani.Jichunguze mwenyewe kisha jiulize tu kwanini Daktari wa Macho kwanini hawezi kutibu moyo halafu jiulize ni nani anaweza kutibu vyote. Umewahi kufikiri kwanini Madaktari nguli lakini bado wanakwenda Ibadan. Umewahi kuona watu wanapasua Nazi njia panda? Au kuchinja Mbuzi njia panda, Leo fikiria kwa upana zaidi Hivi walioandika vitabu vitKatifu walikuwa na upeo gani wa kufikiri?. Jiulize vijiswali vidogo hivyo kisha njoo utujibu..
Akijibu maswali haya au akiyaelewa anaokoka peponi
 
Nishawai kwenda kanisani tukapangwa foleni ya kupakwa mafuta[emoji3][emoji3][emoji3]...ikawa mchungAji anakupaka mafuta kuchwani alafu akaongea maneno yake...Mimi nikawanashangaa Watu wanaanguka TU...mmoja baada ya mwingine.

Kuna Watu nyuma yetu na wamama wamebeba khanga...

Kila mtu akawa anaanguka ..ilivyofika zamu Yangu nami nikaapiga kelele...alafu nikaajiangusha chini[emoji3][emoji3][emoji3]....

Wengine wanajinyonganyonga Kama nyoka nguo zinawavuka wamama wanakuja kuwafunika...

Kwakweli Sijawai kujua Sababu ya Watu kuanguka...Mimi nilifuata mkumbo.
Hebu toa sababu , ulienda kufanya nn?
 
Huu ndio upuuzi wa dini,wanafikiri wataweza kutatua changamoto za dunia kwa maombi,
Ajira,maendeleo ya sayansi na tekinolojia,kilimo,viwanda,Elimu,IT,innovation ,hivi vitu haviji kwa kukesha kanisani,
Kama maombi tu ndio yanakuza nchi,onesheni wachina wamesali wapi wakaunda kampuni giant Kama Huawei,tekinolojia ya 5G,6G,miradi yote mikubwa ya flyovers Afrika inajengwa na mchina,wahandisi wa kwetu wamelala,
Mwsfrika,hana ajira,chakula,maradhi yanamsumbua,anaenda kuombewa kanisani.
Hao akili ujue Maulana kawapa ndiyo maana wanafanya wandaz. Hata sisi Waafrika & Watanzania tuna akili na viwanda vyetu.
 
Back
Top Bottom