"Kuishi na Corona" kunavyopotoshwa Tanzania

"Kuishi na Corona" kunavyopotoshwa Tanzania

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Mabibi na mabwana moja kwa moja kwenye mada. Itifaki yote imezingatiwa.

Shirika la afya Ulimwenguni (WHO), limekuwa likitoa tathmini, mapendekezo na kauli mbalimbali likionya na kushauri kwenye jitihada za kukabiliana na ugonjwa huu hatari.

Kwa bahati mbaya sana hapa nchini kwetu kumekuwa na upotoshwaji wa wazi kwenye baadhi ya jitihada hizo za WHO.

Ushauri wao usipokubaliana na misimamo ya viongozi wetu, utasikia, "wanatumiwa na mabeberu hao". Ushauri ukiangukia tulipo, tunaukumbatia kwa chereko chereko, hata kama ni nje kabisa ya uhalisia (out of context).

Mifano ni mingi ila kwenye uzi huu, itoshe kuangazia kauli yao hii muhimu ya 'kwenye kuishi na Corona.'

Kwa tathmini za wazi na kwa jinsi maambukizi ya ugonjwa huu yalivyo, WHO walisema:

"ugonjwa huu si wa kuondoka leo au kesho." Kwamba, "itabidi tu kujifunza namna ya kuendelea kuishi nao hadi pale tiba au chanjo kamili itakapopatikana".

Kauli hii imekuwa ikinukuliwa hapa nchini nje ya uhalisia (out of context), kuwa WHO wamepata funzo toka kwa rais wetu mpendwa na kuwa eti sasa sisi tuko kwenye mstari wa mbele tayari kuishi na Corona.

Haiyumkiniki hata hizi chereko chereko na mayowe ya ushindi dhidi ya Corona chini ya bwana yule hapo jumapili ni kwa minajili hiyo.

Kauli ya WHO ni kauli sahihi ya kisayansi na iliyokamilika. Kauli ile haitokei hewani bali ina vigezo kamili vilivyo zingatiwa. Kiuhalisia nchi (yenye Corona) haianzi kuishi tu na Corona from nowhere. Kuna pa kuanzia (starting point) kabla ya kufikia kwenye hatua ya kuishi na ugonjwa huu hatari Ila katika hali ya usalama. Hii ikiwa, wakati hatua zingine zikisubiriwa.

Nchi zote tunazozisikia kuwa zinalegeza masharti yao ya udhibiti zilizo kuwa zimejiwekea, huko kulegeza hayo masharti, ndiyo katika kujipanga kuingia sasa salama kwenye awamu hii ya pili ya kuendelea na maisha kwa tahadhari wakati ugonjwa huu ukingalipo. Angalizo la msingi, "lakini ugonjwa ukiwa umedhibitiwa vilivyo kwanza."

Rwanda, Uganda, USA, UK, Australia, New Zealand, Namibia, Italy, Spain nk, ni mfano wa nchi zilizoko kwenye hatua hizo. Kenya wanapambana vilivyo ili nao angalau waweze kufika kwenye hatua hiyo.

Unaweza ishi na mnyama hatari aliyeko kwenye cage au mhalifu hatari aliyeko jela si anayezurura huru mitaani.

Brazil, Tanzania, Sudan kusini, Burundi, Congo nk, tungali na makundi ya simba, chui, fisi, mbwa mwitu, nk yakizurura mitaani mwetu.

Eti kuwa tunataka sasa kujiaminisha na kuwaachia watoto wetu wadogo kabisa wa chekechea wajiendee tu shule peke yao kwamba wanyama hao watawazoea tu muda unavyopita! Mbona itakuwa ni kujidanganya kwa wazi kuliko pitiliza mno?

Brazil na sisi kwa hali ya sasa kimsingi tofauti haiwezi kuwapo. Kiuhalisia maambukizi yangali bado yanaongezeka sana. Tunatofautiana kwa viwango tu na hilo kwa mwendo wetu huu ni suala la muda tu.

Angalia hapa hawa (Brazil). Wanaanza vipi kuishi na Corona katika hali hii waliyomo sasa?




Kilicho wafikisha hapo ni kama hiki hiki cha kwetu - kibri kilicho pitiliza cha kiongozi wao mkuu.
 
Nilisikia mapambio kwenye kituo kimoja cha television wakidai mataifa sasa yameanza kuiga na kufata mbinu za Mh fulani,

Wakaenda mbele zaidi na kuwahoji wakazi wa mataifa mengine eti wanatoa pongezi sana kwa mbinu hizo na utafiti.

Nikajiuliza kulikuwa kuna umuhimu wowote wa hizi propaganda? Na zinafanywa kwa malengo gani?
 
Kwendeni huko mmeanza kusema tusubiri, sijui Corona itatunyoosha karibia miezi mitatu na bado tunadunda.

Mtasubiri sana.

WHO ndio wamekuwa wapuuzi kabisa siku hizi. Walisema Corona haienezwi kati ya mtu na mtu. Wakasema Barakoa wavae wagonjwa tu.

Baadae wanakuja tena kukanusha. Kila habari mbaya wanaitabiria Africa wakati wazungu ndio wanakufa kama kuku wa mdondo.

WHO wapite hivi ndio maana Trump anawazingua.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilisikia mapambio kwenye kituo kimoja cha television wakidai mataifa sasa yameanza kuiga na kufata mbinu za Mh fulani, Wakaenda mbele zaidi na kuwahoji wakazi wa mataifa mengine eti wanatoa pongezi sana kwa mbinu hizo na utafiti. Nikajiuliza kulikuwa kuna umuhimu wowote wa hizi propaganda? Na zinafanywa kwa malengo gani?

Ujinga ni mzigo wa kutosha kabisa kumkabidhi mnyamwezi akahangaika nao.
 
We mleta maada na wengine kama wewe, kwa taarifa yenu JPM ana trend sana ulimwenguni sema hawaweki mtandaoni wengi. Kwa kifupi amejenga jina mataifa mbalimbali kwa jinsi alivyolikabiri hili suala.

Endeleeni kutuombea mabaya mtaaibika tu mwisho wa siku

God save us
 
Wewe na Ndugu zako wote mtasubiri sanaa. Na kwa taarifa yako jumapili tunapiga shangwee. Wewe kama unaona huwezi kaaa nyumbani. #lockdown your self

Sent using Jamii Forums mobile app

Nasikia wote waliokimbia Dar akiwapo yule nambari moja wameitishwa kurejea mara moja kwa sababu hawawezi kukimbia kifo.

Vipi mkuu, unajua anawasili lini ili tukampokee kamanda wetu mpendwa?
 
Na uwaambie kama wao ni WHO sisi TZ ndiyo US hatuyumbishwi.


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
unasema WHO wako perfect, wakati Mdhamini wake mkuu anataka kujitoa.
Embu jifikirie tena

Sent using Jamii Forums mobile app

Lini anakuwa mdhamini mkuu na lini anakuwa beberu?

Lini kauli au pendekezo la WHO ni sawa na lini wanatumiwa na mabeberu?

Mstari unaujua ulipo? Au mambo ni kibongo bongo tu kupima uelekeo wa upepo kwanza?
 
Sasa si ujilockdown ww na familia yako bro kwani kuna mtu kakukataza

Sent using Jamii Forums mobile app

Mkuu ndiyo maana niliandika mwanzo kabisa kuhusu "itifaki kuzingatiwa".

Bandiko hili lilizingatia uwepo wako pia mkuu.

Ila hadi pale utakapoivua miwani ya mbao uliyoivaa, ni wazi kuwa kuona vizuri itakuwa taabu kidogo.
 
Next Sunday tumeambiwa tuka paree na kuogelea ili kuiaga corona

Sent using Jamii Forums mobile app
Ningependa kuwaambia kisa flani cha kwenye bible hao Jamaa wanaojiandaa kwenda ku-party hio J2 kusherekea 'kumalizika' kwa Corona:

Baada gharika kuisha Nuhu akaona amtume Njiwa nje ya Safina ili kuona vipi hali ikoje huko nje,maji yameisha au lah ili aone kama anaweza kutoka nje ya safina au la.

Sasa wajiulize kwa mazingira tuliyonayo Njiwa anaweza kua nani?
 
Ningependa kuwaambia kisa flani cha kwenye bible hao Jamaa wanaojiandaa kwenda ku-party hio J2 kusherekea 'kumalizika' kwa Corona:

Baada gharika kuisha Nuhu akaona amtume Njiwa nje ya Safina ili kuona vipi hali ikoje huko nje,maji yameisha au lah ili aone kama anaweza kutoka nje ya safina au la.

Sasa wajiulize kwa mazingira tuliyonayo Njiwa anaweza kua nani?

Mkuu usitake ncheke miye ...!
 
Ningependa kuwaambia kisa flani cha kwenye bible hao Jamaa wanaojiandaa kwenda ku-party hio J2 kusherekea 'kumalizika' kwa Corona:

Baada gharika kuisha Nuhu akaona amtume Njiwa nje ya Safina ili kuona vipi hali ikoje huko nje,maji yameisha au lah ili aone kama anaweza kutoka nje ya safina au la.

Sasa wajiulize kwa mazingira tuliyonayo Njiwa anaweza kua nani?
Kwahiyo mkuu, wehau ungi mkono hii send off party ya Corona..??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom