"Kuishi na Corona" kunavyopotoshwa Tanzania

"Kuishi na Corona" kunavyopotoshwa Tanzania

Na uwaambie kama wao ni WHO sisi TZ ndiyo US hatuyumbishwi.


Sent from my iPhone using JamiiForums

Mkuu miye nitawaambia kama nani?

Unadhani hadi WHO kutuambia kuwa zile mashine za vipimo hazina issue yoyote au hata kututaka kutoa takwimu zetu za ugonjwa tulizokomaa nazo tokea Apr 29, hawa viongozi wetu wapendwa hawajawafikishia tu huo ujumbe wako mkuu?

Tafadhali check nao basi, kama bado hawajafanya kazi hiyo utuletee mrejesho ili nasi sasa tuseme na bwana Tedros Ghebreyesus kama ulivyotaka.
 
Hata mheshimiwa ni mwanasayansi kama hao wa WHO

Mkuu ipo tofauti ya mwanasayansi na mwanasayansi jina.

Huyu wa nyungu, maombezi na mitishamba kwenye janga kama hili? Mbona unataka kutomtendea haki kiasi hicho mchana wote huu?
 
Vile naisubiri hiyo jumapili kuona watu wakishangweka.
 
We mleta maada na wengine kama wewe, kwa taarifa yenu JPM ana trend sana ulimwenguni sema hawaweki mtandaoni wengi. Kwa kifupi amejenga jina mataifa mbalimbali kwa jinsi alivyolikabiri hili suala.

Endeleeni kutuombea mabaya mtaaibika tu mwisho wa siku

God save us

Nani anapinga kuwa ha trend sana? Lakini je ana trend kwenye yapi?

Kwamba "hawaweki mtandaoni wengi", au labda kama hata maana ya ku trend nayo hujui?

Kwamba kajenga jina? Does it concern you, ni jina la namna gani alilojenga au hata kama ni kwa kutu sokomezea akhera tukiwa bado hai?

Mkuu hayupo mwenye kutuombea mabaya. Wasiwasi wako tu. Mabaya tunajipalilia wenyewe kwa mikono yetu.

Hatuna mchawi kwenye hili zaidi ya kuwa mchawi ni uchaguzi wetu wenyewe.
 
Waafrika wengi sana mna upumbavu wa kujidharau na kutukuza vya mzungu mshenzi, katika gonjwa hili JPM ni mshindi na gumzo duniani japo wanaficha,.

Lakini mnatokea wa kudharau na kumuona mzungu kua ni kila kitu,kinachoendelea wala hakionekani mitaani wala kwa ndugu zetu wala kwa majirani,marafiki huko mikoani kote.

Tatizo lipo lakini linadunda kwa ngozi nyeusi,watu hawa sisi hutembea na Maralia, Typhod, Kichocho, Madonda ya tumbo na tunaanza kutibu kimoja kimoja huku tukiendelea na shughuli zetu ije iwe hii mafua?

Nyie vibaraka mnakuja na ngonjera chungu mzima wapuuzi wakubwa nyie..RAIS wetu ni zaidi ya kina Tyson na Mohamed Alli iwapo angekua ulingoni

JAH Rastafari Morning Africa.Trust JAH respect nature
 
Kwendeni huko mmeanza kusema tusubiri, sijui Corona itatunyoosha karibia miezi mitatu na bado tunadunda...

Mkuu huu ugonjwa ni mgeni na haukuwahi kuwapo. Kwamba WHO amekuwa wakirekebisha taarifa zake ili ziwe sahihi zaidi kwa manufaa yetu na wewe unawalaumu kwa hilo, mbona hayo ndiyo yatakuwa yale maajabu yenyewe ya Mussa sasa?

Mkuu hakuna asiyependa kuona tukidunda. Maonyo, mausia, miito ya hadhari nk ni katika kututakia kuendelea kudunda kwa muda mwingi zaidi sana ya miezi mitatu tu unayoongelea.

Wanasema wahenga: "asiyesikia la mkuu huvunjika guu".

Mpaka guu livunjike tu mkuu? Au yale yale ya mtoto mkaidi kutofaidi hadi siku ya Iddi?
 
Machizi yanaongezeka nikuulize machache.

Kuna ndugu au jilani ako kafa kwa covid
Hao wanaochukua hatua wangapi wanakufa kwa siku. Kama unaona tunapingana why usiende uko ambako hawapingani.

Wapuuzi kama ww mnao ombea taifa matatizo ni wa kuwapiga risasi
Mods futeni huu ujinga.
 
Machizi yanaongezeka nikuulize machache.

Kuna ndugu au jilani ako kafa kwa covid
Hao wanaochukua hatua wangapi wanakufa kwa siku..

Mkuu mwanzoni mwa bandiko 'kuzingatiwa kwa itifaki' kulikuwa na maana ya kuwavumilia watu kama wewe:

"msiojua mlitendalo, msiojuwa mkisemacho, msiojitambua, msiojielewa, mnaojidhania kuwa mmesimama, mnaojidhania kuwa mna hati miliki za uzalendo, mnaojidhania kuwa na hati miliki za utanzania nk, ati hata kiasi cha kuwaamrisha mods kufuta nyuzi."

Kwa ufupi mkuu wewe ni wa kuhurumia wala si wa kutukanwa tu bali kupuuzwa kabisa:

IMG_20200517_112354_371.jpg


Disgrace!
 
Kwenye iyo tafrija tutashangilia pamoja na makonda au atabaki na familia yake amejifungia ndani, na magufuli apewe taarifa uku mjini Corona imeisha arudi Daslamu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom