Kuishi na majirani yataka moyo

Fundi manyumba

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2018
Posts
3,799
Reaction score
8,063
Wakuu ni mwezi sasa tangu nijiunge na chama cha wapangaji. Sasa naona kasheshe ya kukaa nyumba moja na wanafunzi plas mdada ambaye pesa yake kutoa mpaka bwana wake amzingatie.

Watu wanakera sana sana sana. Ishu imekua changamoto hapa ni umeme yaani umeme unaisha kama kuna mpangaji anakunywa.

Na biashara yangu hapa inategemea umeme hivo kuna mda ukikatika wenyewe wanajikausha kimya wakitegemea mimi lazima nitalipa tu.

Wakuu naombeni ushauri hapa au maoni hiki tatizo naepuka vipi. Maana mama mwenye nyumba nae ana mambo mengi mno.

Nyumba inakula umeme kama kiwanda cha misumali aiseee. Nilijua baada ya kupata biashara hii ya kupata chochote kitu nitakua nishamaliza kumbe kuna huu ujinga ujinga wa wapangaji kuwa na visirani na watu.

Na hiki kisirani ndo kinafanya vijana tuwe tunawaka hawa wadada ambao wameolewa ila wanashindwa kutimiziwa haki ya msingi. Sometimes genye zinaweza kuleta taflani.

Nawasilisha. Juu hapo nimeomba ushauri kutokana na hii ishu ya umeme watu kushindwa kulipa wanategemea mimi wa biashara nitalipa. Natatua vipi?
 
Omba LUKU yako TANESCO.
 
Umesema shida kubwa ni luku kuisha kama mb za Vodacom au Kuna shido nyingine?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…