Kuishi na mke kunataka uvumilivu wa chuma

Kuishi na mke kunataka uvumilivu wa chuma

Ndoa kazi!no likizo,no salary,no day off, full time employment! Halafu promotion sahau kabisa .Sasa shida ni pale mchumba unapompatia fesibuku utaimba kikwenu.Ukimwambia pika tule hajui,fagia!hawezi, fua basi anakuuliza kwani mie dobi?
 
Nianze kwa kusema mimi ni kijana wa miaka 35 sasa, nimeoa mwaka wa 6 huu, na nina watoto wawili, ila ujumbe wangu wa leo vijana mnapoamua kuoa muwe mmemaanisha hawa wake zetu unahitaji akili ya ziada kuishi nao wengi wana upeo wa chini sana na wasahaulifu kupitiliza.

Hivyo kijana usipokuwa muelewa unaweza kuwa unagombana nao kwa sababu ambazo unaweza kuziepuka.

NB: Binafsi katika miaka hiyo ya ndoa nimejifunza na kushuhudia mengi upo wakati nilitaka kuachana na mke wangu kwa kelele zake na kutofuata ninachotaka mimi. Ila baadae nikaamua kumpotezea nimeamua kuwa kimya kama mjinga flani hivi ila akili kumkichwa.

UPDATE: 22 Novemba 2016
Wake zetu tunawapenda sana ila mnaongea mno kupitiliza. Binafsi situmii kilevi, wala si mtu outgoing kivile isipokuwa mara chache nikiwa na pesa kidogo tunatafuta outing na familia ufukweni au nje ya mji Bagamoyo ama Lushoto au Arusha. Lakini sasa huyu mke wangu yeye hataki nifanye kazi na mwanamke yeyote, duuh! Hili kwangu haliwezekani maana kwa kazi yangu nakutana na wengi (wanaume & wanawake).

Pia usafi chumbani ni ovyo ovyo si usafi wa kitanda wala nguo za ndani, nimezungumza mpaka nimechoka, kuna wakati fulani dada wa kazi eti alikuwa anafanya usafi chumbani kwetu, bila kuingilia kati huenda angepewa na cchuup afue.

Nimeamua kuwa mhanga nafua nguo za ndani ninazozikuta kwenye tenga (zikiwemo zake) na kufanya usafi chumbani.
**Ila akili kichwani asee hapa nimechamba nimeibuka na nnyaa
mkuu una kibamia nini??? kama ulivyo na akili kichwani vivyo ivyo na wanawake nao nazani wana akili kichwani.... mwanamke mwingine mpaka akufanyie ivyo hujui nae ulimfanyaje my be anakutafutia njia ya wewe uchepuke ili uwe chanzo
 
Ndio maana wazungu wamejihalalishia ndoa za jinsia moja nadhani na wao walianza kuona kuoa jinsi tofauti ni stress na huku kwetu ndipo tunakoelekea maana wanaume wanalalamika sana
 
Wanawake (hasa wakristo) baada ya kuolewa wanajisahau, maana dini hairuhusu Talaka, ndoa ni mpaka kifo kiwatenganishe hapo ndo tatizo linapoanza.
 
Matatizo mengi kwenye ndoa tunajitakia wenyewe. Hasa pale panapotokea tatizotunalala nalo kabla hatujawekana sawa. Kitendo chakutokuwekana sawa nafsi zinaumia na nafsi iliyoumia inataka kulipa kisasi. Na iwapo hilo jambo litaongezewa lingine ndivyo nafsi inavyozidi kujeruhika na kujenga ukungu wa majeraha na kuzidi kulipa kisasi. Ukitaka kujua chunguza siku uliyoumizwa na mwenzako na hamjatengeneza. Muda mwingi ndani mwako kunakaa vikao fulani na agenda kubwa ni hizi. Kwani kanionaje? Yeye hanijui! Anafikiri sina akili sio? Hajawahi kuona watu vichaa, aulize aambiwe nk. Hatima yake ni hii nikulipa kisasi ili umie km wewe ulivyoumizwa. Na iwapo lengo litafanikiwa mtaongeza matatizo na hamtaona umuhimu wa mwenzake. Pia walimu wetu wanachangia sana kuharibu mahusiano ya watu. We fikiri kwanini una tabia yakusikiliza rafiki wa nje kuliko mkeo au mumeo? Kutokana na hiyo tabia ndoa zinapitia wakati mgumu. Mara mia muwe mnaelezana pale panapotokea kutoelewana kuliko kukaa na uchungu au kutokuongea an mwenzako. Kutokuongea na mwenzako kunazalisha sumu mbaya kuliko unavyofikiri. Hasa kwa mwanaume, wanaumia sana iwapo mke atamchunia, fikiri unalala kitanda kimoja mwenzako kUkoboa siku mbili tatu hadi mwezi, hamuongei, na mwenzako anatamani muongee. Hii ni mbaya kuliko. Utamu wa ndoa ni mawasiliano tu asikudanganye mtu yeyote. Mm binafsi nina ndoa naumiaga sana tena sana. Ukiona mwanaume anarudi nyumbani saa sita hiyo inachangia sana. Niombe wanandoa jitahidini kujitambua na kumuweka Mungu mbele. Jinsi unavyosema wamama ni shida si kweli ni kwamba pande zote kuna baadhi wenye shida. Na nyie wa mama msijisahau kuwa ninyi ni wanawake na mnapaswa kuwa wanyenyekevu kwa waume zenu na kuwaheshimu bil hofu. Na ninyi wanaume tuwapende hao wake zetu na tusiwafanye km vyombo vya starehe. Nb. Wamama chondechonde msije mkafikiri kuwanyima waume zenu tendo la ndoa ni kuwaadhibu. Mnajidanganya hapo ni kujiadhibu mwenyewe. Wanaume hiyo ndiyo sumu yetu, hakuna cha limbwata hapo. Toa vizuri na kwa moyo uone utamu wa hiyo ndoa
 
Vijana msifikir ndoa ni kucheza kwaito na kutuma picha instagram. Kwa wale waliooa kabila lililopo pembezoni mwa mlima mrefu Afrika na kule Kyela moto tunauona!
Huku ndipo walipo wanawake ambo uptstairs kumechangamka na wenye kuona mbele na utatakiwa uwe flexible kupokea ushauri kutoka kwao kwa sababu huwa na malengo makubwa ya kufanikiwa. Mwanaume asiyependa kushauriwa ndiye atawaona threat tu. Mimi nimeoa pembezoni mwa mlima na ninaona tukipiga hatua kwa speed kubwa kimaendeleo. Kuwa transparent na kukaribisha mijadala ktk kupanga mambo na kuepuka kilevi na uzinzi kutawafikisha mbali kimaendeleo. Tatizo hawapendi maisha ya kona kona wala kudanganywa.
 
Back
Top Bottom