Kuishi na mke kunataka uvumilivu wa chuma

Kuishi na mke kunataka uvumilivu wa chuma

Wanawake tunaooa sasa hivi ni watoto wa Wazazi wa kidigitali. Hakuna malezi wala makuzi ya kuheshimu na kutii ndani ya ndoa. Ukienda kuchumbia mapokezi ya Kiwango cha Lami, kumbe wanajua umekuja kuwaondolea aibu ya mtoto wao kukwama ndani..... Utakapooa sasa ndo utajiuliza hivi huyu alitokea mlangoni au dirishani.???

Na nyie wanawake Muwe na akili ya kutofautisha ndoa na harusi. Na Mjue kuwa harusi ni ya siku moja ndoa ni kitu cha maisha. Mnavyojiandaa kwenye harusi mngekuwa mnajiandaa hivyo kwenye ndoa mambo yangekuwa murua kabisaa.... Ila kinyume chake ndoa zimekuwa kiwanda cha kutengeneza wajane tu. Maana wanaume wanajifia hovyohovyo. Pumbavu kabisa.
Hili tatizo la malezi ni la pande zote, sio kwa wanawake tu. Ni kweli wazazi aina ya maisha wanayoishi na malezi wanayowalea watoto wao yanainfluence aina za ndoa watoto wao watakazokuwa nazo.

Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo, ndio maana kuna umuhimu wa kujuana vyema kabla ya kukimbilia hizo harusi, ndoa hazina shida wenye shida ni sisi wake kwa waume.

Haki sawa nalo janga lingine, ndani ya nyumba hajulikani mke nani mume nani, kwa malezi na tamaduni zetu waafrika, mke huwa chini ya mume, na ili ndoa iwe na amani hilo lazima lizingatiwe. Ila sio mwanaume ndio utake advantage ya kumnyanyasa mkeo,mpendane,mheshimiane na kuchukuliana ila kubwa zaidi kuwa karibu na Mungu, inasaidia sana na mtajenga familia imara na bora.
 
Aisee najuta. Lakini si unajua WAGALATIA tulivyo wanafiki TALAKA anatoa Rais wa Vatikane. Mm nimeamua kufanya yangu.
Hahaha aisee bob nakuelewa sana....mimi nakumbuka kuna wakati kaka/cousin yangu (mtoto wa mama yangu mkubwa)....kuna kipindi like 5 years ago aliumwa sana inasemekana ni kipapai (kazini huko gov't walimfanya habari sizo, inasemekana na mkewe ali play part kumzunguka jamaa atake over everything)

Baada ya wajomba kuhangaika nae sehem sehem chimbo huko akapona. Unaambiwa kipindi anaumwa hajiwezi ni mama yake mzazi (mama mkubwa) ndio alikua ana muogesha na kumhudumua mwanae, huyo mkewe alikua hafanyi chochote kile....yeye anakuja analeta vitu anaondoka. Hapo ndipo nilipokuja amini aisee kuna wanawake sio kabisa.

Sisi ni wachagga pure ila aisee kuna baadhi ya wachagga hawafai kabisa hasa wa machame na rombo (sio sana kama machame) sina maana ya ku generalise na si wote najua ila hzo sehem mbili hata mama yangu alinionya sana nisiende kuoa pande hzo. Nitajuta !!!
 
Kumbe wachaga hata nyie kwa nyie mnatengana!!! Basi sawa.
 
Mwanaume au mumeo si mtu sahihi wa kwenda nae ligi hata siku moja mtazamo wangu hata Kama kakufanyia ubaya we tafuta njia tu ya kutafuta amani ya moyo wako ila sio eti kafanya hivi na mimi nafanya vile utaumia ww.

Just take care of yourself maradufu tu oga hata Mara kumi fundisha watoto wako kuna ving vya kufanya Kama mwanamke zaidi ya kuleta ligi na mwanaume
 
Aisee kuna haja ya kuwa na semina elekezi kwa vijana wa kiume kabla ya kuoa. Ipo tofauti kubwa kati ya kuoa/kuwa baba Vs Kupiga mitti (NJE-NJE-NDANI)
 
wakati mwingine nyie wanaume msikimbilie kulaumu matokeo ya mbegu mbaya uliyoipanad, ukaipalilia, na kuimwagilia maji mwenyew
mfano mtu kipnd cha uchumba ulimlea kama yai akikutembelea hata usafi hafanyi chakula unaenda kununua chips bloira hiv unategemea ndan ya ndoa awe wife material?
wewe kama ulioa maonyesho endelea kutunza hicho kivutio chako cha utalii
 
Ukiwaona wanandoa wanaadhimisha miaka kadhaa ya ndoa. Wape SHIKAMOO wamepitia mengi.
 
we mwenyewe una matatizo siri za chumbani na mkeo hazifai kuziweka nje kama hivi tabia zingine tunawafundisha wake zetu naye akifanya hivi utakuja kulialia
 
Hv mtu umuoe kama Sepenga, Wolpa au Babbra si kujitafutia ugonjwa wa moyo aisee.
 
Back
Top Bottom