Kuishi na mke kunataka uvumilivu wa chuma

Kuishi na mke kunataka uvumilivu wa chuma

Nianze kwa kusema mimi ni kijana wa miaka 35 sasa, nimeoa mwaka wa 6 huu, na nina watoto wawili, ila ujumbe wangu wa leo vijana mnapoamua kuoa muwe mmemaanisha hawa wake zetu unahitaji akili ya ziada kuishi nao wengi wana upeo wa chini sana na wasahaulifu kupitiliza.

Hivyo kijana usipokuwa muelewa unaweza kuwa unagombana nao kwa sababu ambazo unaweza kuziepuka.

NB: Binafsi katika miaka hiyo ya ndoa nimejifunza na kushuhudia mengi upo wakati nilitaka kuachana na mke wangu kwa kelele zake na kutofuata ninachotaka mimi. Ila baadae nikaamua kumpotezea nimeamua kuwa kimya kama mjinga flani hivi ila akili kumkichwa.

UPDATE: 22 Novemba 2016
Wake zetu tunawapenda sana ila mnaongea mno kupitiliza. Binafsi situmii kilevi, wala si mtu outgoing kivile isipokuwa mara chache nikiwa na pesa kidogo tunatafuta outing na familia ufukweni au nje ya mji Bagamoyo ama Lushoto au Arusha. Lakini sasa huyu mke wangu yeye hataki nifanye kazi na mwanamke yeyote, duuh! Hili kwangu haliwezekani maana kwa kazi yangu nakutana na wengi (wanaume & wanawake).

Pia usafi chumbani ni ovyo ovyo si usafi wa kitanda wala nguo za ndani, nimezungumza mpaka nimechoka, kuna wakati fulani dada wa kazi eti alikuwa anafanya usafi chumbani kwetu, bila kuingilia kati huenda angepewa na cchuup afue.

Nimeamua kuwa mhanga nafua nguo za ndani ninazozikuta kwenye tenga (zikiwemo zake) na kufanya usafi chumbani.
**Ila akili kichwani asee hapa nimechamba nimeibuka na nnyaa
Rekebisha hapo kwenye heading mkuu sio Chuma badala yake weka Almasi.
 
1481291698474.jpg
Majibu hayo hapo..

Ongeza mke wa pili, atashika adabu..
 
Mimi nadhani kuishi pamoja kama mume na mke ndo kunahitaji uvumilivu.

Wote mvumiliane na sio uvumilivu uwe wa upande mmoja tu.

Kumwona mwenzio ndiye mwenye mapungufu na wewe kujiona uko timilifu nayo ni mapungufu.
Well said..!! Tatizo la wanaume mnajiona very sent wakat in real sense mnamadhaifu meng sana tunawavumilia sana bt hamtambui hilo..!! Badiliken hakuna mwanamke jeuri kwa mwanamme anayemjali na kumpenda kwa dhat kwa kumwonyesha mapenzi ya kweli..ndo maana Mungu alisema mtupende na sisi tuwaheshimu..usipo mpenda mwanamke usitegemee kuheshimiwa hata siku moja that's the real fact
 
Well said..!! Tatizo la wanaume mnajiona very sent wakat in real sense mnamadhaifu meng sana tunawavumilia sana bt hamtambui hilo..!! Badiliken hakuna mwanamke jeuri kwa mwanamme anayemjali na kumpenda kwa dhat kwa kumwonyesha mapenzi ya kweli..ndo maana Mungu alisema mtupende na sisi tuwaheshimu..usipo mpenda mwanamke usitegemee kuheshimiwa hata siku moja that's the real fact

Usituweke wanaume wote kwenye tenga moja.

Wengine tunajielewa na kuyatambua madhaifu yetu bila hata kuambiwa.

Vilevile, si wanawake wote wanaoyatambua na kuyakubali madhaitu yao. kuna wengine ni wabishi kupita maelezo na huwa hawajioni kuwa wana madhaifu.

Haya masuala hayana jinsia. Ni masuala ya kiubinadamu zaidi kuliko jinsia mahsusi ya mtu.
 
Ukute mdada wa kichaga na ana advanced diploma au bachelor degree ya kuunga unga kaSoma zake Topic za Gender kwenye DS. Ukajichanganya ukaoa. Utajuta.
 
Miaka 6 bado sana bwana mdogo,women are slow learners, as time goes atakuelewa tu,kikubwa usichoke kutoa maelekezo unavyofikiri ni sahihi,pili huenda naye anaishi kwa kadiri ya gia uliyotumia kumuingia hapo mwanzo.tatu Tabia ikiendelea washirikishe baadhi ya ndugu zake anaowaheshimu ili wakusaidie pia,usijaribu katu kuwahusisha ndugu zako.
 
Mwanaume au mumeo si mtu sahihi wa kwenda nae ligi hata siku moja mtazamo wangu hata Kama kakufanyia ubaya we tafuta njia tu ya kutafuta amani ya moyo wako ila sio eti kafanya hivi na mimi nafanya vile utaumia ww.

Just take care of yourself maradufu tu oga hata Mara kumi fundisha watoto wako kuna ving vya kufanya Kama mwanamke zaidi ya kuleta ligi na mwanaume
Ligi ndio zinapelekea mpaka ndoa zinavunjika..
Lakin watu haelewi hilo.. na baadhi ya wanawake wanataka kuota oembe ndabi ya nyumba
 
hebu mtupishe, kuna watu wanavumilia kwenye ndoa kama wanawake? tena sio kumvumilia mume tu, unamvumilia mume, wakwe, mawifi na mashemji, tatizo lenu wanaume mnapenda kuabudiwa na hizo zama za mama zetu na bibi zetu zilishapita na wao walikuwa na haki ya kuwanyeyekea sababu walikuwa wanakaa tu nyumbani kazi kuu ni kuzaa na kulea na kumuhudumia mume, sasahv nimwendo wa sawa kwa sawa, haiwezekani wote tunatoka asubuhi kila siku tunarudi wote jioni mwisho wa mwenzi wote tunaleta mezani mishahara, alafu utake kujifanya mfalme wa nyumba. Maisha ya sasa ni kusikilizana na kuelewana kiustaarabu tu nyumba itaenda ila ukileta ubabe kweli ndoa utaiona chungu
mwanamke kama wewe!!!hata kama nimekuoa ndani ya wiki unaenda kwenu, nyie ndio mnasababisha hata maadili ya watoto kuporomoka na hata heshima ndani ya nyumba isiwepo
 
mwanamke kama wewe!!!hata kama nimekuoa ndani ya wiki unaenda kwenu, nyie ndio mnasababisha hata maadili ya watoto kuporomoka na hata heshima ndani ya nyumba isiwepo
kibaya kipi hapa niliachoandika mpaka utokwe povu hivyo?
 
Wanawake tunaooa sasa hivi ni watoto wa Wazazi wa kidigitali. Hakuna malezi wala makuzi ya kuheshimu na kutii ndani ya ndoa. Ukienda kuchumbia mapokezi ya Kiwango cha Lami, kumbe wanajua umekuja kuwaondolea aibu ya mtoto wao kukwama ndani..... Utakapooa sasa ndo utajiuliza hivi huyu alitokea mlangoni au dirishani.???

Na nyie wanawake Muwe na akili ya kutofautisha ndoa na harusi. Na Mjue kuwa harusi ni ya siku moja ndoa ni kitu cha maisha. Mnavyojiandaa kwenye harusi mngekuwa mnajiandaa hivyo kwenye ndoa mambo yangekuwa murua kabisaa.... Ila kinyume chake ndoa zimekuwa kiwanda cha kutengeneza wajane tu. Maana wanaume wanajifia hovyohovyo. Pumbavu kabisa.
 
Back
Top Bottom