Hakuna ndoa isiyokuwa na matatizo, na bahati nzuri hayo matatizo ndo rutuba ya kuidumisha, ila hakuna sumu kubwa ya ndoa kama kusuluhishwa na watu mkiwa na mgogoro, matatizo ya ndoa hutatuliwa na wanandoa wenyewe, mkishamshirikisha hata mzazi tu juu ya ugomvi wenu mnapalilia kuivunja ndoa yenu. Hakuna mwalimu wa ndoa, hakunaga wala hatakuwepo.
Mkuu hili umeongea ni kweli kabisa yani ukweli mtupu, mimi huyu wangu tunatibuana mpka analia inafikia hatua mtu anataka kuondoka usiku usiku kwenda kwao namwambia nenda, ila akiwa anatoka namwonea huruma namfata namwambia lala utaondoka asubuhi ,nikimrudisha tu ,namsema weeee anabaki analia ,akianza sasa kumwaga fact najikuta naumia sana ,anaanza sasa kuniambia:
" Baba Stecy tukiachana mm na wewe mtoto etu atapata shida sipend kumuona mwenetu anateseka kwasababu ya upumbavu wetu ,kama isingekuwa mtoto mm hata usiku uu uniembie niondoke ntaondoka ila ujue nakupenda sana ,ww ndio mme wangu siwezi acha kukwambia uo ukweli, na unajua ni jinsi gani nakupenda ,najua nimekuumiza mme wangu ila nisamehe sana naomba nipe nafasi nyingine tena nirekebishe hya mambo yanazungumzika……. Huku analia… .,,dah unakuta hasira zilikuwa zimenikaba mpka machozi yananitoka kwa hasira ,akishasema hvyo najikuta naanza kuwaza hv kweli nataka kumuacha huyu mwanamke then badae nije niwe na mwingine af anitesee mwanangu af aje anifanyie jambo kubwa kuliko hili ntafanyaje? Hv siitakuwa aibu kurudi kumwomba msamaha turudiane?? Na je nikirudi kumwomba msamaha turudiane af nikute ameolewa na lijamaa lingine af mwanangu apate shida ,sasa nkitaka turudiane ukute upendo ushahama kwa jamaa,… dah nikishawaza hayo nashikwa na uchungu sana af naanza kujitathmini na mm nasema nilifanya kosa hili akanisamehe ,nilimcheat af hakujua ,dah najikuta naanza kumbembeleza yaishe, asubuhi anaamka anafanya usafi kazi zote ananiandalia chai af ananifata kitandani ananiamsha ,mme wangu majia ya kuoga tayari ila nna maongezina ww kabla ujaenda kuoga,,,
" mme wangu najua nimekukosea sana nisamehe nikuaidi sitarudia tena ,najua mm ni binadamu nilifanya either kwa kutokujua ,naomba tuanze upya mpenz wangu… ..
Yani ndio nazidi kurojoka najikuta nmkumbatia namwambia nimekusamehe ,sawa nakuomba usifanye tena kitu kama hicho. Apo macho yamemvimba kwakulia usiku kucha ..
Any way nadhani kila mtu ana njia yake yakusuluhisha magomvi ya ndani kwake mm nashujuru nimepewa mke wa tabia hiyo ya kuomba msamaha kwa namna hiyo pindi anapokosea ,namshukuru Mungu kwa mtu huyu ,mm mwenyewe namkosea sana ila ananifundisha kitu. Usipende kupeleka magomvi kwa mtu mwingine labda mkishindwa kabisa kabisaaaaaaa
Nawasilisha