Ndalilo
JF-Expert Member
- Jan 30, 2013
- 3,343
- 7,516
hebu mtupishe, kuna watu wanavumilia kwenye ndoa kama wanawake? tena sio kumvumilia mume tu, unamvumilia mume, wakwe, mawifi na mashemji, tatizo lenu wanaume mnapenda kuabudiwa na hizo zama za mama zetu na bibi zetu zilishapita na wao walikuwa na haki ya kuwanyeyekea sababu walikuwa wanakaa tu nyumbani kazi kuu ni kuzaa na kulea na kumuhudumia mume, sasahv nimwendo wa sawa kwa sawa, haiwezekani wote tunatoka asubuhi kila siku tunarudi wote jioni mwisho wa mwenzi wote tunaleta mezani mishahara, alafu utake kujifanya mfalme wa nyumba. Maisha ya sasa ni kusikilizana na kuelewana kiustaarabu tu nyumba itaenda ila ukileta ubabe kweli ndoa utaiona chungu
Soma maneno mekundu kama sentensi moja, hayo ndio mawazo yako bila kuremba remba. Aliyeitengeneza hii DUNIA aliitengenezea na INSTRUCTION MANUAL yake, kama inasema hivyo unavyowaza, basi uko sawa.