Kuishi na mke kunataka uvumilivu wa chuma

Kuishi na mke kunataka uvumilivu wa chuma

Tatizo kubwa ambalo hatulifahamu.

Mwanaume anatamani kwanza ndio mapenzi kwa ampendae hufuata.
Mwanaume atatamani umbo zuri na sura nzuri ya mwanamke na baada ya hapo anaweza kumuoa huku bado anatamani na hajapenda bado.
Na kwakuwa wanamke wengi wanaona kilele cha mafanikio yake nikuolewa ataishi kipindi hicho kabla ya kuolewa na miezi michache baada ya kuolewa kwa tabia na maisha ya kuigiza.

Nini hutokea
Mnapooana mwanamke kwake inamaana amefikia kilele cha mafanikio ya maisha yake baada ya kuolewa mwanamke alokuwa anaigiza ataanza kuishi maisha yake halisi atatoka kwenye maigizo na mbaya zaidi wanafundishana baadhi yao kuwa kuwa kumdhibiti mume ni kutawala sita kwa sita huku wakifundishwa na makungwi walosindwa himili ndoa zao na bila kujua tendo lile linachangia asilimia 5 tu ya mapenzi.
Nakwa akili ya baadhi yao wanakuwa bize na muonekano wa upendezao wa nje yaani umbo bila kuwa na muoneka wa vyote viwili umbo na kujitoa kwa nafsi kwa ajili ya mumewe.
Sasa watu wakioana wataishi pamoja hapa ndio muda wa kuliona umbo la mkeo kila siku likiwa wazi na kwakuwa wanawake wengi wanawekeza kwenye muonekano wa nje kuna kipindi inafikia wakati mwanaume anazoea hilo umbo na kuona hakuna kipya kwa mwanamke husika ni katika stage hii mwanaume anaanza kutamani wengine walo nje. Kama huamini hili linganisha mwanaume anavyokuwa wakati akimfukuzia mwanamke kabla ya kumvua nguo na anavyokuwa baada ya kumvua nguo.
Nini kifanyike
Mapenzi hujengwa baada ya umbo kwa sababu umbo lipo kwa ajili ya kutamaniwa mapenzi hujengwa na vitu ufanyavyo kwa umpendaye baada ya umbo lako. Ukisikia ndugu wa mume wanamuwekea ngumu mume kukupa talaka au wanakutetea au ukikuta mume anasimama kukutetea ukiwa umekosea na kukuombea msamaha ujue kunaunayoyatenda ya kumvutia nje ya umbo lako.
Mwanamke jiulize unalipi umelitenda nje ya umbo lako kumvutia mumeo litakalo mfanya akukumbuke siku nzima ya leo?
Tafakari chukua hatua usipochukua hatua utakesha kwa waganga, misikitini na makanisani bila kusahau maombi ukiiombea ndoa yako kutokee muujiza.

Natumai mada hii itasaidia

Haha kutwanga hakuna kazi ujue utachungaje gari lisosukani dada abiria tutapandaje
 
wanawake nao wanatofautiana hasa ukizingatia kila mmoja ana makuzi yake,mimi kuna kaka yangu mmoja kaoa mwanamke wa kipare aisee yule mwanamke ana heshima, akiongea na mume wake ni kwa sauti ya upole haswa,msafi ,anajua mapishi ,ni mwenye upendo na watu wote hakuna jirani asiyempenda pale anapokaa ,ni muajiriwa na vishilingi anavyo ila bado heshima ya mumuwe iko palepale,vya ndani sivijui ila kiukweli wazazi wa huyu mwanamke wanastahili kupewa tuzo ya heshima na huyu bro. kama umeoa kichomi pole mkuu kuna watu wamebahatika kupata wake haswa
 
Huyo bro atulie na mkewe sasa asianze kurukaruka akamchafua moyo mkewe.
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]Nimecheka sana ila wacha niuguze yangu kwanza
Huyo aliyesema kuhusu kyela naunga mkono hoja niliwahi kuwa na mchumba toka pande hizo kuna muda niliishi naye hakuna rangi nilikosa ona. Niliamua hata mahari siidai nikaingia mitini maana niliona hapa nikujitaftia lawama.
 
Haaaaaah noma sana Mimi nmekosa pesa katika ndoa yangu aisee acha tu usiku naona jua linawaka
 
Ndoa yangu ina umri kama ya kwako.

Mwanzo tulisumbua sana, kisa hataki kufanya ninavyotaka mimi. Na niseme ukweli hiki ni kitu kinatutesa sana wanaume tunasahau wanawake ni binadamu pia wanye sifa zote za kibinadamu wakati wewe unataka aishi unavyotaka wewe yeye pia anataka uishi atakavyo yeye, magari yanagongana.

Baada ya kuligundua hilo nilikaa nae chini tukazungumza serious jamii tuliyopo inataka mwanamke aishi vipi na mme, yapi anayaweza yapi hayawezi, yapi nayaweza yapi siyawezi, zipi anadhani ni haki zake, zipi anadhani ni haki zangu na mimi pia nikamweleza tukachora msitari.

Nikienda kinyume ananilaumu na nimejifunza kukubali ikiwa nipo nje ya msitari yeye pia hivyohivyo naona kwa sasa mambo yanasonga.

Kama shetani mwingine hataingia hapo katikati pengine tukazeeka pamoja.

Nimejifunza kutambua madhaifu yake (yasiyo ya maksudi) najitahidi kuyaziba kwa moyo mkunjufu na yeye halalamiki kuna mambo amegundua ni mapungufu yangu anajitahidi kuyaziba.
Bro mta dumu.
 
Mwanaume ili uishi na mwanamke inabidi uwe mwanamke na ubaki kuwa mwanaume.

Unatakiwa ubalansi hzo pande
 
Back
Top Bottom