Kuishi na ndugu wa mume

Kuishi na ndugu wa mume

Mapema yote hiyo hata ndoa bado
Asipoangalia hata ndoa yenyewe ataikosa, maana atamwambia mama yake anateswa
na mchumba wa uncle, dada mtu atavuruga uchumba amwambie tu hapana
 
dah inachanganya hii kiasi...sina hakika kama nimeelewa inavotakiwa labda nirudie maara mbili au tatu
 
kuna mdogo wangu anamchumba wake ambae process zote za kuoana tayar japo jamaa kaomba hajajipanga kufunga ndoa sasa hv uchumi haujakaa sawa anaomba amchukue kwanza ndoa baadae

bint amepanga kwake mkoa tofauti na jamaa sasa jamaa kamuomba akae na mtoto wa dada binti kamaliza form 4 mwaka huu. hataki kurudi kijijin hivyo akae kwa bint siku ya kuolewa ikifika wataenda pamoja kw a jamaa maana jamaa hawez kukaa na ndugu yake kwa sasa anataka kuchukua likizo hivyo akae kwa bidada mpaka akitaka kuolewa ndio atamchukua binti anasema kukaa nae sio shida Ila tabia zake ndio shida

Alishawahi kukaa nae anavitabia flan vinakera hana heshima wala uoga anaweza maliza kuoga akachukua nguo yako akavaa bila kuomba yaan anavitabia tu vya ajabu ajabu ukimgombeza kidogo anaanza kulia, alishakaa nae mwez 1 alihisi kuumwa sasa hv anataka aje akae mda wote mpaka atakapo pata maisha yake,

anashindwa amjibuje mchumba wake anaogopa kukataa ataonekana hapend ndugu bado mapema na akikubal anahisi changamoto kubwa bora angekua anakuja kusalimia tu kuliko kuishi nae siku zote
anaomba ushaur afanyeje au amjibu mini jamaa?
Pole sana rafiki
 
Back
Top Bottom