Kuitana 'babe' kwenye mahusiano ni utoto na mwanzo wa kukosa kuheshimika, hasa kwa mwanamme

Kuitana 'babe' kwenye mahusiano ni utoto na mwanzo wa kukosa kuheshimika, hasa kwa mwanamme

Naona wanaume wenzio wanakushambulia kwelikweli. Lols

Mi wa kwangu juzi nilimuuliza anapenda nikimuita nani zaidi akajibu yote mazuri, doh!
Wa kwako bado ni mpya, kila kitu kizuri kwa stage hiyo.
 
Se
Imagine mwanamme unaitwa babe sijui baby, yaani mtoto?

Hii sio kweli.

Kwa mwanamke ni sawa, sababu hata kwa kiswahili tunawaita watoto yaani 'totoz' au 'bebez'.... kwa mwanamme ina maana gani?

Kama ni kwa mahaba, basi iishie siku za mwanzo tu za uchumba ile kudanganyia.... ukishanasa haina maana tena na sio heshima.

Mkeo akuite kwa heshima na hadhi yako, majina yanayosadifu mamlaka yako ndani ya nyumba.

Bwana, baba au mume na mengine ya kufanana hivyo kwa lugha yoyote yatumike sana.

Japo mapenzi ni utoto, ila familia haihitaji mapenzi tu bali heshima na wajibu kuijenga.... huwezi kumtiisha mtu anayekuita 'mtoto'.

Ncha Kali

Sema tu umevurugwa na mkeo acha kuzunguka
 
Back
Top Bottom