DR HAYA LAND
JF-Expert Member
- Dec 26, 2017
- 23,928
- 63,499
Sasa unaposikia kelele za 'mwizi' kwanini usijiridhishe kwanza,matokeo yake mnaua watu bila hatia,dhamira inabaki inawachoma mioyoni?Siku ukiibiwa utaona kuita mwizi ni option sahihi pia.
Siku yako ikifika hauwezi kuchomoka regardless ya sababu, sote ni wapita njia
Kuna ukweli mwingi kwenye hiliWatu wengi wana Stress za maisha tu hivyo wanamalizia hasira kwa wengine.
Niliwahi kuokoa mtu anapigwa karibu afe na hana hatiaKweli ni ushamba,wengine wanamengi ya kusimulia
Mwaka gani hiyo? Nilikuwa naishi huko tukawa na same case nikiwa first year, kijana kidogo auliweNi tabia ya kishenzi sana, hata kama mmejaaliwa kuwa na roho mbaya na kutamani kuua watu basi angalau msikilizeni huyo mtuhumiwa.
Kisha msikilizeni na anayedai kuibiwa. Miaka ya nyuma kidogo pale mabibo hosteli kuna dogo aligombana na demu wake basi demu akamwitia mwizi, acha kijana ale kipigo. Angalau wale watoto wa chuo walikumbuka kumhoji kabla hawajamuua, wakagundua ni mwenzao kabisa na amezushiwa tu.
Kama sio 2014 basi 2015.Mwaka gani hiyo? Nilikuwa naishi huko tukawa na same case nikiwa first year, kijana kidogo auliwe
2015 naikumbuka hii issue....Kama sio 2014 basi 2015.
Mimi ndugu yangu ilibaki nusu apigwe vibaya mbagala kisa Mama mmoja aligundua kuwa anatoka na Mwanae ambaye mwanafunzi akamkodia wahuni wachache wakamtarget njiani akiwa kabeba Flat screen yake akapigiwa kelele za mwizi dakika chache raia wakamzunguka kipindi kikaanza , ila bahati nzuri alifuatana na kijana mmoja akawa analia huku akipiga kelele wamuache sio mwizi hapo ndio ikawa salama yake japo aliumia kidogo.Siku ukiibiwa utaona kuita mwizi ni option sahihi pia.
Siku yako ikifika hauwezi kuchomoka regardless ya sababu, sote ni wapita njia
Ndio.Umemuelewa mtoa mada?
Comment yangu, nimegusia kuwa. Siku yako ikifika hauwezi kuizuia.Na wewe siku ukisingiziwa wizi ndo utajua umuhimu wa hoja iliyoletwa jukwaani.
Kuna tatizo sehemu ndio maana neno "Mwizi" limeanza kutumika kama silaha rahisi ya kuangamiza.Sasa unaposikia kelele za 'mwizi' kwanini usijiridhishe kwanza,matokeo yake mnaua watu bila hatia,dhamira inabaki inawachoma mioyoni?
Hizi tabia za kuitia watu jina la wezi,niliiona hata chuoni,mdada anapiga yowe kua MWIZI... kumbe huyo siyo mwizi,wameshindwana tu.
MTU ameiba unamkatamata then unamsikiliza baada ya hapo unampeleka police wakamalizane naye.