Kuitwa mwizi na wananchi kuanza kushusha kipigo bila kuhoji ni kukosa ustaarabu jamii za Tanzania Bara, Wengi wamesingiziwa na kuuawa / kupata vilema

Kuitwa mwizi na wananchi kuanza kushusha kipigo bila kuhoji ni kukosa ustaarabu jamii za Tanzania Bara, Wengi wamesingiziwa na kuuawa / kupata vilema

Umasikini ndo chanzo cha kuwa na jamii katili Kama hizo.

MTU ameiba unamkatamata then unamsikiliza baada ya hapo unampeleka police wakamalizane naye.

Kuna watu wamefungwa jela kwa makosa Kama haya ya kupiga watu na kuwaua.


Jamii duni na zenye UPEO mdogo wa fikra ndo hufanya haya mambo.
 
Siku ukiibiwa utaona kuita mwizi ni option sahihi pia.

Siku yako ikifika hauwezi kuchomoka regardless ya sababu, sote ni wapita njia
Sasa unaposikia kelele za 'mwizi' kwanini usijiridhishe kwanza,matokeo yake mnaua watu bila hatia,dhamira inabaki inawachoma mioyoni?
Hizi tabia za kuitia watu jina la wezi,niliiona hata chuoni,mdada anapiga yowe kua MWIZI... kumbe huyo siyo mwizi,wameshindwana tu.
 
Ni tabia ya kishenzi sana, hata kama mmejaaliwa kuwa na roho mbaya na kutamani kuua watu basi angalau msikilizeni huyo mtuhumiwa.

Kisha msikilizeni na anayedai kuibiwa. Miaka ya nyuma kidogo pale mabibo hosteli kuna dogo aligombana na demu wake basi demu akamwitia mwizi, acha kijana ale kipigo. Angalau wale watoto wa chuo walikumbuka kumhoji kabla hawajamuua, wakagundua ni mwenzao kabisa na amezushiwa tu.
Mwaka gani hiyo? Nilikuwa naishi huko tukawa na same case nikiwa first year, kijana kidogo auliwe
 
Siku ukiibiwa utaona kuita mwizi ni option sahihi pia.

Siku yako ikifika hauwezi kuchomoka regardless ya sababu, sote ni wapita njia
Mimi ndugu yangu ilibaki nusu apigwe vibaya mbagala kisa Mama mmoja aligundua kuwa anatoka na Mwanae ambaye mwanafunzi akamkodia wahuni wachache wakamtarget njiani akiwa kabeba Flat screen yake akapigiwa kelele za mwizi dakika chache raia wakamzunguka kipindi kikaanza , ila bahati nzuri alifuatana na kijana mmoja akawa analia huku akipiga kelele wamuache sio mwizi hapo ndio ikawa salama yake japo aliumia kidogo.

Kingine kwa Sheria ya Uislamu kupiga mwizi na kuua ni makosa inatakiwa , inatakiwa kuwe na ushahidi wa wazi na afikishwe kwenye vyombo vya Sheria ikiwa.
 
Umemuelewa mtoa mada?
Ndio.

Point ya mleta mada ni kuwa, mtu akiitiwa Mwizi asikilizwe kwanza kabla ya kushambuliwa.

Comment yangu:
Nimemaanisha, kuna situation hasa ukipata kweli mkasa wa kuibiwa, kuita Mwizi itakuwa ni option sahihi, ishu ya kumsikiliza huyo uliyemuitia Mwizi ndio itabaki mikononi mwa watakaomkamata

Hata hivyo, kuhusu kifo cha Mandojo nimesema "siku ikifika hauwezi kuizuia regardless ya sababu hata kama ni ya uongo".
 
Na wewe siku ukisingiziwa wizi ndo utajua umuhimu wa hoja iliyoletwa jukwaani.
Comment yangu, nimegusia kuwa. Siku yako ikifika hauwezi kuizuia.

Hata mimi nikiitiwa mwizi kwa uongo na nikaingia kwenye 18 za raia, itakuwa siku yangu ishafika hiyo, sitaweza kuizuia.

Je, unafikiri ni kwa nini neno Mwizi linatumika kama silaha ya maangamizi? tuweke neno "kusikiliza, kisikilizwa" pembeni kwanza.
 
Sasa unaposikia kelele za 'mwizi' kwanini usijiridhishe kwanza,matokeo yake mnaua watu bila hatia,dhamira inabaki inawachoma mioyoni?
Hizi tabia za kuitia watu jina la wezi,niliiona hata chuoni,mdada anapiga yowe kua MWIZI... kumbe huyo siyo mwizi,wameshindwana tu.
Kuna tatizo sehemu ndio maana neno "Mwizi" limeanza kutumika kama silaha rahisi ya kuangamiza.

Mtu anajua kabisa akitumia neno jingine ili raia wamsaidie, anaona hatasaidiwa badala yake anaamua kutumia neno MWIZI sababu watu washajua hilo neno lazima liamshe hasira za watu.

Mimi naona mfumo wa kuwaadabisha hawa Wezi kwa kutumia mfumo wa sheria una matobo ndio maana raia wanaamua kumalizana nao moja kwa moja, ndipo sasa hili neno MWIZI likaanza kutumika kama bomu la kuangamiza.

Ni jukumu la kila mmoja kuwa makini na hili neno katika mienendo yake, maana likikuangukia ujue umekwisha.
 
MTU ameiba unamkatamata then unamsikiliza baada ya hapo unampeleka police wakamalizane naye.

Ukimalizana naye ataachiwa na kurudi kuendelea na kazi yake ile ile ya wizi

Ndipo sasa raia hupata hasira na kuona bora wamalizane naye tu, na hapo ndipo neno Mwizi likisikika raia wanaamka kwenda kumalizana na muhusika chap chap.

Laiti hawa wezi wangekuwa wanakomeshwa ipasavyo huko huko Polisi, raia wangekuwa na hamasa ya kuwakamata bila kuwapiga/kuwaua na kuwapeleka huko Polisi
 
Back
Top Bottom