Huo ni mtazamo hasi kabisa, mi ajabu unatak kutwambia kwamba mtu anayejua vitu ni yule mwenye GPA ya 3.5! hii ni ajabu mno.Nakumbuka mzee Nimrod Mkono pamoja na kuwa Advoket anayeheshimika kwa umahili wake aliwahi kuwaambia applikants wa kazi ktk firm yake kwama yeye haangalii GPA kwani hata yeye ana lower second.Lakini hata Jaji mkuu mstaafu Ramadhan aliwahi kuwaeleza wanafunzi aliokuwa anawafundisha pale chuo kikuu cha Zanzibar juu ya yeye kuwa na lower second class.Wanasheria wengi, madaktari na mainjinia hupata lower second kutokana na masomo haya kuwa magumu kidogo, lakini hii haiwazuii kufanya vizuri ktk kazi.Hii inanikumbusha upuuzi uliofanyika pale Udom eti wakati wanashortlist ktk baadhi ya posts walikinzana sana lilipokuja suala la nani apite kati yule wa Mlimani mwenye lower second na wa Makumira mwenye upper second.Hoja ikatoka ktk paneli hiyo ati mtu akasema heri ya C ya mlimani kuliko A ya vyuo vingine.nAKUBALI KWAMBA GPA ina msingi sana kuiangalia sana kwa malengo ya kupunguza watu kama ulivyosema kwamba mlifanya, ila hoja ya kwamba pasipo Upper second haajiriki, hiyo ni hoja hewa.Hata hivyo wapo wanaojua maksi wanazipataje.We fikiria ktk darasa langu la Tax lenye wanafunzi 180 ktk chuo nilichokuwa nasoma demu mmoja tu aliyekuwa anatoka na mwalimu ndiye pekee aliyepata A ya Tax Law, na mabinti wawili marafiki za yule demu ndo walipata B+ wengine tukaangukia B, C, na supplementary za kumwaga.