Ni raha isiyoelezeka kwa urahisi, Roho Mtakatifu anapokujaza. Moyo unakuwa na amani na furaha ambayo dunia haiwezi kukupa. Unahisi uwepo mkubwa wa Mungu ndani yako. Unaanza kunena kwa lugha mpya, na kujiunga na ulimwengu wa rohoni. Unaanza kuwasiliana na Mungu directly.
Kama bado hujajazwa Roho Mtakatifu, anza kuomba ujazwe. Ila ngoja kwanza nikuelezee zaidi faida za kujazwa Roho Mtakatifu na kunena kwa lugha, ili uwe na kiu ya kuomba ujazo wa Roho Mtakatifu.
Ukijazwa, unapata nguvu ya kushinda dhambi na majaribu. Roho Mtakatifu atakupa uwezo wa kuishi maisha matakatifu na kumshinda shetani.
Utapata nguvu ya kushuhudia. Unapojazwa Roho Mtakatifu, unakuwa na ujasiri wa kutangaza habari njema za Yesu Kristo ulimwenguni, na kushuhudia utukufu wa Mungu maishani mwako.
Kunena kwa lugha ni ishara ya kujazwa Roho Mtakatifu. Ukijazwa, utaanza kuomba maombi yenye kina. Kunena kwa lugha kutakuwezesha kuomba mambo ambayo akili yako haiwezi kuyafikiria, kwa kuwa Roho mwenyewe ataomba kupitia kwako.
Kujazwa Roho Mtakatifu na kunena kwa lugha sio hadithi, ni experience halisi ya kiroho, inayoambatana na raha isiyoelezeka. Ni zawadi ambayo Mungu anatupatia sisi watoto wake, ili tuishi kwa ushindi, furaha na ushirika wa karibu naye.
Wakristo wa kwanza walijazwa Roho Mtakatifu siku ya Pentekoste. Wakanena kwa lugha mpya na kupata nguvu ya kuwa mashahidi wa Yesu (Mdo 2:4)
View attachment 3464355
Nanena kama Roho anavyonijalia.Wewe unanena kwa lugha gani? Maana wakati wa Pentekoste, walioongea kwa lugha ngeni, walisikika
Danganya wasio juaNanena kama Roho anavyonijalia.
Siku ya Pentekoste, walipojazwa Roho Mtakatifu, Maandiko yanasema "wakaanza kunena kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia kunena" (Matendo 2:4). Wenyewe hawakusema wanaongea lugha gani, bali waliokuwa wakiwasikiliza ndio walioshuhudia kwamba wananena lugha zao (Matendo 2:6-8). Vivyo hivyo leo, kunena kunaweza kuwa kwa lugha za wanadamu au lugha za rohoni ambazo hazieleweki kwa akili ya kawaida ila ni mawasiliano ya moja kwa moja na Mungu (1 Wakorintho 14:2). Umenipata?
Ngoja nikufafanulie tena: kuna aina mbili za kunena kwa lugha:Danganya wasio jua
Huwa mmepagawa na mapepo
Kunena kwa lugha lazima ueleweke
Siyo kupagawa na mapepo bali ni utimilifu wa ahadi ya Mungu. Hata siku ile ya Pentekoste walikuwepo watu waliodhihaki na kusema: "‘wamelewa kwa mvinyo mpya" (Matendo 2:13), lakini Petro akasimama akasema siyo ulevi, bali ni utimilifu wa unabii (Matendo 2:15-17). Hivyo kunena kwa lugha sio kupagawa na mapepo, ni kazi ya Roho MtakatifuDanganya wasio jua
Huwa mmepagawa na mapepo
Sio kweli, nani kakwambia haya hebu acha maneno ya uzushi unayorishwa na mwalimu wako asiyejua roho mtakatifu anapokuwa ndani ya mtu anakuwa vipi, heti anasikia raha ?Ni raha isiyoelezeka kwa urahisi, Roho Mtakatifu anapokujaza. Moyo unakuwa na amani na furaha ambayo dunia haiwezi kukupa. Unahisi uwepo mkubwa wa Mungu ndani yako. Unaanza kunena kwa lugha mpya, na kujiunga na ulimwengu wa rohoni. Unaanza kuwasiliana na Mungu directly.
Kama bado hujajazwa Roho Mtakatifu, anza kuomba ujazwe. Ila ngoja kwanza nikuelezee zaidi faida za kujazwa Roho Mtakatifu na kunena kwa lugha, ili uwe na kiu ya kuomba ujazo wa Roho Mtakatifu.
Ukijazwa, unapata nguvu ya kushinda dhambi na majaribu. Roho Mtakatifu atakupa uwezo wa kuishi maisha matakatifu na kumshinda shetani.
Utapata nguvu ya kushuhudia. Unapojazwa Roho Mtakatifu, unakuwa na ujasiri wa kutangaza habari njema za Yesu Kristo ulimwenguni, na kushuhudia utukufu wa Mungu maishani mwako.
Kunena kwa lugha ni ishara ya kujazwa Roho Mtakatifu. Ukijazwa, utaanza kuomba maombi yenye kina. Kunena kwa lugha kutakuwezesha kuomba mambo ambayo akili yako haiwezi kuyafikiria, kwa kuwa Roho mwenyewe ataomba kupitia kwako.
Kujazwa Roho Mtakatifu na kunena kwa lugha sio hadithi, ni experience halisi ya kiroho, inayoambatana na raha isiyoelezeka. Ni zawadi ambayo Mungu anatupatia sisi watoto wake, ili tuishi kwa ushindi, furaha na ushirika wa karibu naye.
Wakristo wa kwanza walijazwa Roho Mtakatifu siku ya Pentekoste. Wakanena kwa lugha mpya na kupata nguvu ya kuwa mashahidi wa Yesu (Mdo 2:4)
View attachment 3464355
Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa, mungu ni wa utaratibu kunena kwa lugha maana yake ni kuongea lugha inayoeleweka kama kristo na kufundisha wengine na sio shakakakakakakkaka vitu ambavyo kwenye biblia hakuna.Ngoja nikufafanulie tena: kuna aina mbili za kunena kwa lugha:
- Lugha za wanadamu (kama ilivyokuwa Pentekoste) – ambazo mtu mwingine anaweza kuzisikia na kuelewa bila tafsiri, kwa kuwa ni lugha halisi za watu.
- Lugha za rohoni – ambazo si za kibinadamu, bali ni lugha mpya za kiroho kwa mawasiliano ya moja kwa moja na Mungu. Hizi mara nyingi hazieleweki kwa akili ya mwanadamu bila karama ya tafsiri za lugha (1 Wakorintho 14:2, 14-15).
Hakuna kitu kama hicho bali kuweweseka kutokana na uwezo mdogo wa kuchambua na kuhoji mambo.Ni raha isiyoelezeka kwa urahisi, Roho Mtakatifu anapokujaza. Moyo unakuwa na amani na furaha ambayo dunia haiwezi kukupa. Unahisi uwepo mkubwa wa Mungu ndani yako. Unaanza kunena kwa lugha mpya, na kujiunga na ulimwengu wa rohoni. Unaanza kuwasiliana na Mungu directly.
Kama bado hujajazwa Roho Mtakatifu, anza kuomba ujazwe. Ila ngoja kwanza nikuelezee zaidi faida za kujazwa Roho Mtakatifu na kunena kwa lugha, ili uwe na kiu ya kuomba ujazo wa Roho Mtakatifu.
Ukijazwa, unapata nguvu ya kushinda dhambi na majaribu. Roho Mtakatifu atakupa uwezo wa kuishi maisha matakatifu na kumshinda shetani.
Utapata nguvu ya kushuhudia. Unapojazwa Roho Mtakatifu, unakuwa na ujasiri wa kutangaza habari njema za Yesu Kristo ulimwenguni, na kushuhudia utukufu wa Mungu maishani mwako.
Kunena kwa lugha ni ishara ya kujazwa Roho Mtakatifu. Ukijazwa, utaanza kuomba maombi yenye kina. Kunena kwa lugha kutakuwezesha kuomba mambo ambayo akili yako haiwezi kuyafikiria, kwa kuwa Roho mwenyewe ataomba kupitia kwako.
Kujazwa Roho Mtakatifu na kunena kwa lugha sio hadithi, ni experience halisi ya kiroho, inayoambatana na raha isiyoelezeka. Ni zawadi ambayo Mungu anatupatia sisi watoto wake, ili tuishi kwa ushindi, furaha na ushirika wa karibu naye.
Wakristo wa kwanza walijazwa Roho Mtakatifu siku ya Pentekoste. Wakanena kwa lugha mpya na kupata nguvu ya kuwa mashahidi wa Yesu (Mdo 2:4)
View attachment 3464355
Hakuna kitu kama hicho bali kuweweseka kutokana na uwezo mdogo wa kuchambua na kuhoji mambo. Ni sawa na zamani wakatoliki wakiaminishwa kuwa lazima waombe kwa kilatini sawa na waislam na kiarabu.
AMENFaida zaidi za kujazwa Roho Mtakatifu
Unapata ufunuo wa Neno la Mungu. Roho Mtakatifu akijaa ndani yetu anafungua akili na macho ya kiroho ili tuweze kuelewa Maandiko kwa undani na kuyatenda (Yohana 14:26).
Ujazo wa Roho Mtakatifu huzaa tabia ya Kristo ndani yetu na kutuwezesha kuzaa tunda la roho: upendo, uvumilivu, fadhili, utu wema, upole, na kiasi (Wagalatia 5:22-23). Hili ni jambo muhimu katika maisha ya Ukristo.
Roho Mtakatifu akijaa ndani yetu, anaweza kutugawia karama mbalimbali kama vile unabii, uponyaji, neno la hekima, neno la maarifa, imani na miujiza, kupambanua roho, aina za lugha na fasiri za lugha, kwa ajili ya kulijenga Kanisa na kuwahubiri watu wapate wokovu (1 Wakorintho 12:7-11).
Ukijaa Roho Mtakatifu atakuongoza kwenye maamuzi sahihi. Roho Mtakatifu hutoa mwongozo wa kiungu katika maamuzi magumu ya maisha, akitufunulia mapenzi ya Mungu na kutuonya tusije tukapotea (Warumi 8:14).
Roho Mtakatifu anatupatia shauku ya kumwabudu Mungu. Roho Mtakatifu hufanya moyo wa mtu kuwa na kiu ya ibada ya kweli na kumtukuza Mungu kwa moyo wote.
Anatuimarisha katika dhiki na mateso. Ujazo wa Roho humpa mtu ujasiri wa kusimama imara hata katikati ya mateso, dhihaka, au upinzani kwa ajili ya Injili (soma Mdo 7:55-56, utaona mfano wa Stefano).
Roho Mtakatifu anatuandaa kwa utukufu ujao. Roho Mtakatifu ni "mhuri" wa urithi wetu wa milele. Anatupa hakika na tumaini la ufufuo na maisha ya milele (Waefeso 1:13-14).
Hizo ni faida za kujazwa Roho Mtakatifu, ambaye ni Nafsi ya tatu katika Utatu Mtakatifu.
Ndugu yangu mwina97Huwa mmepagawa na mapepo
Mie siuamini kwa vile nina akili kubwa na najua ulipoibuliwa huko Roma ili kuwaibia wajinga sawa na ile stori ya Muhamed kubanwa mbavu kwenye jabali na kusingizia kuwa kashushiwa ujumbe au quran wakati anayosema yalishaandikwa kwenye torati naye akaamua kuchukua na kuyaandika kishairi.Hii ni kauli ya wasioamini Utatu Mtakatifu
Hivyo vifungu vya raha vinazungumzia watu watakao fika mbinguni sio dunianiNdugu yangu mwina97
Ngoja nikudadavulie tofauti iliyopo kati ya mtu aliyepagawa na mapepo na mtu aliyejazwa Roho Mtakatifu:
Dalili za mtu aliyepagawa na mapepo:
Dalili za mtu aliyejazwa Roho Mtakatifu:
- Anapoteza udhibiti wa nafsi. Mapepo humpa mtu nguvu zisizo za kawaida au kumlazimisha kufanya mambo ambayo hataki (Marko 5:3-5).
- Anateseka badala ya kufurahi. Mtu aliye na mapepo huwa na mateso ya ndani, huzuni, hofu, na vurugu, sio furaha na amani.
- Anachafua na kuharibu. Mapepo yanaleta uharibifu wa mwili, akili, na nafsi. Mfano mzuri ni yule kijana aliyekuwa akirushwa na mapepo motoni na majini (Marko 9:22).
- Hutamka maneno ya kukufuru au ya chuki kwa Mungu. Mapepo hayawezi kumtukuza Yesu kuwa ni Bwana (1 Wakorintho 12:3).
- Mtu aliye na mapepo mara nyingi hujitenga na watu, anaishi katika giza na uchafu, kama yule aliyekaa makaburini (Marko 5:2).
- Ana amani na furaha ya kweli kama ilivyoandika katika Warumi 14:17: “Maana ufalme wa Mungu si kula na kunywa, bali ni haki na amani na furaha katika Roho Mtakatifu”
- Ana udhibiti wa nafsi. Anakuwa na tunda la Roho “kiasi” (Wagalatia 5:22-23).
- Anamtukuza na kumwinua Yesu kama Maandiko yanenavyo: “Kwa hiyo nawaarifu, ya kwamba hakuna mtu anenaye katika Roho wa Mungu, kusema, Yesu amelaaniwa; wala hawezi mtu kusema, Yesu ni Bwana, isipokuwa katika Roho Mtakatifu.” (1 Wakorintho 12:3).
- Ana upendo na msamaha. Roho humjaza mtu upendo wa kweli (Warumi 5:5).
- Anakuwa na nguvu ya kuomba na kushuhudia. Mtu aliyejazwa Roho Mtakatifu ana ujasiri wa kumtumikia Mungu (Matendo 1:8).
- Maisha yake hubadilika na kuwa ushuhuda wa wokovu, utakatifu, na baraka kwa wengine.
Ndugu yangu, ukisikia mtu ananena: "shakakakakakakkaka" hayo sio maneno ya kipuuzi, bali ni lugha za rohoni ambazo Biblia imethibitisha. Imeandikwa: ‘Kwa maana mtu yeyote anayesema kwa lugha, hasemi na wanadamu bali anasema na Mungu. Kwa kuwa hakuna mtu yeyote anayemwelewa, kwani anasema mambo ya siri kwa roho.’ (1 Wakorintho 14:2). Hapa Paulo anaonyesha wazi kwamba kuna kunena lugha ambazo akili ya mwanadamu haielewi, kwa sababu ni siri za kiroho mbele ya Mungu.Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa, mungu ni wa utaratibu kunena kwa lugha maana yake ni kuongea lugha inayoeleweka kama kristo na kufundisha wengine na sio shakakakakakakkaka vitu ambavyo kwenye biblia hakuna.
Kama unaamini hivyo vifungu vinazungumzia watakaofika mbinguni; na kifungu hiki je: Mt 11:28-30Hivyo vifungu vya raha vinazungumzia watu watakao fika mbinguni sio duniani