Genius Man
JF-Expert Member
- Apr 7, 2024
- 3,558
- 7,935
Hayo maneno ya siri ndio hayo shabahabahababa ahaba sindiyo ? watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa.Ndugu yangu, ukisikia mtu ananena: "shakakakakakakkaka" hayo sio maneno ya kipuuzi, bali ni lugha za rohoni ambazo Biblia imethibitisha. Imeandikwa: ‘Kwa maana mtu yeyote anayesema kwa lugha, hasemi na wanadamu bali anasema na Mungu. Kwa kuwa hakuna mtu yeyote anayemwelewa, kwani anasema mambo ya siri kwa roho.’ (1 Wakorintho 14:2). Hapa Paulo anaonyesha wazi kwamba kuna kunena lugha ambazo akili ya mwanadamu haielewi, kwa sababu ni siri za kiroho mbele ya Mungu.
Ndiyo maana pia akaongeza: ‘Kwa maana nikiomba kwa lugha, roho yangu inaomba, lakini akili yangu haina matunda. (1 Wakorintho 14:14). Hii inamaanisha kwamba sauti au maneno yanayosikika yanaweza kuonekana kama hayana mpangilio kwa masikio ya kawaida, lakini kwa Mungu ni maombi ya rohoni yaliyo safi kabisa.
Najua kuna baadhi ya watu huwa wanaigiza kunena kwa lugha. Hata hivyo, wanaojazwa Roho Mtakatifu na kunena kwa lugha bila kuigiza, wapo wengi.
Nakwambia kunena kwa lugha na nikuongea kwa ligha flani kwani hakuna maandiko kwenye biblia yanayo onesha hizi tiwa savage tiwasavage shabakabakabaka
Nimekupa reference nitajie mfano wa mtu kwenye biblia aliye ongea lugha kama hizo, hata malaika hawakuwa wayahudi lakini tunaona waliongea na danieli na yesu kwa lugha zinazo eleweka.
Mungu aliongea na musa kwenye mlima wa sinai kwa lugha inayoeleweka sio shabakannkakma, labda kama huu sio uzushi na uchizi nionesha mfano wa aliyefanya hivi ili na uwe ushuhuda kama hakuna vipi kama utakuwa unaongea shabakakakakkaka alafu kumbe ulidanganywa utajuaje ?